Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
'Jua lilikuwa linang'aa, lakini maji yaliendelea kuja'
Mahali ilipo Bangladesh kijiografia, mpangilio na muonekano wake vinaifanya kuwa moja ya nchi zinazokumbwa zaidi na mafuriko duniani.
Hilo pia linamaanisha kuwa imo hatarini kukumbwa na ongezeko la viwango vyama maji ya bahari, mojawapo ya athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa mamilioni ya wakazi wa Bangladesh kuongezeka kwa bahari ni dhahiri.
Jashim Salam amejua mafuriko katika maisha yake yote, lakini kile alichokishuhudia mwandishi huyu wa habari wa kibarua katika mwaka 2009 kilikuwa ni tofauti.
Maji yalivamia Chaktai, katika makazi mji wa Chittagong ambapo alizaliwa na kukulia, yaliendelea kuongezeka hata baada ya mvua kuisha.
"Tulikuwa tumezoea mafuriko yanalkaribia kuletwa na mvua kubwa au vimbunga," Salam aliiambia BBC.
"Lakini katika siku ile, nilishuhudia nyumba nyingi zikifurikwa na maji, na hapakuw ana mvua - jua lilikuwa linang'aa."
Mafuriko yalikuwa yamesabaisha wa maji mengi ya guhuba ya Bengal na mwambao wa Chittagong mojawapo ya bandari za zamani zaidi suniani, ulikuwa hatarini.
Akiwa na kamera mkononi , Salam alianza kuchukua picha ya hali katika mitaa ya Chaktai.
Nchi iliyo chini tambarare
Kuchukua picha za kuongezeka kwa maji ilichukua muda mwingi wa Salam: Mafuriko yalikuwa ni ishara kwamba viwango vya maji ya bahari vinapanda - mojawapo ya athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabia nchi - ilikuwa hofu ya wakati wote kwa Chittagong na maeneo mengine ya Bangladesh. Bangladesh ni nchi iliyo tambarare, ikimaanisha kuwa sehemu kubwa ya ardhi yake iko karibu au hata chini ya viwango vya bahari.
Hilo linaifanya kukabiliwa na mchakato ambapo viwango vya joto zaidi vya dunia husababisha kuongezeka wka viwango vya bahari kwa kuongeza maji kutoka kwenye barafu inayoyeyuka, na theruji, na kwa kupanuka kwa maji ya bahari kadri inavyokuwa joto.
Kwa upande wa Chittagong kulikuwa na tatizo la ziada : mji wa mwambao ulikuwa unadidimia.
Miji inayodidimia
katika mwezi wa Machi mwaka huu, tathmini ya data za setilaiti za miji 99 yamwambao kote duniani ilichapishwa katika jarida la masuala ya utafiti wa Jiografia ya mazingira.
Watafiti walikokotoa ni kwa miji hii iliathiriwa vibaya na mkusanyiko wa ardhi unaotokana na shughuli za kuhama kwa maji ya chini ya bahari, ambako kunahusiana na kuongezeka kwa idadi ya watu na ongezeko la haraka la ukuaji wa miji.
Walibaini kuwa miji 33 ilikuwa imedidimia kwa zaidi ya sentimeta moja mkwaka mmoja baina ya 2015 na 2020, mara tano ya viwango vya dunia ya kupanda kwa maji ya bahari lilikadiria jopo la Umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (IPCC). Chittagong ulikuwa wa kwanza katika orodha ya miji 10.
Watafiti walibaini kwamba "ongezeko la haraka zaidi lamkusanyiko wa ardhi" lilikuwa linatokea kusini, kusini - mashariki, na mashariki mwa Asia. Ni jambo halisi ambalo tayari limesababisha athari mbaya nchini Indonesia : Kutokana na viwango vya hali ya juu vya lundo la mchanga, Jakarta umepangwa kubadilishwa kutokuwa mji mkuu wa nchi kwani kuna mji mwingine unaojengwa katika kisiwa tofauti kilichopo umbali wa kilomita 1,300.
"Chittagong unafahamika kama mji mkuu wa masuala ya fedha wa Bangladesh. Kuna viwanda zaidi ya 1,200 biashara kubwa ambazo zinategemea sana maji ya ardhini," Shamsuddin Illius, mwandishi wa habari wa mazingira wa Bangladeshi ,ameiambia BBC.
Utafiti mwa mwaka 2020 wa idara ya kazi za umma ilikadiria kuwa 69% ya mji inaathiriwa na viwango vya juu zaidi vya joto,
Maeneo yaliyokumbwa na mafuriko ni pamoja na Agrabad, eneo la makazi ambalo zamani lilikuwa linakaliwa na wakazi wa Chittagong,kuwanzia wanasiasa hadi wafanyabiashara.
''Sasa ni karibu linatelekezwa," Illius anasema.
"Yeyote ambaye aliweza kuhamia kwenye maeneo ya juu amekwishafanya hivyo tayari ."
Jashim Salam ana ndugu zake hawakuwa na uwezo wa kuondoka Chaktai, kwahiyo iliwabidi wazowee maisha ya kuongeza sakafu ya nyumba ya familia yao. Lakini maji yaliendelea kuja.
"Kimsingi watu walilazimika kujifunza kuishi na maji yanayoongezeka . Unaepuka uwezavyo kwenda nje katika maeno yenye maji mengi," Salam anafafanua
"Inasikitisha sana na ni ajabu."
Zaidi ya usumbufu
Ajabu ni neneo ambalo linaweza kutumiwa kuelezea kazi yake pia : Picha za Salam huonyesha watu na familia – wakiwemo watu wake – wakijaribu kuelezea kuishi maisha ya kawaida . Katika oja ya picha, watoto wanatazama televisheni katika sebule iliyofurika maji.
Mara kwa mara Bangladesh huorodheshwa kama moja ya nchi zinazokabiliwa na hatari zaidi za maafa yanayohusiana na hali ya hewa.
Repoti ya Benki ya dunia ilibaini kuwa takriban watu milionio 4.1 katika nchi hiyo walihama makazi yao mwaka 2019 kutokana na matukio ya aina hiyo na walau milioni 13 wanaweza kukabiliana na hali hiyo kufikia mwaka 2050.
‘Najichukulia binafsi kama mkimbizi wa mabadiliko ya tabia nchi’
Salam amefanya hivyo kwa kujitolea. Tangu mwanzoni mwa mwaka amekuwa akifanya kazi New York kujaribu kukukusanya pesa ili mke wake na binti yake waweze kuungana naye nchini Marekani.
"Ilibidi niweke kumbukumbu ya kile kilichkuwa kinaendelea kuwaonyesha watu katika Bangladesh na nje kwamba mabadiliko ya tabia nchi ni halisi ." Na ni zaidi ya usumbufu - na ni hatari kwa afya.
Maji kuja kutoka baharini yamechanganywa na maji machafu ya mto Karnaphuli na takataka kabla ya kuingia katika nyumba zetu. Salam anasema kwamaba magonjwa ya maambukizi ya ngozi ni jambo la kawaida katika eneo lake.
Hospitali za mji huo katika maeneo tambarare zinakumbwa na mafuriko. Moja ya picha inaonyesha mkongwe mwanaume akisukumwa kwenye maji akiwa amebebwa katika kiti cha magurudumu katika Hospitali Mother and Children , iliyopo katika mji wake
"Ninajichukulia binafsi kama mkimbizi wa hali ya hewa. Na nitafanya kila nimnaloweza kulifanya kuwakumbusha watu kwamba mabadiliko ya tabia nchi hayaiathiri Bangladesh pekee. Hebu angali tu mawimbi ya joto na dhoruba katika Ulaya mwaka huu," anasema.
"Lakini ninahitaji kumpatia binti yangu fursa ya maisha bora. Ninataka aende shule bila kuwa na hofu kuhusu afya yake na usalama wake."
Wakati huo huo, familia ya Salam – na wengine wengi Chaktai na Chittagong – watakuwa makini kuangalia viwango vya maji kabla ya kuondoka nyumbani