Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ukraine: Marekani na nchi za Ulaya zaahidi kutoa silaha nzito kwa Kyiv
Nchi zaidi zimejibu wito wa Rais Volodymyr Zelensky wa kutuma silaha zaidi nchini Ukraine.
Marekani inasema kifurushi cha thamani ya $2.5bn (£2bn) kitatumwa, ikijumuisha magari ya kivita na mifumo ya ulinzi wa anga.
Mataifa kadhaa ya Ulaya yaliahidi vifurushi vyao vipya - ikiwa ni pamoja na mamia ya makombora yaliyoahidiwa Kyiv na Uingereza.
Matangazo hayo yanakuja kabla ya mkutano wa dharura uliopangwa kufanyika nchini Ujerumani siku ya Ijumaa, ambapo nchi 50 zimepangwa kuratibu usambazaji wa silaha.
Mkutano wa Alhamisi uliwashuhudia wawakilishi kutoka mataifa 11 wakikusanyika katika kambi ya jeshi nchini Estonia kujadili aina mbalimbali za vifurushi vipya vya kuisaidia Ukraine kutwaa tena eneo na kuzuia maendeleo yoyote zaidi ya Urusi.
Nchi tisa - Uingereza, Poland, Latvia, Lithuania, Denmark, Jamhuri ya Czech, Estonia, Uholanzi na Slovakia - ziliahidi msaada zaidi.
Vifurushi vilivyotangazwa katika taarifa ya pamoja ni pamoja na:
- Uingereza - makombora 600 ya Brimstone
- Denmark - Kaisari 19 waliotengenezwa na Ufaransa wanaojiendesha wenyewe
- Estonia - vipita, risasi, magari ya usaidizi na vizindua vya mabomu ya kukinga tanki
- Latvia - Mifumo mikali ya ulinzi wa anga, helikopta mbili, na ndege zisizo na rubani
- Lithuania - bunduki za kupambana na ndege na helikopta mbili
- Poland - bunduki za kupambana na ndege za S-60 na vipande 70,000 vya risasi
- Jamhuri ya Czech - kuzalisha zaidi caliber risasi kubwa, howitzers na APCs
Uholanzi itatangaza kifurushi chake cha msaada siku ya Ijumaa.
Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Estonia, Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace alisema: "Mwaka 2023, ni wakati wa kugeuza kasi ambayo Waukraine wamefikia katika kurudisha nyuma Urusi katika mafanikio na... uhuru, ambayo ni haki yao chini ya sheria za kimataifa."
Tangazo la usaidizi mpya wa Marekani lilifika baadaye siku ya Alhamisi. Licha ya matumaini ya Kiukreni, haikuwa na ofa ya mizinga.
Lakini Pentagon iliahidi Kyiv magari ya ziada 59 ya kivita ya Bradley, magari 90 ya kubeba wanajeshi ya Stryker na mifumo ya ulinzi wa anga ya Avenger, kati ya risasi zingine kubwa na ndogo.
Ilisema mashambulizi ya hivi karibuni ya anga yalionyesha "athari mbaya ya vita vya kikatili vya Urusi nchini Ukraine" - lakini ikasema kuwa silaha mpya zilizoahidiwa zitasaidia kukabiliana na haya.
Taarifa iliongeza kuwa Marekani sasa imetoa zaidi ya $26.7bn katika usaidizi wa usalama kwa Ukraine tangu uvamizi kamili wa Moscow tarehe 24 Februari 2022.
Mkutano wa Kundi la Ulinzi la Ukraine, linaloundwa na washirika wakuu ikiwa ni pamoja na Marekani, utafanyika katika kituo cha anga cha Ramstein nchini Ujerumani siku ya Ijumaa ili kujadili msaada zaidi wa kijeshi.
Rais Zelensky alisema anatarajia "maamuzi makali" juu ya mauzo zaidi ya silaha kufanywa katika mkutano huo, ikiwa ni pamoja na "mfuko wa msaada wa kijeshi" kutoka Marekani.
Mazungumzo hayo yana uwezekano wa kuzingatia suala la kupeleka mizinga mizito, na hasa ni nani atakayeisambaza. Licha ya mabilioni ya dola yaliyoahidiwa katika silaha mpya na washirika wa Magharibi siku ya Alhamisi, swali hili bado halijajibiwa.
Ukraine inaomba mizinga ya Leopard iliyotengenezwa Ujerumani kutumwa mstari wa mbele.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anakabiliwa na shinikizo la kimataifa na la ndani ili kuzisambaza, au angalau kuidhinisha uwasilishaji wao na nchi nyingine.
Poland na Finland zote zimeahidi kutuma Leopards zao - lakini zinahitaji kibali cha Ujerumani, kama nchi ya iliyozitengeza, kufanya hivyo.
Waziri Mkuu wa Poland, Mateusz Morawiecki, alisema "ana mashaka kiasi" kuhusu Ujerumani kutoa kibali cha kusafirisha tena Leopards kwenda Ukraine.
Na Rais Zelensky pia amezungumzia kusitasita kwa Ujerumani.
"Sasa tunasubiri uamuzi kutoka kwa mji mkuu mmoja wa Ulaya ambao utawezesha minyororo iliyoandaliwa ya ushirikiano kwenye mizinga," alisema Alhamisi jioni.
Chanzo cha serikali huko Berlin kiliiambia Reuters kuwa bado haijapokea ombi kutoka kwa nchi yoyote ya kusafirisha tena mizinga yao.
Uingereza ilikuwa taifa la kwanza kutoa mizinga kwa Ukraine ilipoahidi kutuma 14 aina ya Challenger 2.