Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa DRC: Ushawishi wa Qatar katika mzozo huu utafanikiwa?
Taifa la Qatar limekuwa msitari wa mbele katika juhudi za kutafuta amani kwenye baadhi ya mizozo inayoathiri maeneo kadhaa duniani. Na baada ya kikao cha Jumanne, ambapo Kiongozi wa taifa hilo aliwakutanisha Marais wa Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Qatar imeonekana kuorodheshwa katika kundi la mataifa kama vile Marekani, Milki za Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na mengine mengi ambayo yanajaribu kusitisha vita katika bara Ulaya, Mashariki ya kati na hata hapa Afrika. Sasa je, ni kwa nini nchi hiyo imepata umaarufu mkubwa katika juhudi za kusaka amani duniani?.
Leila Mohammed anaelezea zaidi.