Kwanini kuna misururu ya kuchoma miili ya wafu China?

Huduma za kuchoma miili ya wafu kote nchini China zinahangaika kukabiliana na idadi kubwa ya miili baada ya serikali ya kuamua kuondoka hatua za 'Zero-Covid' zilizolenga kutokomeza kabisa Covid, kulingana na vyombo mbali mbali vya habari nchini humo.

Mwandishi wa habari Dake Kang, mwenye makao yake mjini Beijing, anayefanyika kazi Shirika la habari la Associated Press (AP), alitembelea jumba la kuchoma miili ya wafu , ambalo limetengwa kwa ajili ya wafu waliokufa kutokana na Covid.

 "Watu kumi na wawili au 24 walikuwa wamesimama nje yake huku watu wakiingiza miili ya wafu na kuita majina ya wafu ," Kang aliiambia BBC kutoka Beijing.

Alizungumza na wenye maduka waliopo karibu na jumba la kuhifadhia maiti ambao walisema kuwa wameshuhudia ongezeko la magari yanayowaleta wafu.

"Mmoja wao alisema kuwa wanakadiria kuwa labda watu 50 hadi 100 wanachomwa pake kila siku, kinyume na watu 12 ambao kwa kawaida huchomwa kwa simu ," anasema Kang.

Sio tu Beijing, ambako wanaishi watu zaidi ya milioni 22, maeneo yote ya uchomaji wa miili ya wafu kote nchini yanaonekana kuwa na shughuli nyingi kuliko kawaida.

Kuanzia askazini – mashariki mwa nchi hadi kusini – magharibi , shirika la habari la AFO limeripoti kwamba wafanyakazi wa kuchoma wafu wanasema wamekuwa wakihangaika kuchoma miili mingi ya wafu kutokana na wimbi la covid.

Kilomita takriban 700k kaskazini -mashariki mwa Beijing, katika mji wa Shenyang, mfanyakazi katika jumba la mazishi alisema kuwa miili ya wafu imekuwa ikiachwa bila kuzikwa kwa hadi siku tano.

Maeneo ya huduma za kuchoma miili kwakweli ‘’yamejaa kabisa’’, alisema.

"Sijawahi kuona mwaka kama huu."

Lakini Kang anasema haiwezekani kuelezea ukubwa wa ongezeko la vifo vya Covid ni wa kiasi gani.

Maafisa nchini China waliripoti vifo vitano tu vya Covid Jumanne, kufuatia viwili siku ya Jumatatu, ambavyo vilikuwa ni vifo vilivyoripotiwa katika kipindi cha wiki kadhaa.

Nini kinachofanyika katika maeneo ya kuchoma miili ya wafu kote Uchina?

Jumapili, siku mbili baada ya kang kutembelea Dongijao, magari ya kubebea maiti yalijipanga kwenye barabara , Reuters iliripoti.

Moshi kutoka kwenye maeneo hayo ulijitokeza juu kutoka kwenye miili iliyokuwa ikichomwa, takriban magari 30 yalionekana nje ya jumba la kuchoma miili la Dongijao.

Watu wa familia walikuwa wakipiga picha za video mbele ya hilo hilo katika mji wa beijing, wakisubiri masalia ya wapendwa wao.

 Polisi walikuwa wakilinda baadhi ya maeneo ya kuchoma moto, Bloomberg na Sky News ziliripoti.

Ongezeko la visa vya Covid

"Nilizungumza na jamaa kadhaa wa watu ambao walifariki baada ya ndugu zao kupatikana na Covid. Hilo linashangaza , kwasababu katika orodha rasmi katika wakati ambapo hapakuwa na ripoti ya vifo vinavyotokana na Covid. Inaweza kuwa jambo gumu kidogo kwasababu ya jinsi China inavyohesabu vifo vya Covid," Kang alisema.

Uchina iliripoti vifo 5,242 vya Covid tangu janga lilipotokea katika mji Wuhan mwishoni mwa mwaka 2019 - idadi hiyo ikiwa ni ndogo kwa viwango vya dunia.

Kumalizika kwa mpango wa kupima kwa lazima kumefanya juhudi za kubaini ongezeko la idadi ya visa vya Covid kuwa ngumu, huku maafisa wiki iliyopita wakikiri kwamba kwa sasa "haiwezekani " kuhesabu ni watu wangapi wameugua.

"Mmoja wa watu katika nyumba ya kuhifadhia maiti alikuwa anasema kuwa kwenye cheti cha kifo waliona imeandikwa kwa homa ya mapafu -pneumonia ilikuwa ndio sababu ya kifo, Covid," Kang alisema.

Vifo milioni moja katika mwaka 2023, utafiti unabashiri

Kuondolewa ghafla kwa sheria za kudhibiti Covid kunaweza kusababisha mlipuko wa visa na zaidi ya vifo milioni moja katika mwaka 2023, kulingana na makadirio kutoka katika taasisi ya afya nchini humo-Health Metrics and Evaluation (IHME).

IHME ni kituo huru cha utafiti wa afya katika chuo kikuu cha Washington nchini Marekani.

Utafiti huo ulibaini kuwa kutakuwa na vifo 322,000 kufikia Aprili 1, 2023 na kwa tarehe hiyo hiyo, maambukizi yataongezeka.

"Sera ya China ya zero-Covid huenda ilikuwa na ufanisi katika kuzuia aina za mwanzo za kusambaa zaidi lakini aina ya Covid inayosambaa zaidi ya Omicron iliweza kudhibitiwa," IHME alisema mkurugenzi Christopher Murray.

Makadirio hayo yalitokana na data za kimikoa na taarifa kutoka katika mlipuko wa hivi karibuni wa Omicron mjini Hong Kong.

 "China ambayo awali ilikuwa na mlipuko wa Wuhan haikuripoti kifo chochote. Hiyo ndio maana tuliitazama Hong Kong ili kupata kiwango cha maambukizi ," Murray alisema.

 Lakini ilionekana kwamba hospitali za Uchina ni, walau kwa hapa, hatukushangazwa na ongezeko . Kang alitembelea mojawapo ya hospitali mjini Beijing.

 "Hakuna dalili halisi za kujaa kwa watu. Lakiini bila shaka, beijing sio mwakilishi wa uchina. Huenda ina raslimali bora zaidi za matibabu katika nchi nzima," alisema.