Trump: Ninaweza kumaliza vita vya Ukraine kwa siku moja tu

Chanzo cha picha, ALEX WONG
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema Jumapili kwamba anaweza kusimamisha vita vya Ukraine ndani ya siku moja ikiwa atachaguliwa tena kuwa rais wa Marekani, akiapa kutokomeza kile alichokitaja kuwa "deep state" kwa kiingereza au udhibiti wa sera ya serikali.
Na mbele ya umati wa wafuasi wake wakati wa kongamano la kila mwaka la viongozi wa kihafidhina, Trump aliahidi kumaliza mzozo huo ambao umedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa kusema: "Nitatatua tatizo na nitalitatua haraka iwezekanavyo, na haitachukua zaidi ya siku moja. Ninajua vyema nitakachosema kwa pande zote mbili."
Wakati wa mkutano wa siku tatu wa mrengo wa kulia huko Washington, DC, Trump alisisitiza kuwa hakutakuwa na vita tena, akisema, "Ningezuia Vita vya Tatu vya Dunia kwa urahisi sana."

Chanzo cha picha, PACIFIC PRESS
Trump aliahidi, wakati wa hotuba ya saa mbili, kuokoa Marekani kutoka kuwa "jinamizi chafu la kikomunisti"; Na hii ni kwa kuondokana na "udhibiti wa sera ya serikali" na kupindua sera za Rais wa sasa wa Marekani, Joe Biden, ikiwa atapata nafasi ya pili ya urais, akisisitiza kuwa yeye ndiye mtu pekee anayeweza kuifanya Marekani kuwa bora tena, na kuahidi kung'oa "udhibiti wa sera ya serikali" kutoka kwa mizizi yake, nitawafukuza watendaji wa serikali ambao hawajachaguliwa, ni watu wagonjwa."
Chama cha Trump chakumbwa na vita vya ndani huku utafutaji kura 2024 ukianza
Wakati kinyang'anyiro cha urais wa 2024 kinapoanza, mashirika ya ndani ya chama cha Republican katika maeneo mengi ya Marekani yanatawaliwa na uasi, mizozo ya ndani kwa ndani na kesi za mahakamani kiasi kwamba baadhi ya maafisa na wataalamu wa mikakati wanasema yanaweza kuharibu nafasi ya chama hicho kurejea White House.
Shirika lahabari la Reuters lilizungumza na zaidi ya watendaji 50, wanaharakati na maafisa wa chama katika majimbo ya ushindani ya Arizona, Georgia na Nevada, ambayo Trump alipoteza kidogo mnamo 2020; North Carolina, ambayo alishinda; na katika jimbo kuu la msingi la South Carolina. Nevada pia inashikilia ushindani wa mapema katika uteuzi wa rais.
Baadhi ya wataalamu wa mikakati na maafisa walionya kuna uwezekano wa kuwa na chama kinachopigana chenyewe wakati wa uchaguzi na majimbo ya awali yanahatarisha kutovutia wapiga kura wala wafadhili.
"Kiwango tunachoweza kusimamia hili kitaamua jinsi mgombea wetu wa urais anavyofanya vyema," alisema Maurice Washington, mwenyekiti wa Chama cha Republican katika Kaunti ya Charleston ya South Carolina, eneo ambalo mara kwa mara wagombea urais hufika kuomba kura.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Siku zote kuna uwezekano wa mienendo ya tabia kubadilika njiani wakati wa kupiga kura," Washington ilisema.
Ingawa ni mapema sana kuona athari za moja kwa moja za mvutano huu wa ndani ya chama, na ugomvi huu unaweza kupungua mara tu mgombea mteule wa rais atakapochaguliwa, Ronna McDaniel, mkuu wa Kamati ya Kitaifa ya Republican alisema.
Larry Hogan, mkosoaji wa Trump ambaye aliondoka madarakani Januari baada ya kuhudumu kwa mihula miwili kama gavana wa Republican wa Maryland, aliambia Reuters ni muhimu kwa chama hicho kusonga mbele zaidi ya rais huyo wa zamani ikiwa kinataka kushinda uchaguzi wa 2024.
Wanademocrat walifanya vyema zaidi ya matarajio yao katika uchaguzi wa katikati ya muhula wa Novemba 2022, katika sehemu nyingi kwa sababu wapiga kura waliepuka kampeni nyingi za wagombea wanaoungwa mkono na Trump, na wenye siasa kali za mrengo wa kulia.
"Wapiga kura walituma ujumbe wa wazi katika chaguzi tatu zilizopita: wanataka umahiri na suluhisho la akili ya kawaida, sio mambo ya wazimu wazimu zaidi," Hogan alisema.
"Ikiwa tunataka kuanza kushinda tena, basi lazima tuanze kusikiliza."
Sio kila mtu anakubali. Mwakilishi wa Jimbo la Carolina Kaskazini Mark Brody, ambaye anaunga mkono kukemea Seneta Tillis, anasema ni bora kushughulikia tofauti moja kwa moja.
Kongamano la 2023 lilishuhudia hotuba za baadhi ya wafuasi shupavu wa Trump, pamoja na watu kadhaa wanaotarajiwa kuwania urais wa 2024.















