Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini usingizi wa vijana ni muhimu sana kwa afya ya akili?
Wakati fulani vijana wanaweza kutatizika kuamka kitandani asubuhi - lakini kuhakikisha wanapata usingizi wakutosha kunaweza kuwa muhimu kwa afya katika maisha ya baadaye.
Ni asubuhi sana na vijana ndani ya nyumba bado wamelala fofofo muda mrefu baada ya wewe kuamka. Je, unapaswa kukimbilia chumbani mwao na kuwavuta kutoka kitandani mwao? Unaweza kuona kuwa labda ni jambo jema, lakini jibu huenda likawa ni hapana. Ushahidi wa kisayansi unaendelea kuongezeka ukionyesha kwamba usingizi katika ujana ni muhimu kwa afya ya akili ya sasa na ya baadaye.
Haipaswi kushangaza kwamba ukosefu mkubwa wa usingizi, au kupata usingizi kwa shida sana, ni mojawapo ya dalili za kawaida za msongo wa mawazo miongoni mwa vijana.
Baada ya yote, hata kama wanaweza kuhisi uchovu, ni vigumu kuondokana na msongo ikiwa wana mashaka au wasiwasi mwingi. Hii pia hutokea kwa watu wazima pia, huku 92% ya watu walio na msongo wa mawazo wakilalamikia shida za kulala.
Jambo ambalo labda halieleweki ni kwamba, kwa wengine, matatizo ya kulala yanaweza kuanza kabla ya mfadhaiko, na hivyo kuongeza hatari ya matatizo ya afya ya akili katika siku zijazo . Je, hii ina maana kwamba usingizi kwa vijana unapaswa kuchukuliwa kwa uzito zaidi? Na inaweza kupunguza hatari ya msongo wa mawazo baadaye?
Katika utafiti uliochapishwa mwaka wa 2020 , Faith Orchard, mwanasaikolojia katika Chuo Kikuu cha Sussex, alichunguza data kutoka katika kundi kubwa la vijana kuanzia umri wa miaka 15 hadi 24. Wale ambao waliripoti kulala vibaya katika umri wa 15, ' Waliokuwa na msongo wa mawazo au wasiwasi wakati huo, walikuwa na uwezekano zaidi kuliko wenzao kuwa na wasiwasi au mfadhaiko walipofika miaka 17, 21 au 24.
Pamoja na watu wazima pia, matatizo ya usingizi yanaweza kuwa kiashiria cha kupatwa na msongo wa mawazo kwa siku zijazo.
Uchunguzi wa meta wa tafiti 34, ambazo miongoni mwake zilifuatilia maisha ya watu 150,000 kwa kipindi cha kati ya miezi mitatu na miaka 34, uligundua kwamba iwapo watu walikuwa na matatizo ya usingizi, hatari yao ya kupata mfadhaiko baadaye iliongezeka maradufu.
Bila shaka, si lazima kwamba kila mtu asiye na usingizi atapatwa na msongo wa mawazo baadaye. Watu wengi hawataupata.
Jambo la mwisho ambalo watu wenye kukosa usingizi wanahitaji bila shaka, ni wasiwasi juu ya nini kinaweza kutokea kwao katika siku zijazo.
Lakini unaweza kuona kwa nini katika matukio fulani usingizi duni unaweza kuchangia afya mbaya ya akili. Upungufu wa usingizi una athari mbaya kwetu, ikiwa ni pamoja na tabia ya kujitenga na marafiki na familia, ukosefu wa motisha na yote hayo tanaweza kuathiri mahusiano ya mtu na kuwa katika hali ya msongo wa mawazo.
Zaidi ya hayo kuna mambo ya kibiolojia ya kuzingatia. Ukosefu wa usingizi unaweza kusababisha kuongezeka kwa kuvimba kwa mwili (inflammation), ambayo imehusishwa na matatizo ya afya ya akili.
Watafiti sasa wanachunguza uhusiano kati ya tatizo la ukosefu wa usingizi na hali zingine za afya ya akili.
Hata wakati matatizo ya afya ya akili yanapotangulia kuvurugika kwa usingizi, kukosa usingizi kunaweza kuzidisha matatizo ya mtu.
Mwanasaikolojia wa kimatibabu Daniel Freeman, ametaka matatizo ya usingizi yapewe kipaumbele cha juu ndani ya huduma ya afya ya akili . Kwa sababu ni kawaida katika utambuzi tofauti, huwa hazizingatiwi kama msingi wa hali fulani.
Anahisi wakati mwingine hupuuzwa, wakati wangeweza kushughulikiwa.
Hata wakati matatizo ya afya ya akili yanapotangulia usingizi uliovurugika, kukosa usingizi kunaweza kuzidisha matatizo ya mtu. Baada ya yote, usiku mmoja tu wa kukosa usingizi una athari mbaya juu ya hisia na fikra.
Hii inaonyesha kuwa matatizo ya ukosefu wa usingizi na matatizo ya afya ya akili yanaweza kutokana na sababu sawa. Matukio ya kutisha au mabaya, kwa mfano.
Na, kama tumeona tayari, kuna uwezekano kwamba kukosa usingizi na masuala ya afya ya akili huzidisha kila mmoja, na kufanya masuala yote mawili kuwa mabaya zaidi.
Inawezekana pia kwamba ukosefu wa usingizi sio sababu ya msongo wa mawazo wa wa siku zijazo maishani , lakini ni ishara ya uwezekano wa tatizo hilo kutokea baadaye.
Kwa hivyo labda masuala usingizi unapaswa kuchukuliwa kwa uzito zaidi kwa vijana na watu wazima
Jaribio kubwa la Oasis lililoongozwa na Daniel Freeman katika vyuo vikuu 26 nchini Uingereza liligundua kuwa tiba ya utambuzi wa kitabia ya kidijitali kwa wanafunzi walio na usingizi, sio tu uliwasaidia kulala, lakini ilipunguza tukio la kuona na kuwa na wasiwasi , dalili za saikolojia.
Swali kuu ni kama hatua za kulala zinaweza hata kuzuia matatizo ya afya ya akili . Ili kujibu hili, majaribio makubwa, ya muda mrefu yanahitajika.
Faida moja ya hatua za awali na bora za kuzuia usingizi duni wenyewe na uwezekano wa kupunguza matatizo mapana ya afya ya akili - ni kwamba kuna unyanyapaa mdogo unaozunguka kukosa usingizi, kwa hivyo inaweza kuwa rahisi kuwashawishi watu kujitokeza kupata matibabu ya tatizo hili.
Kupata usingizi bora peke yake hakuwezi kutatua mgogoro wa afya ya akili, bila shaka
Wakati huo huo, mtu yeyote ambaye ana tatizo la kupata usingizi anaweza kujaribu mbinu zilizoonyeshwa kuwa za ufanisi zaidi: kuhakikisha kupata mwanga wa kutosha wakati wa mchana (asubuhi kwa watu wengi); si kulala kwa muda mrefu zaidi ya dakika 20; kutokula au kufanya mazoezi au kunywa kafeini jioni sana; epuka kusoma barua pepe zako au kujadili mada zenye ugumu kitandani; kuweka chumba cha kulala baridi, kimya na giza; na kujaribu kuamka na kwenda kulala kwa wakati mmoja kila siku.
Kupata usingizi bora peke yake hakuwezi kutatua mgogoro wa afya ya akili, bila shaka. Lakini inaweza kuleta mabadiliko kwa muda mrefu? Hata kama ukosefu wa usingizi hautakusababishia msongo wa mawazo hakuna kitu bora kama kupata usingizi wa kutosha kwa vijana.