Tetesi za soka Ulaya: Vinicius agoma kusaini mkataba mpya Madrid

Vinicius Junior

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Mshambuliaji wa Brazil Vinicius Junior, mwenye umri wa miaka 25, ameiarifu Real Madrid kuwa hana nia ya kuongeza mkataba wake unaoisha majira ya joto 2027, kutokana na uhusiano uliodorora kati yake na kocha Xabi Alonso. (Athletic)

Liverpool, Manchester United na baadhi ya klabu nyingine za Ligi kuu England vinafuatilia kwa karibu hali ya Vinicius. (Mirror)

Liverpool tayari imefanya mazungumzo ya kina kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Bournemouth na Ghana, Antoine Semenyo, 25, na wanajua kuhusu kifungu chake cha kuuzwa kwa pauni milioni 65. (Florian Plettenberg)

Manchester United na Chelsea zote zimemfuatilia kiungo wa RB Leipzig na Ujerumani Assan Ouedraogo, 19. (Sky Sports Germany)

Antoine Semenyo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Antoine Semenyo

Marseille wanataka kufanya mazungumzo na Brighton kuhusu kumsajili kiungo wa Denmark Matt O'Riley, 25, kwa mkataba wa kudumu Januari. (Sky Sports)

Klabu kubwa barani Ulaya ikiwemo AC Milan zinapanga uhamisho mkubwa wa mshambuliaji wa Crystal Palace na Ufaransa, Jean-Philippe Mateta, 28. (Teamtalk)

Klabu za ligi kuu England zinatarajiwa kujipanga kumsajili kiungo wa Atletico Madrid na England Conor Gallagher mwezi Januari, endapo klabu hiyo ya Hispania itakubali kumuuza au kumtoa kwa mkopo. (Sky Sports)

Paris Saint-Germain wameungana na Real Madrid katika mbio za kumsajili beki wa Bayern Munich na Ufaransa Dayot Upamecano, 27, ambaye huenda akawa mchezaji huru mwishoni mwa msimu. (Sky Sports Germany)

s

Chanzo cha picha, getty

Kiungo wa Wolves na Brazil Joao Gomes, 24, amevutiwa na nia ya Manchester United na angependa kuhamia huko Januari. (Teamtalk)

Kiungo wa Ureno Bernardo Silva, 31, huenda akaondoka Manchester City pale mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu. (Fabrizio Romano)

Chelsea na Arsenal watapambana kumsajili mshambuliaji wa Marseille, Mfaransa Robinio Vaz, 18, anayekadiriwa kati ya euro milioni 20 hadi 30 (pauni milioni 17.6 hadi 25.5). (Caught Offside)

Atletico Madrid wanamfikiria mshambuliaji wa Marseille Mason Greenwood, 24, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa karibu pauni milioni 70. (Fichajes)