Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
DRC 'kuharakisha' kuondoka kwa wanajeshi wa UN nchini humo
Serikali ya DR Congo imeambia BBC kwamba inatumai itaharakisha kuwaondoa wanajeshi walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa MONUSCO nchini humo.
Kupitia makubaliano mapya , wanajeshi hao wa UN walitarajiwa kuondoka mwisho wa 2024.
Tangazo hilo linajiri kufuatia maandamano ya ghasia dhidi ya vikosi hivyo vya UN katika eneo la mashariki mwa taifa hilo ambayo yalisababisha mauaji ya makumi ya raia Pamoja na wanajeshi wanne wa UN.
Siku ya Jumatatu , Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres aliomba msamaha baada ya wanajeshi wawili wa Umoja huo kuwafyatulia risasi waandamanaji na kuwauwa watu watatu huku wengine 15 wakijeruhiwa siku ya Jumapili katika mji wa mpakani wa Kasindi .
Ijapokuwa waliohusika wamesimamishwa kazi kwa muda tukio hilo limewakasirisha raia wa DRC.
Kulingana na mwandishi wa habari wa BBC Joice Etutu aliyeko mjini Goma, Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa , MONUSCO umekuwa ukifanya operehsnei zake mashariki mwa DRC kwa zaidi ya muongo mmoja. Lengo lake , ni kuleta amani na udhabiti katika eneo hilo ambalo limekumbwa na ukosefu wa usalama kwa zaidi ya miaka 20.
Hatahivyo raia wa DRC wamesema kwamba uwepo wa jeshi hilo la Umoja wa Mataifa haujaleta amani na wamekuwa wakiliomba jeshi hilo kuondoka haraka iwezekanavyo.
Baada ya zaidi ya maandamano ya wiki moja, rai swa DRC Felix Tshisekedi amesema kwamba serikali yake itaangazia upya hatua ya kuondoka kwa wanajeshi hao.
Kauli ya Msemaji wa Serikali
Msemaji wa serikali Patrick Muyaya, amesema kwamba hatuwezi kuwa na viksi vya Umoja wa Mataifa kila mwaka kwasababu tatizo la ukosefu la usalama limeendelea kuwepo.
Ni afadhali pengine kuwa na jeshi letu, maafisa wa polisi na changamoto zetu na kuwakabili wale wanaoleta shida na vita katika eneo la mashariki mwa DRC.
Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa MONUSCO ameambia BBC kwamba ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa utatathminiwa.
Akiongeza kuwa mpango wa mpito wa taratibu na unaowajibika utawekwa mashariki mwa DRC.