Useja ulianzaje? Je, hizi ndizo sababu za kweli za kunzishwa kwake?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa nini mtu yeyote aachane na maisha ya familia na kuamua kuishi maisha ya useja? Kuzaana ni kiungo muhimu katika ukuaji wa jamii ya wanadamu. Kwa upande mwingine , dini zote duniani zinaweka msisitizo katika maadili na utakatifu.
Jamii ya wanadamu inaendelea kukuwa kwa sababu ya kuzaana, lakini kuibuka kwa mtindo wa maisha ya useja kumewashangaza wanaathropolojia.
Kwa kuwa 'ushiriiano' ni msingi mwingine wa maisha ya binadamu, baadhi wanaashiria kuwa desturi ya kupatia kipaumbele mambo yayonufaisha kundi imeendela kuimarika.
Hata hivyo, desturi hii inasemekana kuwa inaweka mzigo mzoto kwa jamii ya wanadamu na ni mzogo wa kukataa watoto.
Wengine wanahoji kuwa wanadamu walibuni taasisi za kidini (au kitu kingine) kwa maslahi yao wenyewe au ya familia, na kuwatenga wale ambao hawakujihusisha. Utafiti mpya kuhusu useja umechapishwa hivi majuzi katika 'Kesi za Jumuiya ya Kifalme B'.
Utafiti wa kina wa waseja watakatifu katika monasteri za Wabudha wa Tibet magharibi mwa China ulijaribu kujibu swali hili la msingi la jinsi useja ulivyoanza.
Hadi hivi majuzi lilikuwa ni jambo la kawaida miongoni mwa baadhi ya familia za Watibeti kupeleka mwana wao mdogo kwenye useja wa kudumu katika monasteri za Wabuddha.
Rekodi za kihistoria, zianonyesha kuwa mmoja kati ya kila watoto saba wa kiume alikuwa mtawa wa Buddha. Familia zao zinataja sababu za kidini kwa hili.

Chanzo cha picha, Getty Images
Famili azinazoongozwa na baba
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Katika utafiti wa hivi punde zaidi, kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Lanzhou nchini China, nyumba 530 katika vijiji 21 vya Uwanda wa Tibetan mashariki katika Mkoa wa Gansu zilihojiwa.
Kwa kuzingatia ukoo wa familia. Historia ya familia ya kila mtu, maelezo kuhusu waanzilishi wa familia zao miongoni mwa zingine yalikusanywa. Vijiji hivi vinakaliwa na baba wa taifa Amdo wa Watibet. Wanafuga wanyama na kuendeleza shughuli za kilimo kwenye mashamba madogo.
Katika jamii zao mali hurithiwa kutoka kwa baba kwenda kwa mwana.Ilibainika kuwa mmoja wa mandugu alikuwa mtawa waliobaki walikuwa matajiri.Walikuwa na mali nyingi kwa sababu hakukua na ushindani wa kung’ang’ania mali ya kurithi kutoka kwa baba yao watoto wanaobaki wanapata sehemu kubwa ya mali ya baba yao na kuwa tajiri zaidi.
Wale wanaonekana kuwa na karama kubwa wanapaswa kuacha mali. Wazazi walikuwa wakimpeleka mmoja wao kwenye ashram ili kuepusha ugomvi baina ya wana. Kwa ujumla mali ya baba huenda kwa mwana mkubwa. Mwana wa pili au wa tatu angepelekwa kwa ashram. Hata hivyo, cha kushangaza wanaume waliokuwa na kaka waseja walizaa watoto zaidi.
Mbali na hayo, walipata watoto mapema. Kwa hivyo, inageuka kuwa kupeleka mmoja wa wana kwa useja sio faida za kifedha pekee bali pia faida za uzazi.
Mfano wa hisabati ya useja
Mfano wa hisabati ulitengenezwa ili kuelewa asili ya useja. Kupitia hili, ikiwa mmoja wa mandugu amezoea useja, manufaa kwa wengine yamechunguzwa. Kwanza, maisha ya useja yanapunguza ushindani kwa wasichana katika kijiji. Hata hivyo, maisha ya useja hayana manufaa yoyote kwa mtu binafsi bali ni faida kwa jamii inayomzunguka.Na kisha, kusiwe na nafasi ya useja kustawi.
Lakini, ndugu wengine wa Brahmachari wanakuwa matajiri. Thamani yao inaongezeka katika soko la ndoa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hata hivyo ingekuwa ni uamuzi wa kibinafsi kuamua kuwa mseja au la, watu wengi hawengekuwa waseja kwasababu manufaa kwa mtu binafsi ni machache.
Wazazi walizingatia maendeleo ya pamoja ya watoto wao. Hata kama mtu atakuwa mseja, wengine watatulia vizuri, kwa hivyo hakuna athari kwa wazazi.
Kuwapeleka kwenye useja katika umri mdogo, kuifanya kama sherehe, na kuwadharau wanapokua na kuacha useja. Yote hii inaonekana kuwa mila iliyoundwa na wazazi kwa maslahi yao wenyewe. Mtindo huu pia unatoa mwanga kwa nini wazazi wanajihusisha na mauaji ya watoto wachanga katika baadi ya jamii, na faida hatua hiyo kwao.
Mfumo huu pia unaelezea kwa nini wanawake waseja hawana uwezekano mdogo wa kuwa waseja katika mfumo dume. Hata hivyo, jamii ambazo wasichana wana haki ya kumiliki mali (baadhi ya nchi za Ulaya) zinaweza kuwa na wanawake waseja zaidi.
Mawazo mapya huunda mifumo mipya, hata kama wakati mwingine sio ya kimantiki. Watu huzoea taratibu hizi mpya.
Hata hivyo , huenda kuna sababu za kiuchumi nay a kimeguzi yanayohusiana na taratibu hizo.












