Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Freddy: Kimbunga kilichodumu zaidi ya mwezi mmoja
Malawi, Madagascar na Msumbiji wanakumbwa na madhara ya Kimbunga Freddy.
Zaidi ya watu 400 wameuawa na maelfu ya nyumba kuharibiwa.
Freddy imekuwa mojawapo ya dhoruba za muda mrefu zaidi kuwahi kurekodiwa katika Ulimwengu wa Kusini, ikiwa sio ulimwengu wote.
Kusini mwa Afrika mara nyingi hukumbwa na vimbunga na dhoruba za kitropiki zinazoingia kutoka Bahari ya Hindi lakini Freddy ilikuwa tofauti kwa sababu kadhaa.
Kimbunga Freddy kimekaa muda gani?
Hatimaye kimbunga Freddy kimetangazwa kumalizika na huduma ya hali ya hewa ya Ufaransa. Dhoruba hiyo ilipewa jina na Ofisi ya Hali ya Hewa ya Australia mnamo tarehe 4 Februari na hatimaye ilimalizika mnamo 14 Machi.
kilikuwa na nguvu ya kutosha kuainishwa rasmi kama mfumo wa kitropiki kwa angalau siku 36.
Hata hivyo, tunahitaji kusubiri uthibitisho wa Shirika la Hali ya Hewa Ulimwenguni kabla ya kusema ikiwa ndio dhoruba iliyodumu kwa muda mrefu zaidi iliyorekodiwa.
Kinachovutia kuhusu Freddy ni umbali ambao umesafiri. Ilianza safari yake kutoka pwani ya kaskazini-magharibi mwa Australia, kikavuka Kusini mwa Bahari ya Hindi kutoka mashariki hadi magharibi, moja ya dhoruba nne tu katika historia kufanya hivyo.
Storm Freddy kilikuwa na nguvu kiasi gani?
Njia ya kawaida ya kupima nguvu ya dhoruba ni kwa kasi ya upepo. Kwa nguvu zake zote, Freddy kilikuwa sawa na kimbunga cha Kitengo cha 5 chenye upepo unaozidi kasi ya 160mph (260 km/h).
Kwa bahati nzuri, kilikuwa kali zaidi juu ya maji.
Kimbunga Freddy kilivunja rekodi ya nishati ya kimbunga iliyokusanywa muda wote (ACE) katika Ulimwengu wa Kusini, kipimo cha nguvu ya dhoruba hiyo kwa muda, na kushinda rekodi ya awali, iliyowekwa na kimbunga Fantala mwaka wa 2016.
Ilikuwa pia dhoruba ya kwanza katika Ulimwengu wa Kusini kupitia mizunguko minne tofauti ya kuongezeka kwa kasi - hii ni ongezeko la upepo wa juu wa kimbunga cha kitropiki cha angalau mafundo 30 katika masaa 24 tu.
Tangu kutua, kiasi cha mvua kimezidi 600mm (inchi 24) katika baadhi ya maeneo yenye mvua kubwa na kusababisha maporomoko ya matope katika maeneo hatarishi.
Pamoja na upepo wa nguvu za kimbunga, dhoruba hiyo pia ilileta mawimbi makubwa ya dhoruba huku kikiendelea kuongeza nguvu kwenye maji ya joto ya Mfereji wa Msumbiji.
Kuna tofauti gani kati ya Kimbunga na dhoruba ya kitropiki?
Kimbunga cha Kitropiki katika Bahari ya Hindi kina nguvu zaidi kuliko dhoruba ya kitropiki.
Kimbunga Freddy kilipiga Msumbiji kwa mara ya kwanza kama dhoruba ya wastani ya kitropiki. Maporomoko yake ya pili nchini Msumbiji yalikuwa kama Kimbunga cha Tropiki na wakati kilipofika Malawi, kilikuwa kimedhoofika na kuwa na nguvu ya dhoruba ya kitropiki - ingawa ni mahali ambapo kilisababisha uharibifu mkubwa.
Storm Freddy atafanya nini baadaye?
Freddy sasa kimeisha, lakini masalia yake bado yanasababisha mvua katika maeneo ya Msumbiji na Malawi ambayo yanaweza kuzidisha hali ya mafuriko.
Kuna tofauti gani kati ya kimbunga, Dhoruba na upepo mkali ?
Zote ni dhoruba kubwa lakini jinsi zinavyofafanuliwa inategemea mahali zilipoanzia. Katika Atlantiki na Pasifiki ya Mashariki huwa vimbunga, katika Pasifiki ya Magharibi ni vimbunga na katika Bahari ya Hindi na karibu na Australiapia huitwa vimbunga.
Je kimbunga Freddy kilisababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa?
Hili ni swali gumu kujibu kwani Freddy hakika sio kawaida.
Tumeona aina hii ya dhoruba hapo awali wakati tumeona muundo wa hali ya hewa wa La Nina wenye nguvu au unaoendelea katika Bahari ya Hindi. Ofisi ya Hali ya Hewa imetangaza mwisho wa matukio ya mfululizo ya La Nina ambayo yalianza Septemba 2020.
Kwa upande wa mabadiliko ya hali ya hewa, ni ukweli unaojulikana kuwa hewa yenye joto inaweza kushikilia maji mengi kwa hivyo kiasi cha mvua iliyonyesha, haswa wakati wake juu ya ardhi, kuna uwezekano kuwa iliimarishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Maji yenye joto katika bahari hushikilia nishati zaidi, kwa hivyo basi dhoruba hizi zinaweza kuwa na nguvu zaidi kadiri muda unavyopita na kuweza kutoa mvua nyingi zaidi.
Kuongezeka kwa kasi kuna uwezekano mkubwa wa halijoto ya juu ya bahari na kwa hivyo ukweli kwamba hii ilitokea mara nyingi inaweza kuwa kwa sehemu kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Mwendo wa polepole wa dhoruba wakati mwingine, haswa kabla tu ya kuanguka kwa mara ya pili nchini Msumbiji, unaweza pia kuhusishwa.