Ni kwanini Warusi wengi wanafumbia jicho mzozo?

Katika wiki kadhaa kuelekea uvamizi wa Urusi, nilikuwa nikitembea kwa saa kadhaa katika wilaya ya katikati mwa mji mkuu Moscow ya Zamoskvorechiye, ambako nilikuwa nikiishi na kufanya kazi katika ofisi za BBC kwa miaka saba.

Likiwa ni eneo la mji lenye amani , kwangu linawakilisha hali ya sasa na iliyopita ya Urusi

Kwa karne kadhaa Watu wa Moscowwamekuwa wakija hapa kujenga nyumba zao na bilashara na kuishi maisha yao ya ukimya, na kuwaacha watawala wao kuendelea na matamanio yao katika jukwaa kubwa zaidi ambayo Mrusi wa kawaida hakuwahi kushirikishwa.

Unapakana na mto Moskva na Kremlin kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine kuna majengo marefu na na marefu yaliyojengwa kwenye mitaa myembamba yenye barabara ya leri likiwemo kanisa lililojengwa karne ya 19 .

Mara ya mwisho nilikuwa kule Februari wakati nilipopigiwa simu na rafiki, ambaye alizaliwa katika mji wa pili kwa ukubwa zaidi wa Ukraine wa Kharkiv, ambaye kwa sasa anafanya kazi mjini Moscow.

Je kweli Putin ataanza vita na Ukraine. Aliuliza. Hakuna hata mmoja kati yetu aliyeamini hilo.

Lakini kwa kuwa tulizungukwa na kumbukumbu za ghasia za mara kwa mara za Urusi nilihisi kuwa sasa vita ni lazima. Matembezi yangu ya kila siku yalikuwa ni njia ya kusema kwaheri kwa dunia, na hata labda nchi, ambayo haiwezi kuwa sawa na ilivyokuwa tena.

Warusi wengi wameiacha nchi yao iendeswe – wengi wakati Vladimir Putin alipotangaza urejeshwaji wa wanajeshi wastaafu jeshini mwezi Septemba mwaka jana.

Maelfu kwa maelfu ya Warusi wameondoka Urusi, nikiwemo mimi na wafanyakazi wenzangu wa BBC Warusi.

Lakini kwa wengi waliobaki nchini Urusi, maisha yameendelea kama kawaida. Hasa katika miji mikubwa.

Bado mnaweza kukutana kunywa kahawa na mabango bado yanafanana, lakini maduka kama Starbucks yaliondoka.

Huduma nyingi kwa ujumla bado zinaendelea kutolewa kama kawaida.

Vikwazo vya kimataifa havijaiathiri Urusi sawa na ilivyokuwa katika miaka ya 1990, ambapo uchumi wa nchi uliporomoka.

Lakini kama anavyosema msomi Mrusi anayeishi Belfast Aleksandr Titov , Urusi bado iko katika mzozo.

Matamasha ya furaha na shangwe yanayoandaliwa wa magavana wa maeneo yanahudhuriwa vyema, rafiki aliniambia.

Lakini madaktari wa maeneo wanaacha kazi zao, kwa kushindwa kuhimili idadi kubwa ya watu wanaojeruhiwa kutokana na vita kwanaoletwa hospitalini kutibiwa.

Wakazi wanahisi kutelekezwa na wana hasira katika mji mdogo wenye mapigano wa Shebikino, ambako mashambulio yanayovuka mpaka yamekuwa hali halisi ya kila siku.

Mmoja wa wanafamilia wanaotembelea St Petersburg alishitushwa kubaini kuwa hakuna lolote lililobadilika wakati maisha yao wenyewe yamesambaratishwa.

Katika Pskov, karibu na mipaka ya Estonian na Latvian, hali ni ya huzuzni na kila mtu hujifanya kuwa vita haimuhusu, niliambiwa.

Pskov ni nyumbani kwa walinzi wa kikosi cha anga - 76th Guards Air Assault Division,ambacho kwa sasa kinafahamika kwa uhalifu wa kivita, wanajeshi wake wanashutumiwa kwa kufanya mshambulizi katika mji wa Bucha, nje ya Kyiv.

Huduma y abasi imeanza kuunganisha mji na makaburi ambako idadi kubwa ya wanajeshi waliouawa nchini Ukraine wamezikwa.

Chini ya daraja kumeandikwa neneo PEACE[amani] kwa herufi kubwa

Wakati BBC ilipotembelea katika maeneo haya ya makaburini karibu na Pskov kulikuwa na makumi ya makaburi mapya ya wanajeshi wa kikosi cha miavuli cha Urusi.

Katika treni kuelekea Petrozavodsk, karibu na mpaka wa Finland, rafiki alikutana na kikundi cha vijana wadogo waliokuwa wakicheza mchezo wa "Kuutaja mji ule’’.

Mtu mmoja alitaja Donetsk:Je ni mji wa Urusi au Ukraine? Hakuna hata mmoja wao aliyekuwa na uhakika. Mji huu umetwaliwa kinyume cha sheria na serikali yao

Ni nini wanachofikiria kuhusu vita? Haviwahusu.

Je Warusi kweli wanaunga mkono ukatili unaofanywa nchini Ukraine kwa jina lao, au wanajifanya hawaelewi unatokea ili waishi?

Kwa mazungumzo nao ni vigumu kufahamu ukweli halisi. Wanasosholojia na waendeshaji maarufu wa kura za maoni wamejaribu kuelewa hilo, lakini hakuna uhuru wa kujieleza au wa habari nchini Ukraine kwahivyo haiwezekani kufahamu iwapo watu ni wakweli.

Kura za maoni zinaelezea kuwa wengi wa Warusi, kama hawaungi mkono vita, basi hawavipingi.