Mkaazi wa Gaza asema Yahya Sinwar aliuawa nyumbani kwake

Chanzo cha picha, Getty Images
Mpalestina aliyekimbia makazi yake kutoka Gaza ameambia BBC kwamba nyumba ambayo kiongozi wa zamani wa Hamas aliuawa ilikuwa ni nyumba yake kwa miaka 15 kabla ya kulazimika kutoroka mnamo mwezi Mei.
Ashraf Abo Taha alisema "ameshtushwa" alipotambua jengo lililoharibiwa kwa kiasi cha haja katika picha zilizochukuliwa na ndege zisizo na rubani za Israel kama nyumba yake kwenye mtaa wa Ibn Sena huko Rafah, kusini mwa Gaza.
Yahya Sinwar, mhusika mkuu wa shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israel, aliuawa na wanajeshi wa Israel siku ya Jumatano.
Jeshi la Israel lilitoa picha za ndege zisizo na rubani ambazo zilisema zilionyesha Sinwar katika nyumba iliyoharibiwa kidogo kabla ya kuuawa.
Bw Abo Taha aliambia Gaza Lifeline ya BBC Arabic kwamba aliondoka nyumbani kwake Rafah kuelekea Khan Younis tarehe 6 Mei, wakati Israel ilipoamuru watu kuhama na kuanza operesheni dhidi ya wapiganaji wa Hamas, na hawajapata habari zozote kuhusu nyumba yake hadi sasa.
Bw Abo Taha alisema binti yake alimwonyesha kwa mara ya kwanza picha zinazodaiwa kunasa dakika za mwisho za Sinwar kwenye mitandao ya kijamii, akisema zilionyesha nyumba yao iliyoko Rafah.
Hapo awali hakuamini, alisema, hadi kaka yake alipothibitisha kuwa kweli nyumba hiyo ilikuwa yake.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Bw Abo Taha aliambia Gaza Lifeline ya BBC Arabic kwamba aliondoka nyumbani kwake Rafah kuelekea Khan Younis tarehe 6 Mei, wakati Israel ilipoamuru watu kuhama na kuanza operesheni dhidi ya wapiganaji wa Hamas, na hawajapata habari zozote kuhusu nyumba yake hadi sasa.
Bw Abo Taha alisema binti yake alimwonyesha kwa mara ya kwanza picha zinazodaiwa kunasa dakika za mwisho za Sinwar kwenye mitandao ya kijamii, akisema zilionyesha nyumba yao iliyoko Rafah.
Hapo awali hakuamini, alisema, hadi kaka yake alipothibitisha kuwa kweli nyumba hiyo ilikuwa yake.
"Nilisema 'ndio, hii ni nyumba yangu' na nikaona picha, nilishtuka", Bw Abo Taha alisema.
Alisema hakuwa na habari kwa nini Sinwar alikuwa pale au jinsi alivyofika huko.
"Sijawahi ama mimi au kaka zangu au wanangu kuhusika kwa vyovyote na hili," alisema.
BBC imethibitisha kuwa picha na video zilizotolewa na Bw Abo Taha za picha ya nyumba yake zinafanana na nyumba ambayo Sinwar aliuawa.
BBC Verify ililinganisha picha za kuta za madirisha ya nyumba, mapambo ya nje kwenye milango, rafu na makochi kutoka kwenye video.
BBC haiwezi kuthibitisha kwa uhuru kwamba Bw Abo Taha ndiye anamiliki nyumba hiyo.

Chanzo cha picha, Ashraf Abo Taha

Chanzo cha picha, IDF
Picha za mauaji ya Sinwar zilichambuliwa na BBC, na nyumba ambayo alionekana mara ya mwisho ilikuwa mojawapo ya majengo machache yaliyoharibiwa kwa kiasi katika kitongoji kilichokumbwa na uharibifu mkubwa.
Shambulio la Israel dhidi ya Rafah mwezi Mei lilikabiliwa na ukosoaji mkubwa wa kimataifa, na kusababisha kuhama kwa Wapalestina zaidi ya milioni moja, kulingana na UN.
Wengi walikuwa wamelazimika kuhama kwa mara ya pili au ya tatu, kwani walikuwa wamejihifadhi ndani na karibu na Rafah baada ya kufukuzwa kutoka sehemu zingine za Gaza.
Bw Abo Taha alisema alijenga nyumba yake huko Rafah mwenyewe kwa usaidizi wa ndugu zake. Ilikuwa imegharimu kiasi cha shekeli 200,000 (£41,400) na ilikuwa katika hali nzuri alipoondoka, alisema.
Alielezea sofa za nyumbani kwake na bakuli za rangi ya machungwa, akikumbuka mara ya mwisho alipoziona wakati akitoroka nyumbani kwake.
"Hizi ni kumbukumbu kwa sababu baadhi ya hizi zililetwa na mama yangu na ni za thamani sana kwangu," alisema. “Kilichotokea kimenisikitisha sana, nyumba niliyoijenga na malipo yangu yote yamepotea,” alisema. "Ni Mungu pekee ndiye anayeweza kutufidia."











