Urusi inavyobadilisha mbinu za mashambulizi dhidi ya Ukraine, je nini kitatokea?

g

Chanzo cha picha, Ministry of Defense of the Russian Federation

Maelezo ya picha, Uzinduzi wa kombora la masafa marefu la Urusi "Iskander-M"
Muda wa kusoma: Dakika 7

Na Sergey Morfinov

BBC Ukraine

Mbinu za makombora ya Urusi dhidi ya Ukraine zimekuwa zikibadilika kwa zaidi ya miaka miwili na nusu.

Mashambulizi ya angani katika msimu wa kiangazi wa 2024 ni tofauti sana na mashambulizi ya kwanza mnamo Februari 22, 2022, na tangu lilipofanyika shambulio la kihistoria mnamo Oktoba 10, 2022, ambalo lilianza mashambulizi makubwa ya makombora dhidi ya mifumo ya nishati.

Muundo wa kutumia aina mbali mbali za mashambulizi kwa wakati mmoja, pamoja na namna ya kuchagua shabaha zinazolengwa na aina ya matumizi ya makombora fulani na droni, vimebadilika.

Kwa hivyo ni mwenendo gani wa sasa katika mashambulizi ya anga ya Urusi na ni utabiri gani wa mashambulizi unaweza kufanywa kwa siku zijazo?

Mkombora zaidi ya balestiki

Suala kuu linaloonekana ni kwamba mwenendo mkuu katika miaka yote ya vita kamili vya Urusi dhidi ya Ukraine ni ongezeko la idadi ya makombora ya masafa marefu yaliyorushwa na Warusi katika anga ya Ukraine.

h

Chanzo cha picha, Ministry of Defense of the Russian Federation

"Kiwango cha makombora ya masafa marefu kinaongezeka kila wakati," Valery Romanenko, mtaalamu wa anga kutoka Makumbusho ya shirika la safari za anga la taifa , aliiambia BBC.

Katika shambulio kubwa zaidi la anga mnamo Agosti 26, jeshi la Urusi lilitumia makombora tisa ya masafa marefu ya aina tofauti ikiwemo: "Kinzhals", "Iskander-M" na KN-23 ya Korea Kaskazini.

"Zaidi ya hayo, Warusi daima wanatafuta maeneo dhaifu ya ulinzi wa anga wa Ukraine kwa ajili ya kushambulia na makombora hayo - wakati ambapo hakuna "Patriots" na SAP/ T, ambayo inaweza kudungua makombora ya balestiki," Valery Romanenko anabainisha.

Kombora kubwa zaidi la Urusi ni "Iskander-M" - kulingana na data ya Agosti ya GUR, Warusi wanaweza kuzalisha makombora ya aina hiyo 40-50 kwa mwezi.

Walipokea makombora ya KN-23 kutoka Korea Kaskazini na katika ripoti za jeshi la Anga la Ukraine, yametajwa pamoja na "Iskander-M" bila kutofautishwa.

h

Chanzo cha picha, missilethreat.csis.org

Maelezo ya picha, Kombora la masafa marefu la KN-23 lililotengenezwa na Korea Kaskazini

Makombora ya masafa marefu ya Aeroballistic X-47M2 "Daggers" ni nadra zaidi - kulingana na data za GUR, Warusi wanaweza kutengeneza kati ya vitengo 2-6 kila mwezi, na hadi katikati ya Agosti walikuwa na makombora 55 kama hayo.

Licha ya hayo yote, "Daggers" hutumiwa mara kwa mara na Urusi - kwa mfano, katika shambulio la Lviv mnamo Septemba 4, kulikuwa na makombora mawili ya aina hiyo yaliotumika.

h

Chanzo cha picha, Ministry of Defense of the Russian Federation

Maelezo ya picha, MiG-31K na "Dagger"

Aina mbali mbali za silaha za masafa marefu za Urusi zimeweza kuongezeka hivi karibuni kutokana na makombora ya masafa mafupi ya Iran ya Fath-360, kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya Magharibi na kuafikiwa na mmoja wa wanasiasa wa Iran, na baadaye kuthibitishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken.

g

Chanzo cha picha, missilethreat.csis.org

Maelezo ya picha, Kombora la Iran Fateh-110

Tofuati ya uwezo wa makombora ya masafa inaweza kuongezeka kutokana na kombora la masafa mafupi la Iran Fath-360 ambalo linaweza kurushwa hadi kilomita 120. Kwa hivyo itakuwa tisho zaidi kwa miji ilio mstari wa mbele na mipaka, kama vile Kharkiv au Sumy.

"Lakini huu ni mfano, na baada ya hapo makombora makubwa zaidi kama vile - Fateh-110 - yanaweza kufuata. Makombora haya ya Iran ni "Iran Iskanders", Vichwa vyake vya vita vina ukubwa wa nusu tani na yanaweza kuruka kwa mamia ya kilomita," anaonya mwangalizi wa kijeshi Yigal Levin.

Ugumu na muda wa mashambulizi

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mwelekeo mwingine wa mashambulizi ya anga ya Urusi ni ongezeko makombora, uzito wake na muda wa mashambulizi.

Katika shambulio hilo la Agosti 26, Warusi walitumia jumla ya makombora 236 ya aina mbalimbali na ndege zisizo na rubani kuishambulia Ukraine.

Yote yalishambulia kutoka maeneo tofauti, katika umbali tofauti na kwa muda mrefu - ili kuifanya kazi ya ulinzi wa anga ya Ukraine kuwa mgumu kadri iwezekanavyo.

Zaidi ya "shaheed" mia moja zilipata kazi kubwa ya kupambana na ndege za mashambulizi.

Kwa ujumla, Warusi kila usiku hufanya mashambulizi kadhaa ya ndege hizi za mashambulizi nchini Ukraine, ambazo huzunguka anga kwa masaa.

Kwa mfano, usiku wa Septemba 5, Urusi ilitumia "Shaheeds" 78, ambazo zilifanya mashambulizi ya "Iskander-M" moja ndani ya Crimea na nyingine katika mkoa wa Kyiv ,mashambulizi ambayo yalidumu kwa saa 11.

Kufanya Shambulizi moja la makombora ya masafa marefu au yale ya ballistic ni mazoea ya kawaida ya Warusi .

"Wakati huo huo, Ukraine kwa mafanikio kabisa hutumia EW dhidi ya "shaheeds" – yakiwa ni makombora yenye uwezo wa kupaa : kwenda Belarus, kurudi Urusi, na "kupotea" angani," anasema Valery Romanenko.

f

Chanzo cha picha, OKB named after Gastello / Defense Express

Maelezo ya picha, "Gerbera"

Ndege hizi mpya mara nyingi hazina kitengo cha kupambana na hutumiwa kuvuruga ulinzi wa anga, kama lengo la kuwachanganya maadui .

" Gerbers ambayo mara nyingi hupaa katika anga ya Belarus baada ya kupita juu ya Ukraine, huvuruga vikundi vya mawasiliano ya simu, kukusanya ujasusi au kufanya uchunguzi wa mawasiliano ya redio.

Na Wabelarus huweza kuwakabidhi taarifa hizo Warusi, baada ya wao kwa namna fulani kutua huko. Lakini hadi sasa hii ni dhana tu, " Valeriy Romanenko anaeleza.

Pia anabainisha kuwa katika mabadiliko mengine katika mbinu za matumizi ya makombora ya "shaheed", yalianza kupaa kwa urefu wa mita 800 na zaidi, ambayo huyafanya yaonekane zaidi kufanya kazi ya ulinzi wa jadi wa anga, jambo ambalo hufanya utambuzi wake kuwa mgumu yanapokuwa angani .

"Yanapopaa urefu wa mita 50, basi mifumo ya ulinzi wa angani hupata mara kwa mara ugumu wa kuyafuatilia.

Mashambulizi dhidi ya miundombinu ya raia

Mtindo mwingine wa mabadiliko ya tabia ya makombora ya sasa ya Kirusi ni kupiga vitu vya raia: kuanzia "Okhmatdyt" huko Kyiv na kituo cha ukarabati huko Sumy hadi hoteli katika mikoa mbalimbali.

f

Chanzo cha picha, State Emergency Service

Maelezo ya picha, Usiku wa Septemba 4, Urusi yalifanya mashambulizi makubwa dhidi ya Ukraine, ya makombora kadhaa, ikiwa ni pamoja na "Daggers", yalishambulia Lviv

"Makombora matatu kati ya manne ya Urusi yanashambulia mali ya umma nchini Ukraine ikiwemo: majengo ya makazi, hospitali za watoto, taasisi za elimu, mitambo ya umeme. hli inayodaiwa kuwa ugaidi wa wazi dhidi ya raia.

Ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu," kinaandika Kituo cha Mawasiliano ya Mkakati wa Jeshi la Ukraine

"Wanablogu wa kijeshi" wa Urusi kwa kawaida huita visa kama hivyo "kazi isiyofanikiwa ya ulinzi wa anga wa Ukraine" - wanasema kuwa majengo ya raia yanapigwa na makombora ya Ukraine ya kupambana na ndege au vifusi kutoka kwa makombora ya Urusi yaliyoanguka ambayo yaliruka "kwa usahihi" kwa madhumuni ya kijeshi.

Nini kitatokea baada ya hapo?

Waangalizi wengi wanaamini kuwa makombora ya Urusi yataendelea katika msimu wa 2024 na labda yatakuwa makubwa zaidi karibu na msimu wa kiangazi.

g

Chanzo cha picha, Ministry of Defense of the Russian Federation

"Mashambulizi ya makombora yataongezeka. Kwa sababu sasa Warusi hawatumii uwezo kamili wa makombora. Na wanatafuta shabaha dhaifu katika ulinzi wa anga ya Ukraine, " Valery Romanenko anatabiri.

Mnamo Mei, WSJ iliandika kwamba Warusi wanapanga kutengeneza Shahed elfu sita katika kiwanda huko Alabuz.

"Hii ni sawa na ndege 500 kwa mwezi. Na yote haya yatakwenda kwa Ukraine, "anasema Valery Romanenko.

g

Chanzo cha picha, Air Force of the ZSU

Maelezo ya picha, Vikosi vya Ukraine vya kupambana na mashambulizi ya anga vina uzoefu mkubwa katika kukabiliana na vitisho vya Urusi. Hata hivyo, suala ni idadi ya kutosha ya mifumo ya kupambana na ndege na risasi kwao. Hasa ile yenye uwezo wa kurusha makombora ya masafa marefu.

Hali ya vitisho vya mashambulizi ya masafa marefu inaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa Iran itasafirisha makombora yake kwa Warusi

Muangalizi wa kijeshi Oleksandr Kovalenko anaamini kwamba kwa upande wa makombora ya Urusi, mashambulizi ya Septemba hayawezi kuzidi ya Agosti na shambulio lake kubwa zaidi wakati wa Siku ya Uhuru wa Ukraine.

" Kwa upande wa shughuli za makombora na Shahed-131/136, ya mwezi Septemba hayapaswi kuwa makali zaidi, au sawa na yale ya Agosti. Inawezekana kwamba sasa amri ya vikosi vya Urusi katika masuala ya mashambulizi ya makombora na mashambulizi ya droni itazingatia zaidi msimu wa kiangazi, "anaandika.

"Ndiyo maana ni muhimu sana kwa Ukraine kupata makombora zaidi ya kupigana dhidi ya makombora ya masafa marefu. Na pia - ruhusa ya kuishambulia Urusi kwa silaha za Magharibi , " Valery Romanenko anaelezea.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Seif Abdalla