Kwa nini kwa miaka 25 idadi ya watu wa Cuba haijaongezeka?

Idadi ya watu duniani iliongezeka katika robo ya mwisho ya karne kwa wastani wa 1.2% kwa mwaka, na kufikia karibu wakazi milioni 8,000.

Hali hiyo ilikuwa sawa huko Amerika Kusini, ambayo tayari inazidi milioni 600.

Isipokuwa katika visa vya vita au hali zingine kali, si kawaida kwa idadi ya watu nchini kutoongezeka au hata kupungua katika kipindi cha miaka 25.

Lakini Cuba si nchi ya kawaida.

Mnamo 1984, kisiwa kilizidi idadi ya ukomo iliyokuwa imewekwa ya wakaazi milioni 10,

Mnamo mwaka 1997 idadi ikafika milioni 11 na baada ya panda shuka nyingi, idadi ya hivi karibuni ya 2021 ni milioni 11.1.

Ni sababu gani zinazoelezea mwelekeo huu usio wa kawaida?

Historia ndogo

‘’Cuba unauliza mtu yeyote anataka kuwa na watoto wangapi na anakuambia watoto 2, na hata utaratibu, kwanza wa kiume na kisha wa kike. Ni uzazi bora ambao unatoka kwa babu na babu zetu wa Uhispania,’’ Juan Carlos Albizu anaelezea BBC World.

Msomi na mwandishi wa tafiti kadhaa juu ya somo hilo anadokeza kwamba, tangu mwanzoni karne ya 20, Cuba imekuwa na tabia tofauti katika idadi ya watu ikilinganishwa na majirani zake wa Amerika Kusini.

‘’Tayari mwaka wa 1900 kuzalia kulikuwa chini ikilinganishwa na Amerika ya Kusini, na watoto wapatao 6 kwa kila mwanamke (huko Mexico, kwa mfano, walikuwa 7 na katika nchi nyingine za eneo hilo idadi ilikuwa hata juu zaidi) na watu walianza kudhani mpango wa kuwa na familia ndogo, ulikuwa mzuri.

Katika nusu ya kwanza ya karne iliyopita, kisiwa hicho kilifikia viwango visivyoweza kufikiwa vya maendeleo kwa nchi zingine za kanda na kupokea wimbi kubwa la wahamiaji wa Uropa, haswa Wahispania.

Sababu zote mbili ziliashiria mwelekeo tofauti wa idadi ya watu.

Kuanzia mwaka wa 1960, kupungua kwa vifo vya watoto wachanga na upatikanaji mkubwa wa huduma za afya na uzazi, miongoni mwa mambo mengine, kulisababisha idadi ya watoto kuongezeka.

Lakini hii haikudumu zaidi ya muongo mmoja: katika miaka ya 1970, kiwango cha watoto 2.1 kwa kila mwanamke ambacho kinahakikisha mbadala wa kizazi kilipungua kwa mara ya kwanza.

Kwa hiyo, mwishoni mwa 1985, mchanganyiko wa uzazi na umri wa kuishi nchini Cuba ulikuwa tayari ‘’sawa zaidi na wastani wa Ulaya kuliko wa Amerika ya Kusini,’’ anasema Albizu-Campos.

Kuzaliwa, vifo na umaskini

Mnamo mwaka 2021, Cuba ilisajili idadi ya chini zaidi ya waliozaliwa, 99,096, na idadi kubwa zaidi ya vifo, 167,645, katika miongo sita iliyopita.

Ingawa idadi ya vifo imeongezeka kutokana na wimbi la Covid-19 lililoathiri nchi, takwimu za kuzaliana zinathibitisha kupungua kwa idadi ya watu.

Leo hii jumla ya kiwango cha kuzaliana ni watoto 1.45 kwa kila mwanamke, chini ya kiwango kuzaa tena kupata mtoto mwingine, na pia wastani wa watoto 2 huko Amerika Kusini kulingana na data ya Benki ya Dunia.

Mwenendo huu unatokea wakati wa mgogoro mkubwa nchini Cuba, ambapo chakula, dawa, bidhaa za afya na bidhaa nyingine za kimsingi ni adimu.

Albizu-Campos anaamini kuwa kile ambacho baadhi ya wasomi wanakiita ‘’Malthusianism of poverty’’ ndicho kinachofanyika kisiwani humo.

Nchini Cuba hadi vizazi 3 au 4 huishi pamoja katika nyumba moja na chakula pia ni shida kupatikana. Hivyo, swali la kwanza ambalo wanandoa wachanga hujiuliza wakati wanataka kupata mtoto ni: nitawezaje kuwalisha? na mara tu hilo likitatuliwa, mtazamo unaanza kuwa sawa. Kwa maneno mengine, leo wanawake wa Cuba wanaona kuzaliwa kwa mtoto mwingine wa pili kama kujiweka katika hatari hasa kwa wale ambao tayari wako katika familia, anasema.

Anasema ‘’hali hiyo ikiendelea kwa muda, uzazi wa wanawake hupungua kama ilivyotokea katika kipindi maalum, wakati wa mgogoro mkubwa uliotokea Cuba baada ya kuanguka kwa USSR katika miaka ya 1990 huku kukiwa na hali ya uhaba mkubwa ikilinganishwa na hali ya sasa.”

Katika kipindi hicho maalum, idadi ya watoto kwa kila mwanamke ilishuka kutoka 1.8 hadi 1.6 na, kwa kuwa ilikuwa janga lililodumu kwa muda, ilibadilisha muundo wa uzazi wa Cuba, anasema Albizu-Campos

Picha: Vijana wengi wa Cuba wanaona Marekani kuwa mahali ambapo wanaweza kutimiza ndoto zao za kikazi na kifamilia.

Uhamiaji

Inakadiriwa kuwa karibu Wacuba milioni moja wameondoka nchini mwao katika miaka 25 iliyopita.

Kati yao, zaidi ya 800,000 wamehamia Marekani, kulingana na rekodi rasmi za nchi hii.

Mtiririko huo wa uhamiaji umekuwa ukisababisha uhamiaji wa watu 30,000 hadi 70,000 kwa mwaka hadi janga lilipoingia.

Lakini ni katika miezi tisa ya kwanza ya 2022, Wacuba 200,000 walifika katika nchi ya Amerika Kaskazini, kiwango cha juu katika historia ambacho kinazidi ule wa uhamishaji wa watu wengi kama ule wa Mariel mwaka 1980 au mgogoro wa boriti katika kipindi maalum.

Wengi walikufariki dunia.

“Ongezeko lisilodhibitiwa la mfumuko wa bei, kupungua kwa thamani halisi ya mishahara na pensheni, uhaba wa chakula, uhaba wa dawa na uchakavu wa makazi, pamoja na mambo mengine, kumepunguza viwango vya ustawi na kufikia viwango vya chini sawa na kipindi hicho lakini vikiwa chini lakini ikiwa na viwango vya chini vya ulinzi wa kijamii na katika mazingira yenye wasiwasi mkubwa wa kisiasa na machafuko ya raia, anaeleza mwanasosholojia Dkt. Elaine Acosta.

‘’Haya yote yanaishia kushawishi maelfu ya vijana na hata wazee kujiunga na mkanyagano wa wahamaji ambao ulianza tena safari za ndege zilipofunguliwa Novemba 2021,’’ anasema.

Idadi ya watu kurejea tena hadi milioni 10

Hii ina maana kwamba, baada ya miaka 25 ya kudumaa, idadi ya watu wa Cuba inaweza kuanza kupungua, hasa ikiwa mtu atazingatia kwamba sehemu kubwa ya wahamiaji ni vijana au watu wa umri wa kuzaa ambao watapata watoto wakiwa nje ya nchi.

Mtaalamu wa demografia Albizu-Campos alitabiri miaka iliyopita kwamba idadi ya watu wa Cuba itarudi kwenye milioni 10 ifikapo 2030, na kizazi kizima watoto waliozaliwa miaka ya 1960 katika uzee.

Hata hivyo, mchakato huo unaonekana kuharakishwa na kupungua kwa milioni 11 kunaweza kutokea mwaka huu wakati sajili itasasishwa na data mpya ya watoto waliozaliwa, vifo na wahamiaji.

‘’Mchanganyiko potovu kati ya uhamiaji endelevu na ongezeko la vifo unaweza kuonyesha kuwa tunakaribia kukabiliana na kizuizi hicho,’’ mtaalam huyo anasema.

Mtazamo wa idadi ya watu ni mgumu zaidi kwa mwaka wa 2050, wakati zaidi ya Wacuba milioni 3.7 watakuwa na umri wa zaidi ya miaka 60 kati ya wastani wa wakazi milioni 10.1, kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa.

Kati ya hawa, karibu milioni 1.3 watakuwa wazee zaidi ya miaka 80.