Ujerumani ndio yenye uwezo wa kumnyamazisha Putin - The Guardian

Makala katika gazeti la Guardian liliishauri serikali ya Ujerumani kuipatia Ukraine vifaru, hasa vifaru vya Leopard, ili kukabiliana na Urusi.

Mwandishi Timothy Garton Ash alisema: "Ikiwa Ujerumani kweli itajifunza kutoka kwa historia yake, ingetuma vifaru kuilinda Ukraine."

Mwandishi huyo aliongeza kuwa Ujerumani inabeba dhima ya kihistoria ya kuilinda Ukraine ilio huru.

Na alisisitiza kwamba Berlin inawakilisha mamlaka kuu barani Ulaya na kwamba ina sifa ya kipekee kutoa jibu kubwa la Uropa kumaliza vita vya "kigaidi" vya Vladimir Putin, kwa njia ambayo inazuia uchokozi wa siku zijazo juu ya maeneo kama Taiwan.

Kama ushahidi wa dhamira ya kimkakati ya kutimiza ahadi hii, kama mwandishi anavyoona, serikali ya Berlin inapaswa kujitolea katika mkutano wa Kikundi cha Mawasiliano cha Kiukreni huko Ramstein, Ujerumani, siku ya Ijumaa, kutuma vifaru vyake huko Kyiv, na sio kuruhusu nchi kama vile Poland na Ufini kutuma vifaru vya Ujerumani vya "Leopard 2" kwa Ukraine. Hii itafanywa kulingana na hatua iliyoratibiwa ya Uropa.

Mwandishi aliutaja mpango huo kwa jina la "Chui wa Ulaya".

Wajibu wa kihistoria wa Ujerumani unakuja katika hatua tatu zisizo sawa.

Miaka 80 iliyopita, Ujerumani ya Nazi yenyewe ilikuwa ikiendesha vita vya ugaidi kwenye ardhi hiyo hiyo ya Kiukreni: miji hiyo hiyo, miji na vijiji vilikuwa wahasiriwa wake kama ilivyo sasa nchini Urusi, na labda watu hao hao walikuwa wahasiriwa wa vita vyote viwili.

 Boris Romanchenko, kwa mfano, mwokokaji wa kambi nne za mateso za Wanazi, aliuawa kwa kombora la Urusi huko Kharkiv.

Anachofanya Putin kwa kuharibu uwepo huru wa nchi jirani, yenye uhalifu wa kivita, mauaji ya halaiki na kulenga raia, ndicho cha karibu zaidi ambacho tumekaribia sasa tangu 1945 kwa kile Adolf Hitler alifanya katika Vita vya Pili vya Dunia.

 Mwandishi alieleza kuwa somo tunalopata kutokana na historia hii si kwamba vifaru vya Ujerumani visitumike kamwe dhidi ya Urusi, chochote kile Kremlin itafanya, bali inapaswa kutumika kuwalinda Waukraine, ambao walikuwa miongoni mwa wahanga wakubwa wa Hitler na Stalin. .

 Hatua ya pili ya uwajibikaji wa kihistoria inatokana na kile Rais wa Ujerumani Frank Steinmeier alichoeleza kuwa ni "kufeli kwa uchungu" kwa sera ya Ujerumani kuelekea Urusi baada ya kunyakuliwa kwa Crimea na kuanza uvamizi wa Urusi mashariki mwa Ukraine mwaka 2014.

Badala ya Ujerumani kupunguza utegemezi wake kwa Warusi. nishati, iliongeza matumizi yake baada ya 2014 kwa zaidi ya asilimia 50 ya jumla ya uagizaji wa gesi kutoka Moscow, pamoja na ujenzi wa bomba la Nord Stream 2 ambalo halikutumiwa hapo awali.

 Hitilafu hii ya kihistoria ilisababisha hatua ya tatu na ya mwisho.

Mwezi mmoja baada ya Urusi kuivamia Ukraine mnamo Februari 24 mwaka jana, kundi la watu mashuhuri wa Ujerumani liliandaa mwito wa kususia mafuta kutoka Urusi mara moja.

Kansela Olaf Scholz aliamua kutofuata njia hii, akisema kwamba ingehatarisha "mamia ya maelfu ya kazi" na kuziingiza Ujerumani na Ulaya kwenye mdororo wa kiuchumi.

 Kuna wasiwasi huko Berlin kuhusu kuongezeka kwa Urusi katika kukabiliana na usambazaji wa silaha za hali ya juu za Magharibi, ambazo zinaweza kuwa sawa na matumizi ya silaha ya nyuklia ya Urusi, ambayo pia inaibua wasiwasi wa Washington.

 Lakini mwandishi anaonyesha kwamba Putin tayari anazidisha hali hiyo, na sasa anahamasisha hifadhi kubwa ya wafanyakazi wa Shirikisho la Urusi, na anaweza kukusudia kuanzisha mashambulizi mapya wakati mwingine mwaka huu.

Putin "ana wasiwasi" kuhusu Moscow kushambuliwa

Gazeti la Daily Mail lilichapisha ripoti kuhusu wasiwasi wa Rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu kulenga mji mkuu, Moscow, kwa makombora kutoka Ukraine, na kutumwa kwa mifumo ya hali ya juu ya ulinzi wa anga ili kuulinda.

Kulingana na ripoti hiyo, jeshi la Urusi liliweka mifumo ya kutisha ya ulinzi wa anga ya S-400 katika maeneo mawili katika mji mkuu, huku kukiwa na hofu kwamba Kyiv ingeanzisha mashambulizi katika mji huo.

Mfumo wa ulinzi wa anga wa S-400 Triumf umeundwa kuharibu ndege na makombora ya balestiki, ikijumuisha ya masafa ya kati. Inaweza pia kutumika dhidi ya malengo ya ardhini.

Uamuzi huo ulikuja baada ya mashambulizi mawili ya ndege zisizo na rubani za Ukraine kugonga kambi mbili za anga huko Urusi Desemba mwaka jana, na kuharibu washambuliaji wawili wa nyuklia wanaoaminika kujiandaa kushambulia Ukraine.

Jeshi limeanza kupeleka mfumo wa S-400, wenye umbali wa maili 248, katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Jimbo la Urusi kaskazini magharibi mwa Moscow. Mfumo mwingine umetumika katika Hifadhi ya Kitaifa ya Losiny Ostrov karibu na wilaya ya Sokolniki kaskazini-mashariki mwa jiji.

Mfumo mmoja unaweza kuangusha takriban shabaha 80 kwa wakati mmoja, na kasi ya kombora hilo inazidi maili 10,000 kwa saa.

Wakazi wanasema kuwa hatu hiyo ni mpya mjiini Moscow, jambo ambalo linadhihirisha hofu ya Putin ya kuligonga jiji lake kubwa zaidi, hasa baada ya mlipuko mwezi uliopita kugonga kambi ya ndege ya Engels-2 karibu na Saratov na kuharibu ndege mbili aina ya Tu-95. Kambi hiyo iko umbali wa kilomita 450, kutoka eneo la karibu zaidi la Ukraine.

Mlipuko mwingine ulipiga kambi ya kijeshi ya Urusi ya Diaghilev karibu na mji wa Ryazan, takriban maili 470 kutoka mpaka wa Ukraine, na kuua watu watatu baada ya lori la mafuta kulipuka.

Licha ya mashambulizi mengi yaliyoanzishwa na Urusi kwenye mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, Moscow bado haijashambuliwa.