Jinsi nyota wa muziki walivyochangia kuboresha viwango vya soka Tanzania

Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania inalenga kupita hatua ya makundi ya dimba la Afcon kwa mara ya kwanza katika historia yake.

Huku timu hiyo ikijiandaa kufungua kampeni yake ya Afcon mwaka huu na pambano dhidi ya Morocco hiyo kesho, mwandishi wa michezo wa BBC Kelvin Kimathi anaangazia jinsi ambavyo mastaa wa Bongofleva, wamechangia kuboresha na kuinua viwango vya soka ya vilabu nchini humo.