CHAN 2024: Tanzania yasema ilikuwa tayari kuandaa michuano

Maelezo ya sauti,
Muda wa kusoma: Dakika 1

Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani ya nchi (CHAN) 2024 zimeahirishwa hadi Agosti, zikiwa ni siku 18 tu kabla ya kuanza kwake nchini Tanzania, Kenya na Uganda.

Taarifa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), imesema wataalamu wake wameshauri kwamba muda zaidi unahitajika ili kuhakikisha miundombinu na vifaa vya fainali hizo viko katika viwango vinavyohitajika.

CHAN 2024 ilipangwa kufanyika kati ya Februari mosi hadi 28, huku baadhi ya nchi zikiwa tayari zimetangaza vikosi vyao na kuanza kambi za mazoezi.

Kufahamu hatua hii inaziweka wapi nchi waandaaji na nini kinapaswa kufanyika, Scolar Kisanga amezungumza na Katibu Mkuu wa wizara ya michezo nchini Tanzania ambaye pia ni msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa anayeanza kwa kuelezea taarifa hiyo ilivyopokewa.