Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Liverpool inaongoza mbio za kumsajili Antoine Semenyo

Muda wa kusoma: Dakika 3

Liverpool imeungana na Tottenham katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana Antoine Semenyo, 25. (Team talk)

Meneja wa Manchester United Ruben Amorim anavutiwa na Semenyo lakini kufikia kipengee chake cha pauni milioni 65 na Bournemouth itakuwa vigumu kwa klabu kufanya hivyo Januari. (Athletic - usajili inahitajika)

Klabu ya Brighton inataka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Real Madrid Mhispania Gonzalo Garcia, 21, mwezi Januari, huku Leeds na Sunderland pia wakimuwania. (Mail)

Manchester United na Borussia Dortmund wako mbioni kusaka saini ya mshambuliaji wa Sweden Kevin Filling kutoka AIK Stockholm, 16. (Florian Plettenberg)

AC Milan inavutiwa na mshambuliaji wa Ujerumani Niclas Fullkrug, 32, ambaye anaweza kuondoka West Ham mwezi Januari. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)

Vilabu vya West Ham, Everton na Roma vinakamia kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Joshua Zirkzee, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 24, akiwa pembeni ya Old Trafford. (The I - Usajili unahitajika)

Barcelona inamfuatilia kwa karibu mlinzi wa Crystal Palace Marc Guehi, 25, lakini Liverpool bado wanapigiwa upatu kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza. (Cadena SER - kwa Kihispania)

Mshambulizi wa Senegal Nicolas Jackson, 24, atasalia Bayern Munich kwa mkopo wa msimu mzima badala ya kurejea katika klabu yake ya Chelsea Januari. (Football Insider)

Mkufunzi wa Fulham Marco Silva anajiandaa kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu hiyo. Mkataba wa sasa wa Mreno huyo Craven Cottage unarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu. (Sky Sports)

Mazungumzo kati ya Manchester United na Kobbie Mainoo kuhusu kandarasi mpya yamesitishwa huku kiungo huyo wa kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 20 akitarajia kuhamia Napoli kwa mkopo mwezi Januari ili kupata muda zaidi wa kucheza. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Manchester United ilikataa ofa ya Chelsea ya kumjumuisha kiungo wa kati wa Ubelgiji Romeo Lavia, 21, au mshambuliaji wa Ufaransa Christopher Nkunku, 28, kama sehemu ya makubaliano ambayo yalimfanya winga wa Argentina mwenye umri wa miaka 21 Alejandro Garnacho kujiunga na The Blues. (ESPN)