Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 22.05.2023

Chanzo cha picha, EPA
Chelsea wamewasilisha ofa ya euro milioni 80 kwa Juventus kumnunua mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 23. (ESPN)
Manchester United pia wanaandaa ofa rasmi kwa ajili ya Vlahovic, ambaye ameweka wazi kuwa anataka kucheza soka la Ligi ya Mabingwa msimu ujao. (Football Transfers)
Leicester City wanapanga kuwasiliana na mkufunzi wa zamani wa Brighton na Chelsea Graham Potter kuhusu kuwa meneja wao wa kudumu. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi wa Roma Jose Mourinho anataka kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 utakapokamilika mwishoni mwa msimu. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Barcelona wamefikia makubaliano na wakala Jorge Mendes kuhusu uhamisho wa kiungo wa Wolves Ruben Neves, 26, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno akitarajiwa kuhamia Nou Camp kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana na mshambuliaji wa Uhispania Ansu Fati, 20. (Sport - kwa Kihispania)
Aston Villa wanatafakari uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 27, kwa mkopo msimu ujao. (Football Transfers)

Chanzo cha picha, Empics
Crystal Palace wana pania kumnunua kiungo wa kati wa Bournemouth na Colombia Jefferson Lerma, huku mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 na Cherries ukitarajiwa kumalizika msimu huu. (Sun)
Nottingham Forest itaka kumpatia mkataba wa kudumu kipa wa Manchester United na Uingereza aliyejiunga nao kwa mkopo Dean Henderson, 26. (Telegraph - usajili unahitajika)
Manchester City wako tayari kumuuza mlinda lango Zack Steffen, 28, msimu huu wa kiangazi wakati muda wa mkopo wa Mmarekani huyo akiwa Middlesbrough utakapomalizika. (Sun)

Chanzo cha picha, Rex Features
Aston Villa na Wolves wanamuwania kiungo wa kati Mfaransa Habib Diarra 19, kutoka Strasbourg, ambaye thamani yake ni pauni milioni 20. (Sun)
Manchester United wanajadiliana kuhusu uwezekano wa kurefusha mkataba wa winga wa Uruguay Facundo Pellistri, 21 hadi Juni 2028. (Fabrizio Romano).














