'Niliwekewa dawa ya usingizi na kubakwa na mume wangu kwa miaka kadhaa'

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Jane Deith and Emma Forde
- Nafasi, BBC File on 4 Investigates
- Muda wa kusoma: Dakika 7
Wakati Kate na mumewe walipoketi jioni moja kwa mazungumzo, hakuwa amejiandaa kwa kile alichokuwa anajiandaa kumwambia.
"Nimekuwa nikikubaka. Nimekuwa nikikuwekea dawa za kulevya na kukupiga picha kwa miaka kadhaa."
Kate (sio jina lake halisi) alipigwa na butwaa. Alikimya kwa muda asijue la kufanya. Hakuweza kuelewa kile ambacho mume wake alichokuwa akisema.
"Aliniambia kana kwamba ni kitu cha kawaida kama hivi unajua: 'Kesho jioni tutakula tambi, waonaje tukinunua mkate?'"
Tahadhari: Tarifa hii ina maelezo ya kusikitisha ya unyanyasaji wa kingono
Kwa miaka kadhaa,amekuwa akimdhibiti kisiri na kumnyanayasa kingono. Alikuwa mjeuri na alitumia vibayadawa za usingizi.
Kwa miaka mingi pia kumekuwa na matukio ambapo Kate aliamka na kumkuta akifanya naye mapenzi, jambo ambalo hakuweza hakuridhia, kwa sababu alikuwa amelala. Huu ulikuwa ubakaji.
Angejuta baadaye, akimshawishi kuwa alikuwa amelala na hajui anachofanya. Alikuwa mgonjwa na kwamba hakuwa sawa.
Kate alimsaidia kupata usaidizi kutoka kwa wataalamu wa matibabu.
Lakini hakujua wakati huo kwamba usiku alikuwa akimnywesha chai iliyotiwa dawa za usingizi, na kumbaka alipokuwa amelala.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Baada ya kukiri alichofanya, alimwambia kuwa akienda polisi kuwasilisha malalamishi maisha yake yangeisha. Kwa hivyo hakufanya hivyo.
Huyu alikuwa ni baba wa watoto wake. Hakuamini kuwa mwenzi wake wa maisha yake angeweza kumfanyia unyama huo.
Lakini, katika miezi michache iliyofuata hofu ya kile alichosema amekuwa akimfanyia ilianza kumuathiri.
Kate anasema aliugua sana, uzani wake ukapungua, na kuanza kupata kiwewe.
Karibu mwaka mmoja baada ya tukio hilo, Kate alimwambia dada yake kila kitu.
Dada yake alimpigia simu mama yao - ambaye aliwasilisha taarifa kwa polisi. Mume wa Kate alikamatwa na kuhojiwa.
Siku nne baadaye, hata hivyo, Kate aliwasiliana na kituo cha Polisi wa Cornwall na kusema hataki kuendelea na kesi hiyo.
"Sikuwa tayari," anasema. "Kulikuwa na huzuni. Sio kwangu tu, bali kwa watoto. Baba yao hangekuwa vile alivyokuwa."
Lakini, Kate hakutaka tena kuishi na mume, akaamua kuhama.
Baada ya hayo, alianza kufikiria kwa uwazi zaidi juu ya kile kilichotokea. Miezi sita baadaye, Kate alirudi tena polisi.
Uchunguzi ulianzishwa ukiongozwa na Det Con Mike Smith.
Kate anasema mpelelezi huyo alimsaidia kuelewa kwamba alikuwa muathirika wa uhalifu mkubwa: "Alinisaidia kuelewa uovu niliyofayiwa. Alienieleza kuwa nilichotendewa ni ubakaji."

Chanzo cha picha, Getty Images
Rekodi za matibabu za mume wake (sasa wa zamani) zilitoa ushahidi muhimu. Baada ya kukiri kwake kwa Kate, alikuwa amelipa kibinafsi kuonana na daktari wa akili.
Katika kikao hicho alieleza "kumtilia dawa mke wake ili afanye naye mapenzi akiwa amelala". Maelezo hayo yalinakiliwa katika maelezo ya daktari wa akili.
Kate anasema mume wake pia aliungama kwa baadhi ya watu wa Narcotics Anonymous, pamoja na marafiki katika kanisa walilohudhuria wote.
Faili za polisi kuhusu kesi hiyo hatimaye ziliwasilishwa kwa Huduma ya Mashtaka ya Crown (CPS) lakini iliamua kutofungua mashtaka.
Kate hakuelewa kwa nini.
"Nilifikiri, kama huna ushahidi wa kutosha hatua hiyo inaweza kunitia hatiani, licha ya mhalifu kuungama, mtu mwingine anawezaje kupata haki?" Anasema.
Kwa huzuni kubwa aliwasilisha maombi ya kukaguliwa rasmi kwa maamuzi ya waendesha mashataka. Miezi sita baadaye, odisi ya waendesha amashtaka ilisema kwamba mume wake wa zamani sasa atashtakiwa. Pia ilikiri kwamba "uamuzi wa awali uliochukuliwa na mwendesha mashtaka wetu anayemshtaki ulikuwa na dosari".
"Wakati tunapata idadi kubwa ya maamuzi yetu ya malipo mara ya kwanza, haikuwa hivyo na tunaomba radhi kwa mwathiriwa kwa dhiki ambayo itasababishia," msemaji wa mwendesha mashtaka aliiambia makala ya BBC File on 4 Investigates.

Chanzo cha picha, University of Bristol School for Policy Studies
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani mnamo 2022, miaka mitano baada ya mume wa zamani wa Kate kukiri makosa.
Wakati wa kesi, alidai Kate alipata ndoto ya ngono usingizini na aliamka katika hali hiyo kufanya ngono naye kwa ridhaa yake. Alikiri kumtumia dawa za usingizi, lakini aliongeza kuwa alifanya hivyo ili aweze kumhudumia bila kumwamsha. Alikanusha kuwa ilifanya hivyo ili aweze kumbaka, lakini majaji hawakumwamini.
"Niliona kama ujinga kabisa," anasema Det Con Smith. "Hili ndilo jambo la kuhuzunisha zaidi maishani mwake wakati inamuosha kana kwamba aliridhia kufanya aina fulani ya ngono."
Baada ya kesi ya wiki nzima, mume huyo wa zamani alipatikana na hatia ya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia na kutumia dawa ya usingizi kama silaha.
Katika hukumu hiyo, alielezewa na hakimu kama "mtu mwenye ubinafsi, aliyetanguliza mahitaji kwanza", ambaye hakuonyesha "kujutia alichofanya".
Alihukumiwa kifungo cha miaka 11 jela na kuwekewa amri ya maisha ya kutomkaribia Mwathiriwa.
Miaka mitatu baadaye, Kate anajaribu kujenga upya maisha yake na watoto wake. Tangu wakati huo amepatikana na msongo wa mawazo baada ya kukuabiliwa na tukio kubwa lililomuathiri kiakili na ugonjwa wa neva, unaosababishwa na kiwewe kilichopitiliza.
Kate anafananisha kesi yake na ile ya Gisèle Pelicot, mwanamke Mfaransa ambaye mume wake wa zamani alimpa dawa za kulevya na kumbaka, na kuwaambia makumi ya wanaume kumdhulumu.
"Nakumbuka wakati huo nikimuombea Mungu apate usaidizi na uthibitisho ambao anahitaji," Kate anasema.
"Udhibiti wa kutumia kemikali" ni mbinu inayotumiwa na wanyanyasaji wa kingono kama silaha na "huenda imeenea sana," anaonya Prof Marianne Hester kutoka Kituo cha Utafiti wa Jinsia na Unyanyasaji cha Chuo Kikuu cha Bristol.
"Nadhani ni zana inayotumiwa na mnyanyasaji," anasema. "Ikiwa muathiriwa anatumia dawa alizopewa na mhudumu wa afya ili azitumie nyumba, je, mhusika anazitumia kama sehemu ya unyanyasaji kwa namna yoyote?"

Chanzo cha picha, PA Media
Visa vya watu kutiliwa dawa za kulevya kwenye vinywaji havirekodiwi kwa sababu ya mabadiliko ya jinsi polisi wanavyorekodi uhalifu, anasema Dame Nicole Jacobs, Kamishna wa Unyanyasaji wa Majumbani kwa Uingereza na Wales.
"Kama mawaziri wanataka kuhakikisha hatuazilizowekwa kupunguza nusu ya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana katika muongo ujao basi lazima tuzingatie kikamilifu uhalifu wote unaohusiana na unyanyasaji wa nyumbani unaoripotiwa kwa polisi," anasema.
"Hii ni muhimu sio tu kuhakikisha wahalifu wanachukuliwa hatua, lakini ili waathiriwa wanapata usaidizi unaohitajika wa kuanza upya maisha baada ya unyanyasaji."
Ofisi ya Mambo ya Ndani ilituambia kwamba inabuni programu ya polisi ambayo itaweza kutambua matukio ambayo hutokea kama sehemu ya uhalifu mwingine.
Chini ya Mswada wa Sheria ya Uhalifu unaopitishwa hivi sasa Bungeni, serikali inaunda kile kinachoelezewa kuwa kosa jipya la "kisasa" la "kudhubiti matumizi ya dawa zenye madhara, ikiwa ni pamoja na kupaza sauti" - kuwahimiza waathiriwa kuripoti kwa polisi visa vya kutiliwa dawa.
Kumtilia mtu dawa ya kulewesha au kumfanya mtu apoteze fahamu kwenye kinywaji ni uhalifu kote nchini Uingereza. Chini ya sheria mpya - inayotumika nchini Uingereza na Wales - wahalifu watakabiliwa na kifungo cha miaka 10 jela.
Wizara ya Sheria inasema kuundwa kwa kosa mahsusi kutasaidia polisi kufuatilia matukio ya kurushiana maneno, "na itawahimiza waathiriwa zaidi... kujitokeza na kuripoti uhalifu huu".
Jess Phillips - waziri wa ulinzi na unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana - aliitaja hali hiyo kuwa "uhalifu mbaya ambao unakiuka haki ya waathiriwa na hali ya usalama", katika taarifa yake kwa makala ya BBC File on 4 Investigates.
Majadiliano yanaendelea kupanua sheria hadi Ireland Kaskazini.
Serikali ya Scotland inasema haina sasa lakini haina mipango ya kuunda sheria mpya kushughulikia kosa maalum lakini inatathmini suala hilo.
Hatimaye Kate alipata haki. Lakini mume wake wa zamani hangekuwa gerezani kama hangechukuliwa Chatua na mamlaka husika.
"Nataka watu wengine waelewe kwamba unyanyasaji hutokea kimya kimya zaidi kuliko unavyofikiri," Kate anasema. "Bado ninajifunza ipasavyo kile kilichonipata na jinsi hali hiyo ilivyoniathiri."
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












