Kiongozi wa mapinduzi ya Niger Jenerali Tchiani: Mlinda amani wa zamani wa Umoja wa Mataifa aliyenyakua mamlaka

Wafuasi wengi wa serikali ya kijeshi wamechukua msimamo wa kuunga mkono Urusi dhidi ya Ufaransa na ambao ni nadra.

Anaonekana kuwa mtu wa faragha, kwa namna fulani hata asiyejulikana sana na marais waliojikabidhi kwa ulinzi wake.

Ilijulikana kuwa uhusiano wake na Bw Bazoum, mshirika wa muda mrefu wa Bw Issoufou, ulikuwa wa mbali zaidi na katika wiki za hivi majuzi kulikuwa na uvumi kwamba rais alikuwa akijiandaa kumlazimisha kustaafu.

Labda chuki za kibinafsi zilikuwa zimekusanyika, hazikuangaziwa lakini bado zikawa na nguvu.

Kuondolewa kwenye wadhifa wake, hata katika umri wa kawaida wa kustaafu, bila shaka kungekuwa pigo kubwa kwa mtu ambaye kwa zaidi ya miongo minne amepanda madaraja hatua kwa hatua, baada ya kuanza kama mwanajeshi wa kawaida.

Jenerali Tchiani anatoka katika kabila kubwa la Wahausa, na anatoka eneo la Tillabéri, eneo ambalo ni asili ya wanajeshi wengi wa Niger.

Hata hivyo, yeye hakuwa na nguvu au uhusiano wa kisiasa. Alilazimika kufanya kazi kutoka chini hadi ngazi kubwa aliyofikia.

Bw Bazoum pia ni mtu ambaye alitoka katika malezi ya kiasi na kisha akapanda ngazi ya elimu na taaluma hatua kwa hatua, katika chuo kikuu na kisha akawa mwalimu wa shule ya sekondari na mwanaharakati wa vyama vya wafanyakazi, kabla ya kuingia katika siasa mapema miaka ya 1990.

Lakini cha kushangaza, Jenerali Tchiani hakuwahi kuanzisha uhusiano mzuri wa kufanya kazi na Bw Bazoum - ilhali anaonekana kupatana kwa urahisi na Bw Issoufou.

Sasa bila shaka, baada ya miaka mingi nje ya macho ya umma, Jenerali Tchiani anajikuta kwenye mkondo wa mzozo katika usimamizi wa migogoro ya kisiasa na kidiplomasia.

Kufikia sasa ametegemea kile ambacho kwa miaka mingi jeshini kimekuwa nguzo yake kuu: kujizuia, kusitasita kwa uangalifu kusema mawazo yake kikamilifu mbele ya wengine, na kukataa maelewano.

Lakini Jenerali Tchiani na utawala mzima wa kijeshi wamezua chuki dhidi ya Ufaransa miongoni mwa Wanigeria wengi na atajaribu kubadilisha hali hiyo kuwa msingi mpana wa uungwaji mkono kwa mapambano na Ecowas.

Na huku majaribio haya yakikabiliana na Nigeria na wanachama wengine wa kambi ya Afrika Magharibi katika siku zijazo, na huku vikwazo vikizidi kuleta athari na kusababisha ongezeko la gharama ya maisha kwa watu wa kawaida, mbinu hii mpya itachukua jukumu muhimu huku jenerali huyo akicheza kamari ya kiwango cha juu ikilinganishwa na kazi yake ya awali.

Jenerali Tchiani amewaacha viongozi wengine wa utawala wa kijeshi kupigia debe mapinduzi hayo kwa umma.

Mwenyekiti wa sasa wa Ecowas, Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, sasa amesisitiza kuchukuliwa hatua za kidiplomasia na dalili zaidi ya jinsi yeye na wenzake wanavyofikiria inaweza kujitokeza baada ya mkutano wao inaofanyika mjini Abuja siku ya Alhamisi, Agosti 10.

Kutokana na hali hii ya kutokuwa na uhakika, na kutiwa moyo na mafanikio ya viongozi wenzake wa mapinduzi nchini Mali, Burkina Faso na Guinea katika kukabiliana na shinikizo la kikanda, inaonekana kwamba Jenerali Tchiani kwa sasa ameamua kujinyenyekeza na kucheza mchezo huo kwa muda mrefu.

Utawala wake umetangaza uteuzi wa waziri mkuu, waziri wa zamani wa fedha na afisa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Ali Mahaman Lamine Zeini – kuashiria matamanio yake ya kuanzisha kipindi kirefu cha mpito wa kisiasa.

Baadhi ya wachambuzi wamejiuliza iwapo kupinduliwa kwa Bw Bazoum, ambaye anatoka katika jamii ya Waarabu walio wachache, huenda kukazua mzozo wa kikabila nchini Niger.

Hata hivyo, hisia kali ya mshikamano wa tamaduni mbalimbali na utambulisho wa kitaifa daima imekuwa nguvu ya dhahiri ya Niger kisasa.

Aliyekuwa Muasi wa kundi la Tuareg pia waziri mkuu, Rhissa Ag Boula, sasa amezindua kampeni ya kumrejesha ofisini Bw Bazoum. Na hadi sasa hakuna dalili ya utawala wa kijeshi kujitosa kwenye njia inayoyagawanya madhehebu ya dini.

Hata hivyo, Jenerali Tchiani hayupo kujihatarisha. Uamuzi wa kumweka katika kizuizi cha nyumbani Bw Bazoum na kuandaa mapinduzi yenyewe ulikuwa kamari ya hali ya juu. Iwapo ingeshindikana, ni jenerali mwenyewe ambaye sasa angekuwa katika mahabusu.

Na uaamuzi wa kushutumu hadharani makubaliano ya muda mrefu ya ulinzi na ukoloni wa zamani wa Ufaransa na, kutafuta usaidizi wa mamluki wa Kirusi wenye utata Wagner, walikuwa na uhakika wa kuwachukiza zaidi Ecowas na serikali za Magharibi, licha ya kwamba wanaungwa mkono na raia wasiompenda rais Bazoum huko Niamey.

Katika kipindi cha takriban miaka 40 ya kazi yake, Jenerali Tchiani amepata mafunzo yake katika vyuo vya kijeshi nchini Senegal, Ufaransa, Morocco, Mali na Marekani.

Kwa hiyo, inashangaza kwamba sasa anaweka mazingira ya hatari ya makabiliano ya kijeshi na Ecowas kwa kupuuza uamuzi wake wa kurudisha mamlaka kwa Bw Bazoum.

Jenerali Tchiani pia ametumwa katika majukumu mbalimbali ya usimamizi nchini Niger yenyewe, ingawa si kweli katika kampeni dhidi ya makundi ya wanajihadi ambayo sasa yanaweka tishio kubwa kama hilo kwa nchi yake na nchi majirani za Mali, Burkina Faso na Benin katikati mwa eneo la Sahel.

Lakini mambo mawili yanajitokeza kutokana na kazi yake ndefu ya kijeshi.

Hadi kupandishwa cheo kuwa mlinzi wa rais mwaka wa 2011, hakuwa nje ya nchi wala nyumbani alikuwa amechukua majukumu katika ngazi ya juu ya amri ambayo inahitaji kufanya kazi kwa karibu na viongozi wa serikali ya kiraia na washirika wa kimataifa katika kuunda mkakati na kushughulikia matatizo ya kisiasa, kijamii na kidiplomasia.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 62 daima amekuwa "askari wa maaskari", aliyepewa kazi maalum za kijeshi badala ya picha pana ya ulinzi na usalama.

Hata baada ya kuwekwa kuwa msimamizi wa ulinzi wa rais na mtangulizi wa Bw Bazoum, Mahamadou Issoufou, alijiwekea maoni yake na, alizungumza machache.

Hakuwa sehemu ya mjadala mpana wa umma au wa kisiasa kuhusu njia bora ya kukabiliana na ghasia za wanajihadi na mivutano ya hapa na pale kati ya jumuiya ambayo imeleta changamoto kama hizo katika miaka ya hivi karibuni.

Wafuasi wengi wa serikali ya kijeshi wamechukua msimamo wa kuunga mkono Urusi dhidi ya Ufaransa na ambao ni nadra.

Anaonekana kuwa mtu wa faragha sana, kwa namna fulani hata asiyejulikana sana na marais waliojikabidhi kwa ulinzi wake.

Ilijulikana kuwa uhusiano wake na Bw Bazoum, mshirika wa muda mrefu wa Bw Issoufou, ulikuwa wa mbali zaidi na katika wiki za hivi majuzi kulikuwa na uvumi kwamba rais alikuwa akijiandaa kumlazimisha kustaafu.

Labda chuki za kibinafsi zilikuwa zimekusanyika, hazikuangaziwa lakini bado zikawa na nguvu.

Kuondolewa kwenye wadhifa wake, hata katika umri wa kawaida wa kustaafu, bila shaka kungekuwa pigo kubwa kwa mtu ambaye kwa zaidi ya miongo minne amepanda daraja hatua kwa hatua, baada ya kuanza kama mwanajeshi wa kawaida.

Jenerali Tchiani anatoka katika kabila kubwa la Wahausa, na anatoka eneo la Tillabéri, eneo la jadi la usajili wa wanajeshi.

Hata hivyo yeye hakuwa nguvu za kawaida za wa jeshi au uhusiano wa kisiasa. Alilazimika kufanya kazi kutoka chini hadi ngazi aliofikia .

Bw Bazoum pia ni mtu ambaye alitoka katika malezi ya kiasi na kisha akapanda ngazi ya elimu na taaluma hatua kwa hatua, katika katika chuo kikuu na kisha akwa mwalimu wa shule ya upili na mwanaharakati wa vyama vya wafanyakazi, kabla ya kuingia katika siasa mapema miaka ya 1990.

Lakini cha kushangaza, Jenerali Tchiani hakuwahi kuanzisha uhusiano mzuri wa kufanya kazi na Bw Bazoum - ilhali anaonekana kupatana kwa urahisi na Bw Issoufou.

Sasa bila shaka, baada ya miaka mingi nje ya macho ya umma, Jenerali Tchiani anajikuta kwenye mkondo wa mzozo katika usimamizi wa migogoro ya kisiasa na kidiplomasia.

Kufikia sasa ametegemea kile ambacho kimemtumikia vyema zaidi kwa miaka mingi jeshini: kujizuia, kusitasita kwa uangalifu kusema mawazo yake kikamilifu mbele ya wengine, na kukataa maelewano.

Lakini Jenerali Tchiani na junta wamezua chuki dhidi ya Ufaransa miongoni mwa Wanigeria wengi na atajaribu kubadilisha hali hiyo kuwa msingi mpana wa uungwaji mkono kwa mapambano na Ecowas.

Na huku majaribio haya yakikabiliana na Nigeria na wanachama wengine wa kambi ya Afrika Magharibi katika siku zijazo, na huku vikwazo vikizidi kuathiri na kusababisha gharama ya maisha kwa watu wa kawaida, mbinu hii mpya itachukua jukumu muhimu huku jenerali hiyo akicheza kamare ya kiwango cha juu ikilinganishwa na kazi yake awali.

Paul Melly ni mshauri mwenza katika Mpango wa Afrika katika Chatham House huko London.