Steve Rosenberg: Uvamizi wa Ukraine unaonyesha vita vya Urusi haviendi kama ilivyopangwa

Vladimir Putin during a meeting of the security council

Chanzo cha picha, Kremlin Handout

    • Author, Steve Rosenberg
    • Nafasi, Mhariri BBC Russia
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine ulichukuliwa na Kremlin kama operesheni fupi ya kijeshi.

Matarajio yalikuwa kwamba itachukua muda wa siku, kadhaa au wiki chache ikizidi sana, kwa Urusi kufikia udhibiti wa jirani yake.

Hiyo ilikuwa karibu miaka miwili na nusu iliyopita.

Vita nchini Ukraine vinaendelea. Mambo hayajaenda kabisa jinsi Moscow ilivyokusudia.

Katika kipindi cha miezi 29 iliyopita, mara nyingi tumesikia maafisa wakuu wa Urusi wakidai kwamba operesheni inakwenda "kulingana na mpango."

Rais Vladimir Putin alisema mara ya mwisho mnamo Mei kwamba, licha ya yote yaliyotokea katika miaka miwili iliyopita: majeruhi makubwa ya wanajeshi wa Urusi kwenye uwanja wa vita, uharibifu wa meli nyingi za kivita za Urusi katika Bahari nyeusi, mashambulizi ya ndege zisizo na rubani ndani ya Urusi ( hata mjini Kremlin kwenyewe. ), mashambulizi ya makombora ya miji na vijiji vya Urusi karibu na mpaka wa Ukraine, uasi wa wapiganaji mamluki wa Wagner ambao walikuwa wameenda Moscow.

Katika orodha hiyo ndefu sasa kmeongezeka: shambulio la wiki hii la uvamizi wa Ukraine kwenye eneo la Kursk nchini Urusi.

Ni vigumu kujua ni nini hasa kinachoendelea kwa sasa katika wilaya ya Sudzha ya mkoa wa Kursk. Haijulikani ni wanajeshi wangapi wa Ukraine waliopo, wameteka maeneo yapi na lengo lao la ni lipi hasa.

Toleo la Alhamisi la gazeti la Urusi Nezavisimaya Gazeta lilitangaza: "Matukio yanayoendelea Kursk yamegubikwa na ukungu mbaya wa vita."

Lakino licha ya ukungu huo, mambo mengine yako wazi.

Ni dhahiri kwamba kile kinachotokea katika eneo la Kursk ni ushahidi zaidi kwamba vita vya Urusi nchini Ukraine havijaenda "kulingana na mpango". Matukio yanaonekana kuushangaza uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Urusi.

Usitarajie Moscow kukubali hilo.

Uwezekano mkubwa zaidi, maafisa wa Urusi watatumia shambulio la Ukrainekujaribu kukusanyika umma wa Urusi kuzunguka serikali na kuunga mkono maelezo rasmi ya Kremlin kwamba:

  • katika mzozo huu Urusi sio mvamizi
  • Urusi ni nchi iliyozingirwa maadui wanaopanga kuivamia na kuiharibu.
Soma pia:
Ramani
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ukweli ni kwamba Urusi ndio iliyovamia jirani yake Ukraine.

Kuna tofauti kubwa katika lugha. Wakati Urusi ilipowaelekeza wanajeshi wake kuvuka mpaka na kuingia Ukraine mnamo Februari 2022, Kremlin iliitaja hatua hiyo kuwa "operesheni maalum ya kijeshi" na kudai kwamba Urusi "inakomboa" miji na vijiji.

Moscow imetaja hatua ya hivi punde ya wanajeshi wa Ukraine kuingia eneo la Urusi kuwa "shambulio la kigaidi" na "uchokozi."

Mashambulio ya vikosi vya Ukraine katika eneo la Kursk na mapigano makali katika eneo hilo ni ishara kwamba uhasama unakaribia nyumbani. Lakini hiyo itageuza mtazamo wa watu wa Urusi dhidi ya vita hivyo?

Si lazima iwe hivyo.

Mwaka jana nilitembelea Belgorod, eneo la Urusi ambalo, kama Kursk, linapakana na Ukraine. Lilikuwa linashambuliwa kwa makombora kutoka nje ya mpaka.

Kila mtu niliyekutana naye aliniambia kuwa hajawahi kushuhudia shambulio kama hilo kabla ya uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine: kabla ya Februari 2022 kulikuwa na amani na utulivu katika eneo la Belgorod.

Lakini badala ya kuhitimisha kwamba "operesheni maalum ya kijeshi" imekuwa kosa, watu wengi niliozungumza nao waliitaka Urusi kuongeza hatua yake ya kijeshi na kuingia ndani zaidi ya eneo la Ukraine.

Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev aliunga mkono msimamp huo. Katika chapisho la mtandao wa kijamii laliandika:

"Tunaweza na tunapaswa kuchukua ardhi zaidi ya Ukraine ambayo bado ipo. [Tunapaswa kufika] Odesa, Kharkiv, Dnipro, Mykolaiv. Kwa Kyiv na zaidi.

Lakini Dmitry Medvedev hana uwezo wa kutoa amri hiyo. Vladimir Putin anaweza kufanya hivyo. Tunadubiri kuona jinsi atakavyojibu kile ambacho kimekuwa siku chache za kushangaza kusini mwa Urusi.

Maelezo zaidi:

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi na kuhaririwa na Yusuf Jumah