Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Oleksandr Usyk v Anthony Joshua II:Muingereza AJ ashindwa katika jaribio la kutwaa taji ya ubingwa wa dunia
Jitihada za Muingereza Anthony Joshua kunyakua tena mataji ya uzito wa juu yaliyounganishwa ya dunia yalimalizika kwa mafadhaiko huku Oleksandr Usyk akitoa matokeo mazuri na kushinda kwa uamuzi wa uliowagawanya waamuzi huko Jeddah, Saudi Arabia.
Katika pambano lililoitwa ‘Rage on the Red Sea’, Joshua aliyekuwa na ukakamavu, mwenye umri wa miaka 32, alionyesha nia ya kutaka kutwaa taji hilo – na alionekana kujiboresha kutoka kwa pambano lao la kwanza - lakini hakuweza kuendana na ustadi wa raia huyo wa Ukraine .
Majaji wawili waliamua pambano hilo kwa 115-113 na 116-112 wakimpa ushindi Usyk, huku jaji wa tatu akimpa mpinzani 115-113. Ingawa kulikuwa na raundi zenye ushindani, Usyk alistahili ushindi .
'Ushindi huu ni wa nchi yangu'
Oleksandr Usyk baada ya kumpiga Anthony Joshua alisema : "Napenda kuwashukuru wote walioniombea. Napenda kumshukuru Mungu kwa msaada alionipa leo kwani amenipa mengi leo. Bwana wangu ni Yesu Kristo. Naweza kukushukuru Saudia. . Asante sana.
"Natoa ushindi huu kwa familia yangu, nchi yangu, timu yangu, kwa wanajeshi wote wanaotetea nchi hii. Asante sana.
"Hii tayari ni historia. Vizazi vingi vitatazama pambano hili hasa raundi wakati mtu alijaribu kunipiga sana lakini nilisimama na kurudi."
Kuhusu iwapo atapigana na Tyson Fury ili kuunganisha mataji: "Nina uhakika kwamba Tyson Fury bado hajastaafu. Nina hakika anataka kupigana nami. Nataka kupigana naye. Ikiwa sipigani na Fury mim sipigani kabisa.
“Ni Mungu pekee ndiye anayejua nitapigana naye au la, lakini hawa wote waliopo karibu yangu, timu yangu, watanisaidia.
"Asante Bwana kwa yote."
‘Mpiganaji wa kipekee’
Anthony Joshua akichukua kipaza sauti alisema: "Usyk ni mpiganaji mzuri. Hiyo ni hisia tu.
"Kama ungejua hadithi yangu, ungeelewa mapenzi. Mimi si bondia mahiri. Nilikuwa nikienda jela na nilipata dhamana na nikaanza mazoezi. Ikiwa ningehukumiwa, nilitaka kuwa na uwezo wa kupigana.
"Inaonyesha nguvu tuliyoweka katika hili. Kwa kijana huyu kunipiga usiku wa leo, inaonyesha kiwango cha bidii ambacho lazima aliweka kwa hivyo tafadhali mpigieni makofi kama bingwa wa ulimwengu wa uzani wa juu.
"Walisema kwamba mimi si mpiganaji wa raundi 12. Jamaa huyu hapa ni wa kushangaza."
Akizungumza na Usyk moja kwa moja: "Nilikuwa nikisoma kuhusu Ukraine na mabingwa wote kutoka nchi yako ya kushangaza. Sijawahi kwenda huko. Kinachotokea huko, sijui lakini sio kizuri. Kwa Usyk kuwa bingwa, chini ya mazingira hayo, tafadhali inueni mikono yenu'