Leopard 2: Kwa nini Ukraine inasisitiza kupatiwa kifaru hiki cha Ujerumani?

Ukraine inayashinikiza na kuyaomba mataifa ya magharibi kuipatia silaha nzito nzito hususan vifaru vya kisasa ili kuiwezesha kukabiliana na uvamizi katika taifa hilo uliotekelezwa na Urusi katika mstari wa mbele wa vita.

Urusi inadaiwa kuimarisha ulinzi wa jeshi lake katika maandalizi ya kuendeleza uvamizi wake wakati wa majira ya baridi.

Baada ya miezi kumi na moja ya vita kati ya Urusi na Ukraine, Idadi ya vifaru vilivyokuwa vikitumiwa na jeshi la Ukraine vilipungua kutokana na hasara lililopata jeshi lake katika vita mbali na hatua ya kuviondoa vitani kutokana na ukosefu wa vipuri kwasababu idadi kubwa ya silaha za Ukraine kabla ya uvamizi wa Urusi nchini humo February iliopita zilitoka Urusi na ni Urusi pekee ndio ilivyo na vipuri vyake.

Kabla ya vita hivyo, Ukraine ilikuwa na takriban vifaru 900 kutoka Usovieti, kama vile kifaru cha T-72, T64 pamoja na vile vilivyokuwa vikimilikwa na mataifa yaliojiunga na NATO yalioipatia takriban vifaru 200 aina ya T-72 vilivyokuwa vikimilikiwa na usovieti ambavyo vilishirikisha vile vya mataifa ya Ulaya mashariki.

Urusi ilianza vita hivyo ikiwa na takriba vifaru 3000 vya kisasa ,na ilipoteza mamia ya silaha hizo mwanzoni mwa vita , kufuatia mashambulizi ya silaha za kukabiliana na vifaru zilizotolewa na mataifa ya magharibi.

Vikosi vya Urusi vilifika kwenye viunga vya mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, lakini vilijiondoa na kuyahamisha maeneo hayo ili kuelekeza nguvu zake za kijeshi mashariki mwa Ukraine, haswa majimbo ya Donetsk na Donbass.

Vikosi vya Urusi vilitumia mbinu mpya katika vita vya huko, kwani viliepuka makabiliano ya moja kwa moja na vikosi vya ardhini vya Ukraine, na kuamua kushambulia miji na maeneo kabla ya vikosi vya ardhini kuvamia.

Mzigo wa kimkakati

Vifaru vilivyopo vitani vinahitaji uangalizi wa hali ya juu kutokana na changamoto vinvyopitia , na urekebishaji wake maalum hufanyika mbali na eneo la mstari wa mbele wa vita.

Vifaru vya Ukraine, ambavyo ni vya miaka ya sitini na sabini ya karne, vinakabiliwa na mkwamo na matatizo mengi kutokana na kutelekezwa kabla ya vita. Kifaru ambacho kinahusika sana katika vita nchin Ukraine leo ni Soviet T-64, ambacho kilianza kutumika karibu nusu karne iliyopita.

Ukraine inasema inahitaji vifaru 300 vya kisasa vya Magharibi, kwa lengo la kuwatimua wanajeshi wa Urusi wakati wa majira ya kuchipua kutoka katika maeneo ambayo imekalia tangu mwanzo wa vita.

Dkt. Jack Watling wa Taasisi ya Royal ya Huduma za Uingereza anaamini: "Vikosi hivi vichanga vinahitaji vifaru hivi ili kupenya mistari ya ulinzi ya Kirusi, ambayo inalindwa vyema na Vifaru."

Uingereza ni nchi ya kwanza kutoa vifaru vya kivita kwa Ukraine, kwani Waziri wa Ulinzi Ben Wallace alithibitisha kutoa vifaru 14 vya Challenger 2 kwa Ukraine.

Ingawa vifaru hivi vinaweza kuwa na ufanisi katika uwanja wa vita, vinaweza kuwakilisha mzigo wa vifaa kwa Ukraine kutokana na idadi yao ndogo na matumizi ya risasi zao ambazo hazilingani na vipimo vya NATO au vifary vya Urusi vinavyomilikiwa na Ukraine.

Jeshi la UKraine lazima lianzishe mtandao wa usambazaji wa vifaru hivi ili kuvipa risasi zinazohitajika wakati wa vita, na pia kuvipatia urekebishaji mzuri iwapo utahitajika .

Serikali ya Uingereza lazima itoe hitaji la vifaru hivi, ikiwa ni pamoja na risasi na vipuri, na kuvihamishia Ukraine bila kukatizwa.

Marekani na nchi za Ulaya zimeahidi kuipatia Ukraine silaha nzito

Marekani na Ujerumani zinakaribiana na Ufaransa kusambaza magari ya kivita kwa Ukraine

Kwa nini Leopard 2?

Kifaru cha Leopard ndicho chaguo bora kwa Ukraine, kwani ndicho kinachotumika sana na kimeenea zaidi kati ya nchi za Ulaya ambazo ni wanachama wa NATO, kwani kwa sasa kuna zaidi ya vifaru 2,300 ya mifano mbalimbali inayotumika katika majeshi ya nchi hizi na inaweza kwa urahisi kusafirishwa hadi katika ardhi ya Ukraine.

Kifaru hiki kinatumia risasi za NATO, na risasi hizi zinaweza kupatikana kwa idadi inayofaa kutoka kwa nchi yoyote ya NATO, pamoja na nchi hizi kuwa na idadi kubwa ya risasi hizi, na vifaru vya Marekani aina ya M1 Abrams ambavyo pia hutumia risasi sawa na Leopard 2, na kwa hivyo Marekani inaweza kutoa risasi za vifaru hivi.

Ingawa mfano wa kwanza wa kifaru cha Leopard uliingia katika huduma zaidi ya miongo minne iliyopita, ilipata michakato mingi ya maendeleo na ya kisasa, na kuwa mojawapo ya kifaru bora zaidi ulimwenguni kwa suala la usahihi wa kutumia, ulinzi na wepesi. Inatumiwa na majeshi ya nchi 18 kote duniani, ikiwa ni pamoja na Qatar, Singapore, Indonesia na Chile. Canada, pamoja na majeshi mengi ya Ulaya.

Uzoefu huo pia ulithibitisha kuwa ni wa kuaminika kwenye uwanja wa vita kwa sababu ya ukosefu wake wa milipuko ikilinganishwa na vifaru vingine.

Uturuki inamiliki mamia ya vifaru vya Leopard 2 na ilivitumia katika operesheni zake za kijeshi dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi katika eneo la Afrin mwaka 2018 na mwaka 2016 dhidi ya wanamgambo wa "Dola la Kiislamu" huko Jarabulus na al-Bab.

Jeshi la Uturuki lilipoteza vifaru kumi vya aina hii katika vita vya mji wa Al-Bab dhidi ya wanamgambo wa kundi lenye itikadi kali, jambo ambalo liliwakilisha aibu kubwa kwa jeshi la Uturuki ambalo siku zote limekuwa likijivunia nguvu na uimara wake. .

Baadhi ya wachambuzi walihusisha hasara hizi na mafunzo duni ya wanajeshi wa Uturuki na utendakazi wa makosa ya kimbinu, kwani vifaru hivi havikusudiwi kuendeshwa katika vita vya mitaani dhidi ya majambazi wanaovizia magari hayo mazito na ya gharama kubwa katika vichochoro na barabara za pembezoni ili kuwakabili kwa makombora ya kuzuia tanki au vifaa vya vilipuzi.

Jaribio la Ugiriki la vifaru vya Leopard 2, Abrams M1, British Challenger 2, French Leclerc, na Russian T-80 lilionyesha kuwa vifaru vya a Leopard na Abrams vilifikia lengo lake wakati walikuwa katika mwendo kwa asilimia 100 katika raundi ishirini, huku vikiafikia malengo yake dhidi ya Kifaru cha Soviet cha T-80

Wataalam wengi wanaamini kuwa Leopard 2 inalinganishwa na kifaru cha Marekani cha Abrams M1 katika suala la utendaji, usahihi wa mashambulizi, kasi na uwezo, na labda tofauti pekee kati yao ni kwamba kifaru cha Abrams kina vifaa vya injini ya ndege inayoendesha na mafuta ya taa kama ndege na hutumia mafuta mengi, ambayo hufanya kazi yake kuwa ndogo sana kuliko ile ya leopard. Ingawa nguvu ya injini zote mbili zina horse power 1500.

Saudi Arabia ilitaka kununua kati ya vifaru 400 hadi 800 vya Leopard 2 kwa mkataba wa thamani ya dola bilioni kadhaa, lakini serikali ya Ujerumani ilikataa kufanya hivyo kwa sababu ya rekodi ya Saudi Arabia katika uwanja wa haki za binadamu na uingiliaji wa Saudi nchini Bahrain, hivyobasi ikaamua kununua vifaru 400 vya Abrahams kwenye hifadhi yake ya awali ya vifaru.

Mfano wa hivi punde zaidi wa Leopard 2 ni A7+ , ambacho ni kifaru cha kizazi kijacho cha jeshi la Ujerumani. Kina uzani wa tani 67.5 na mfumo wa ulinzi wa hali ya juu dhidi ya makombora na moto ulioelekezwa. Vilevile mwili wake hutoa ulinzi dhidi ya mabomu ya ardhini, vifaa vya vilipuzi vinavyoongozwa, mabomu ya kurushwa kwa roketi kama vile RPG na makombora ya kukinga vifaru.

Silaha kuu katika kifaru hicho ni bunduki ya 120 mm kulingana na viwango vya NATO, pamoja na bunduki ya mashine ya 7.62 mm, kirusha mabomu cha mm 40 au bunduki nyingine ya mashine ya A.50, pamoja na mabomu ya moshi kwa lengo la kujificha kutoka kwa macho ya adui.

Kamanda wa anaweza kuona mchana/usiku kutokana na mfumo wa upelelezi wa umbali mrefu, kamera ya joto, mfumo wa kuona usiku unaojitegemea, kifaa cha kupimia umbali wa leza, na vifaa vingine vya hali ya juu.

Kasi kuu ya kifaru hicho

Kasi ya juu ya kifaru hicho ni kilomita 72 kwa saa na uwezo wake wa kufanya kazi ni Kilomita 450 kwa saa.