Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Madrid wamgeukia Saliba wa Arsenal

Muda wa kusoma: Dakika 2

Real Madrid pia wanavutiwa na mlinzi wa Ufaransa William Saliba, 24, ambaye ni anacheza na Gabriel kama walinzi wa kati katika klabu ya Arsenal. (Mirror)

Arsenal wanajiandaa kumpa Gabriel, 27, mkataba mpya ili kuzuia kunyakuliwa kwa beki huyo wa kati wa Brazil kutoka Saudi Arabia. (Football Insider)

The Gunners, kwa upande wake, wameungana na Liverpool katika mbio za kumsajili mlinzi wa Uholanzi Jorrel Hato mwenye umri wa miaka 19 kutoka Ajax. (Team talk)

Atalanta wameweka bei ya pauni milioni 50 kwa mshambuliaji Ademola Lookman, 27, huku Manchester United na Newcastle United zikiwa na nia ya kumpata. (Tutomercato)

Atletico Madrid wana nia ya kumsajili mlinzi wa kati wa Tottenham mwenye umri wa miaka 26, Cristian Romero. (Sky Sports)

Everton wanatazamiwa kuanza mazungumzo na mlinzi wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 22, kuhusu mkataba mpya ili kuzuia ofa kutoka kwingine. (I Sport)

Manchester United inaweka nia ya kumnunua Branthwaite tu msimu wa joto ikiwa beki wa kati wa Uingereza Harry Maguire, 32, ataondoka Old Trafford. (Yahoo)

Aston Villa wameanza mazungumzo na kiungo wa kati wa Ufaransa Boubacar Kamara, 25, kuhusu kandarasi mpya. (Telegraph)

Crystal Palace wanaendelea na mazungumzo kuhusu mkataba mpya wa meneja Oliver Glasner, huku kukiwa na nia ya kutaka kumnunua raia huyo wa Austria kutoka RB Leipzig. (Football Insider)