Kombe la Dunia 2022: Wachezaji 17 waliozaliwa Afrika wanaoyawakilisha mataifa nje Afrika

Na Dinah Gahamanyi

BBC News Swahili

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ansu Fati

Huku mashindano ya soka ya Kombe la Dunia yakiendelea nchini Qatar, maswali yamekuwa yakiibuka, mijadala imekuwa ikiibuka hususan miongoni mwa baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kuhusu wachezaji waliozaliwa Afrika wanaochezea timu za zisizo za Kiafrika.

Mjadala huu ulipamba moto zaidi Wiki hii wakati Rais wa Liberia mwanasoka wa zamani wa kimataifa George Weah alipompongeza mtoto wake wa kiume, Timothy Weah, baada ya klabu yake ya Lille kushinda taji la Ligi Kuu ya Ufaransa.

"Mimi mwenyewe kama mshindi wa taji la Ligue 1, nafahamu fika kwamba unahitaji kujitolea na kufanya kazi kwa bidii kila wiki ili kupata ushindi ,” Rais Wear alisema katika ujumbe uliowekwa katika tovuti yake rasmi ya urais.

“Licha ya kuumia mara kadhaa na kucheza mechi 28 , hiki ni kitu ambacho kimekuwa ndoto ya Tim. Japo baba yake Timothy Wear alizaliwa ni rais wa Liberia, binafsi Tim alizaliwa Brooklyn nchini Marekani na ana uraia wa Marekani.

Lakini je ni wachezaji gani waliozaliwa Afrika wanaozichezea timu zisizo za Afrika katika Kombe la Dunia la mwaka huu? Na wanachezea timu gani?:

 1. Ansu Fati.(Uhuspania)

Alizaliwa mjini Bissau nchini Guinea Bissau.

2. Alphonso Davies.(Canada)

Alizaliwa Buduburam, Ghana.

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Eduardo Camavinga

3. Eduardo Camavinga.(Ufaransa)

Alizaliwa Cabinda nchini Angola na wazazi wake walikuwa Wacongo

4. Youssoufa Moukoko. (Ujerumani)

Alizaliwa Younde nchini Cameroon

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Danilo Pereira

5. Danilo Pereira.(Ureno)

Alizaliwa mjini Bissau, nchini Guinea Bissau

6. Steve Mandanda.(Ufaransa)

Alizaliwa mjini Kinshasa katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Breel Embolo

7. Breel Embolo.(Uswizi-Switzerland)

Alizaliwa mjini Yaounde nchini Cameroon

8. Mohammed Muntari. (Qatar)

Alizaliwa Kumasi, nchini Ghana

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Amadou onana

9. Amadou onana.(Ubelgiji)

Alizaliwa mjini Dakar, nchini Senegal

10. Ismail Kone.(Canada)

Alizaliwa Abidjan, nchini Ivory Coast.

11. Keanu Baccus.(Australia)

Alizaliwa Durban nchini South Africa.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Musab Kheder

12. Musab Kheder.(Qatar)

Alizaliwa Khartoum, nchini Sudan.

13. Boualem Khoukhi.(Qatar)

Alizaliwa Bou Ismail nchini Algeria.

14. William Carvalho.(Ureno)

Alizaliwa Luanda, Angola.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Thomas Deng

15. Thomas Deng.(Australia)

Msudan Kusini aliyezaliwa kama mkimbizi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, nchini Kenya.

16. Awer Mabil.(Australia)

Msudan Kusini aliyezaliwa kama mkimbizi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, nchini Kenya.

17. Garang Kuol.(Australia)

Alizaliwa nchini Misri