Jinsi uwepo wa Covid unavyo wakosesha China shamrashamra za Kombe la Dunia

Vyombo vya habari vimeangazia pakubwa Kombe la Dunia wiki hii , lakini mechi zimechochea hasira kwamba watu nchini humo kutokana na kuzuiwa kusherehekea.

 Zaidi ya kwamba timu ya China haijafuzu kushiriki tukio hilo, matukio ya watu wanaosherehekea bila kuvaa barakoa na mikusanyiko mikubwa ya Qatar imewakera watazamaji, ambao wamezuiwa kukusanyika kutazama mechi. Wengi walitumia Kombe la Dunia kulalamika kuhusu mikakati iliyopo ya China. 

Nchi hiyo imeendeleza sera yake ya kumaliza kabisa Covid - zero-Covid, ambapo jamii nzima zimefungiwa katika ‘’marufuku ya kutotoka nje’’ kutokana na kisa kimoja cha virusi vya korona , ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo

 China kwa sasa inakabiliwa na mlipuko mbaya zaidi katika kipindi cha miezi sita, na sheria za kukaa nyumbani ''Lockdown'' zimewekwa katika maeneo mbali mbali katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita. Katika kipindi cha saa 24, China imerekodi visa vipya zaidi ya 28,000 vya maambukizi ya covid, hivi viko katika kila jimbo.

Kutazama kutoka nyumbani na maeneo ya makambi

Soka ni maarufu sana nchini Uchina. Rais Xi Jinping anafahamika kama mtu anayependa michezo, na amewahi kuzungumzia awali kuwa ana ndoto za nchi yake kushinda Kombe la Dunia.

 Matokeo yake, mechi zinaonyeshwa kwenye televisheni ya taifa CCTV, na vyombo vya habari vya taifa vimehakikisha ‘’uwepo’’ wa China katika Kombe la Dunia Qatar unaonekana.

Gazeti la The Global Times limeripoti juu ya bidhaa zilizotengenezwa na China "kuanzia mabasi katika uwanja wa [Lusail] , na hata kitengo cha viyoyozi wamewasilishwa vyema katika tukio".

 Vyombo vya habari maarufu kama vile CCTV pia vimepigia debe uwepo wa wawakilishi wa Uchina katika sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia, na jinsi dubu wawili wakubwa walivyowasili mjini Qatar "kukutana" na wageni wanaowasili katika tukio la Kombe la Dunia.

Lakini ni dhahiri kwamba Covid-19 imekuwa kikwazo katika sherehe. Katika miji mikuu, milipuko imesababisha shughuli zisizokuwa lazima kufungwa kwa mara nyingine tena, na watu wanatolewa wito wa kudhibiti matembezi yao.

Huku kukiwa hakuna vilabu vya pombe vya kutembelea gazeti la Global Times linasema kuwa baadhi ya mashabiki "wanaamua kutazama mechi nyumbani na familia zao". Wengine wameripotiwa kuchukuliwa katika maeneo ya makambi

Safari za ndege kati ya Qatar na China pia zimepunguzwa sana kwa wale wanaotumaini kutazama tukio binafsi.

Wengi wanahisi wametengwa vibaya katika kutazama tukio la Kombe la Dunia mwaka huu.

 Barua ya wazi inayohoji sera za nchi hiyo za kumaliza corona - zero-Covid na kuuliza iwapo China iko "katika sayari moja " saw ana Qatar ilisambaa kwenye mtamndao wa ujumbe wa simu wa WeChat Jumanne, kabla ya kuiwa.

 Maoni katika mtandao wa Twitte – saw ana mtandao wa kijamii wa Weibo yalitoka kwa watumiaji ambao walizungumzia kuhusu jinsi kutazama mechi za mwaka huu kunawafanya wahisi wametengwa na maeneo mengine ya dunia.

Baadhi walizungumzia kuhsuu mitazamo yao kwamba ni "ajabu " kuona maelfu ya watu wakikusanyika, bila kuvaa barakoa au kuhitaji kuonyesha ushahidi wa kipimo cha hivi karibuni cha Covid-19 . " Hakuna viti vilivyotenganishwa ili watu wakae mbali na hakuna mtu yeyote aliyevaa mavazi meupe au ya blu ya hospitali kando. Sayari hii kwa kweli imegawanyika."

 "Kwa upande mmoja wa dunia, kuna sherehe za Carnival hilo ni Kombe la Dunia, kwa upande mwingine kuna sheria za kutotembelea maeneo ya umma kwa siku tano ," mmoja alisema.

 Baadhi wanasema wanaona vigumu kuelezea watoto wao ni kwanini wanachokiona katika Kombe la Dunia ni tofauti na kile ambacho watu wanakabiliana nacho nyumbani.

 Hatahivyo hakuna mwisho wa sheria zilizopo kwa sasa za udhibiti wa Covid nchini Uchina. Wiki hii msemaji wa kamati ya afya ya taifa hilo "alionya dhidi ya yeyote kukiuka sherea za kuzuia na kudhibiti janga " na akataka "kuchukuliwa kwa hatua kali " za kudhibiti visa vya janga hilo.

 Serikali za mitaa katika miji mikuu zimeanzisha mpango wa kupima watu wengi na sheria za kusafiri na kwa ujumla kuwataka watu wakae nyumbani.

Lakini baadaya miaka mitatu yah atua hizo, watu wamechoka, na matokeo yake mwezi uliopita waliandamana kupinga hatua hizo katika miji yote miwili ya Guangzhou na Zhengzhou.