'Nilipanga mazishi yangu - sasa nipo jukwaani kama mchekeshaji'

    • Author, Jonathan Geddes
    • Nafasi, BBC Glasgow and West reporter
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Miaka mitano iliyopita, Yvonne Hughes alikuwa akipanga mazishi yake.

Wazo kwamba miaka michache baadaye angekuwa bado hai, na zaidi ya hayo, akisimama jukwaani akiigiza vichekesho kwenye tamasha la Edinburgh Fringe, lingehesabika kama mzaha.

Yvonne, mzaliwa wa Glasgow, aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa uvimbe kwenye kizazi akiwa bado mchanga.

Hali ambayo husababisha matatizo ya kupumua na kumeng'enya chakula katika maisha yote.

Akizungumza na kipindi cha asubuhi cha BBC Radio Scotland, alisema:

"Kufikia mwaka 2020, ilikuwa muujiza kuwa hai na kuwa katika miaka ya arobaini."

Hii ni kutokana na watu wengi kufariki dunia wanapokuwa na uvimbe huo kwenye kizazi.

Lakini dawa mpya iitwayo Kaftrio imebadilisha maisha yake kabisa na kumpa matumaini mapya kwa maisha ya baadaye.

Kufikia umri alio nao sasa haijakuwa rahisi imekuwa na panda shuka zake.

"Wakati nikiwa mdogo, marafiki niliokuwa nao hospitali ya watoto ya Yorkhill walikuwa wakifariki,dunia" alieleza kwa Connie McLaughlin wa BBC.

Aliendelea kuishi, lakini ugonjwa ulizidi kuathiri maisha yake kadiri alivyozeeka.

"Nilipenda kucheza, kuogelea na kushiriki kikundi cha Brownies, lakini mara kwa mara nilikuwa ninalazwa hospitalini."

Kwa kipindi fulani, tafiti za kitabibu ziliongeza changamoto kwake baada ya kubainika kuwa wagonjwa wa uvimbe kwenye kizazi hawapaswi kuchangamana.

"Mapafu yetu huzalisha bakteria hatari kwa wagonjwa wengine wa CF," alisema.

"Ni sawa na jinsi virusi vya Covid vinavyosambaa. Sayansi ilipogundua hilo, tukaambiwa tusiwe karibu na wenzetu sisi ndio kundi pekee la wagonjwa tunaokatazwa kuonana."

Hatia ya kupona

Yvonne anakumbuka akiwa na miaka 20, alihudhuria mazishi ya rafiki yake wa utotoni aliyefariki dunia kwa sababu ya ugonjwa huo.

"Nilitambua kuwa huu ni ugonjwa wa kuua, na nililia kwa siku kadhaa. Naamini nina hatia ya kuwa hai," alisema.

Wakati akiwa mtoto, matarajio ya maisha kwa wagonjwa wa CF yalikuwa ni hadi miaka 31 tu. Kufika miaka ya 40 tayari kulikuwa ni kuvuka mipaka ya matumaini ya kitabibu.

Lakini licha ya maendeleo ya kisayansi, afya yake ilikuwa imezorota vibaya uwezo wa mapafu yake ulikuwa umeshuka hadi asilimia 30 tu.

"Tulijua kuna dawa mpya zenye mafanikio makubwa, lakini nilidhani hali yangu ilikuwa mbaya mno kufuzu. Niliandaa mazishi yangu na familia," alieleza.

"Ilikuwa muujiza kufikia katikati ya miaka ya 40."

Lakini kufikia mwaka wa 2020 dawa ya kaftrio ilikuwa imeidhinishwa kutumika nchini Scotland.

Dawa ya kawaida ambayo inafanya kazi kutibu chanzo cha ugonjwa huo kwa kupuuza makosa ya kijeni yanayosababisha ugonjwa huo.

Yvonne anasisitiza kuwa kaftrio sio dawa ya miujiza na haifanyi kazi kwa kila mtu, lakini kwake, athari ilikuwa ya papo hapo.

Viwango vya nguvu

"Baada ya saa chache tu, nilianza kukohoa kamasi. Kadiri siku zilivyopita, nilihisi nguvu zikirudi."

Dawa hiyo huhitaji kumezwa pamoja na chakula chenye mafuta.

"Baba yangu alitumia kiasi kikubwa cha pesa kununua vyakula vya mafuta. Nakumbuka nilipomfungulia mlango mtu aliyekuwa analeta dawa, nikamwambia: 'Unakuja kuniokoa maisha.' - na kweli ikafanya hivyo."

Akiwa amejaa nguvu mpya, Yvonne alijiunga na kozi ya ucheshi kupitia kituo cha elimu ya watu wazima.

Hatimaye, alianzisha maonyesho yake, na katika tamasha la mwaka huu, anaonyesha kazi iitwayo Absolutely Riddled, inayojumuisha mapambano yake ya kiafya ndani ya vichekesho.

"Inaweza isisikike kama kitu cha kuchekesha, lakini ni onesho lenye joto la moyo na lenye kuhimiza maisha."

Maonyesho hayo yanaendelea hadi tarehe 15 Agosti huko Scotland.

"Kabla ya Kaftrio, nilikuwa naingia hospitali kila wiki sita hadi nane. Sasa nina nguvu nyingi kiasi kwamba wakati mwingine husahau kama niliwahi kuugua."

Ni nini uvimbe kwenye kizazi ama Fibroids?

Ni ugonjwa wa kurithi unaoathiri maisha zaidi Uingereza na hata Afrika.

Huzuia seli kusafirisha chumvi na maji ipasavyo, na kusababisha kamasi kuganda.

Fibroids ni vimbe wa misuli laini wenye mizizi ya kuiunganisha, unaoota na kukua kwenye nyumba ya uzazi ya mwanamke.

Miaka ya hivi karibuni kumekuwapo na wanawake wengi wanaokumbwa na tatizo hili na miongoni mwao huishia kufanyiwa upasuaji kwa ili kuuondoa uvimbe huo.

Huathiri viungo mbalimbali, hasa mapafu na mfumo wa kumeng'enya chakula.

Dalili huanza utotoni, na viungo huathirika kadiri muda unavyoenda.

Ingawa ni ugonjwa hatari, wastani wa maisha umeongezeka tangu miaka ya 1970.

Fibroids husababishwa na nini?

Chanzo hasa cha kuota kwa fibroids katika viungo vya uzazi vya mwanamke bado hazieleweki vizuri ingawa inaamika kwamba kila uvimbe wa fibroid unatokana na seli ya musuli wa uterus ambayo imeamua kuwa na tabia ya tofauti na nyingine na ikaanza kukua kwa haraka ikichangiwa na uwepo wa homoni ya estrogen.

Wanawake wanaokaribia kufikia ukomo wa kupata siku zao za mwezi wanaonekana kuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata fibroids kwa sababu ya kuwa wameishi na homoni ya estrogen kwa muda mrefu zaidi.

Wanawake wenye asili ya mchanganyiko wa wamarekani na waafrika (wamarekani weusi) nao wanaonekana kupatwa na fibroids zaidi ya wanawake wengine ingawa sababu bado haijajulikana.

Utafiti umeonyesha pia kuwa idadi ya wanawake wanaopatwa na fibroids katika kundi la wanawake ambao wamezaa watoto angalau wawili wakiwa hai huwa ni nusu ukilinganisha na wale ambao hawajazaa hata mara moja.

Hapa haieleweki kama kuzaa kulizuia wanawake hawa wasipate fibroids au fibroids ndizo zilizozuia wanawake wa kundi la pili wasizae. Utafiti kuhusu hilli bado unaendelea.

Dalili Za Fibroids

  • Kutokwa na damu kwa wingi wakati wa hedhi
  • Kutokwa na damu kusiko kwa kawaida katikati ya siku za mwezi
  • Mauvimu ya nyonga (uvimbe kugandamiza kwenye viungo vya nyonga)
  • Kupata haja ndogo mara kwa mara
  • Maumivu ya mgongo
  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Upungufu wa damu kwa sababu ya kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku
  • Maumivu ya kichwa
  • Maumivu kwenye miguu
  • Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo (Fibroids kubwa)
  • Uzazi wa shida
  • Mimba za shida
  • Kutopata mimba
  • Kutoka kwa mimba mara kwa mara

Chanzo: NHS

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid