Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ni nini hufanyika ulimwenguni kote wakati wa mwezi mpevu?
Mwezi mpevu hutokea karibu kila siku 29, wakati jua linapochomozea kwenye mwezi moja kwa moja nyuma ya dunia na kuangaza kwa duara lote.
Mwezi mpevu, ambao ulikamilisha duara yake Ijumaa, Novemba 15, ni wa mwisho katika mfululizo wa miezi hiyo mwaka huu na kuonesha ukubwa wake kwa asilimia 14 na asilimia 30 za mwangaza Zaidi kuliko mwezi kamili wa kawaida.
Tukio linalofahamika kama supermoon hutokea mara tatu au nne tu kwa mwaka, na mwezi daima huonekana mfululizo.
Mwezi mpevu umekuwa na jukumu muhimu katika kuunda tamaduni na mila za jamii kote ulimwenguni.
Katika ripoti hii, tunaangazia baadhi ya simulizi, matukio na maana zinazohusiana na jambo hili la anga.
Mwezi mpevu ulikuwa na maana gani kwa watu wa kale?
Mwenendo wa Mwezi - ikiwemo awamu zake za kawaida kutoka kwenye mng’ao hadi kupungua mara moja kwa mwezi - hutumika tangu nyakati za zamani ili kutunza kumbukumbu ya wakati.
Kwa mfano, mfupa wa Ishango - uliopatikana mwaka wa 1957 katika eneo ambalo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Mfupa huo, ambao inaelekea ulitolewa kwenye mguu wa nyani na unaodhaniwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 20,000, unaaminika kutoka katika kalenda ya kizamani.
Mfupa huo, uliogunduliwa na mtaalamu wa elimu ya miamba kutoka Ubelgiji, una maandishi ya kipekee—baadhi yakiwa na umbile la duara au sehemu za duara.
Mtaalamu wa mambo ya kale wa Chuo Kikuu cha Harvard Alexander Marshak amependekeza kwamba maandishi haya yanaweza kuwakilisha awamu tofauti za mwezi,akidokeza kwamba huenda mfupa ulitumiwa kama kalenda ya miezi sita.
Mwezi wa Mavuno ni jina linalopewa mwezi mpevu ambao hutokea karibu na wakati ambapo jua huvuka ikweta na huwa msimu wa vuli (mwishoni mwa Septemba au Oktoba mapema).
Kwa wakati huu wa mwaka mwezi huchomoza muda mfupi baada ya jua kutua,Ikimaanisha kwamba wakulima wanaokimbilia kuvuna mazao yao wanaweza kuendelea kufanya kazi hadi jioni sana kukiwa na mwanga wa mwezi. Bila shaka, siku hizi wengi wao hutumia taa za umeme.
Sherehe gani hufanyika wakati wa mwezi mpevu?
Tamasha la Mid-Autumn, Chongkui Ji (pia huitwa Tamasha la Mwezi), hufanyika siku ya Mwezi wa Mavuno na ni mapumziko ya umma.
Tamasha hilo lilianza miaka 3,000 iliyopita na lilifanyika katika msimu wa mavuno.
Vile vile, huko Korea, Tamasha la Chuseok ni tukio la siku tatu ambalo linaambatana na mwezi wa mavuno. Wakati wa tamasha, familia hukusanyika ili kusherehekea mavuno na kutoa shukrani kwa mababu zao.
Katika utamaduni wa Kihindu, siku za mwezi mpevu, zinazoitwa Purnima, zinaashiria kufunga na maombi.
Sikukuu ya Kartik Purnima inafanyika mnamo Novemba - mwezi mtakatifu zaidi katika kalenda ya Kihindu - na alama ya ushindi wa mungu Shiva dhidi ya Pepo Tripurasura, aina mojawapo ya mizimu.
Vishnu kwa namna ya Matsya.Hujumuisha kuoga kwenye mito na safu za taa zilizotengenezwa kwa udongo.
Wabudha wanaamini kwamba Buddha alizaliwa chini ya mwezi mpevu miaka 2,500 iliyopita.
Pia wanaamini kwamba alizaliwa nuruni na kufa chini ya mwezi mpevu.
Matukio haya yanaadhimishwa kwenye tamasha la Buddha Purnima, ambalo kawaida hufanyika siku ya mwezi mpevu kila mwezi wa Aprili au Mei.
Nchini Sri lanka mwezi mpevu wa kila mwezi huwa likizo ya umma inayoitwa Poya, wakati ambapo uuzaji wa pombe na nyama ni marufuku.
Huko Bali, Purnama ni sherehe ya mwezi mpevu, wakati ikiaaminika kwamba miungu hushuka duniani na kutoa baraka zao.
Ni wakati wa maombi, sadaka kwa Mungu, na kupanda miti ya matunda katika bustani.
Waislamu wanahimizwa kufunga kwa siku tatu karibu na wakati wa mwezi mpevu. Siku hizi zinajulikana kama siku tatu nyeupe. Inasemekana kuwa Mtume Muhammad alifunga siku hizi kama njia ya kumshukuru Mungu kwa kuangazia nuru usiku wa giza.
Katika Ukristo, Pasaka husherehekewa Jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu wa kwanza kufuatia usawa wa kienyeji.
Katika Ukristo pasaka husherehekewa jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu kufuatia wakati jua litakuwa linamulika sawia katika mstari wa ikweta.
Nchini Mexico na mataifa mengine ya Amerika kusini,kumekuwa na mwamko wa ngoma asili ya mataifa hayo ifahamika kama ‘’moon dance’’ambapo wanawake wanajumuika chini ya mwezi mpevu kucheza na kufanya ibada kwenye tamasha hilo la siku tatu.
Je kuna imani gani potofu kuhusu mwezi mpevu?
Tangu nyakati za zamani huko Ulaya , inaaminika kuwa mwezi mpevu husababisha watu wengine kupata wazimu. Neno "madness" linatokana na neno "luna", neno la Kilatini kumaanisha mwezi.
Wazo la kwamba mwezi mpevu husababisha tabia isiyoweza kudhibitiwa limesababisha simulizi ya ‘’werewolves’’—wanadamu ambao bila hiari yao hubadilika na kuwa mbwa-mwitu na kutisha jamii zao nyakati za usiku kwa mwezi mzima.
Katika karne ya 4 KK, mwanahistoria Mgiriki Herodotus aliandika juu ya kabila kutoka Scythia (ambayo sasa ni Urusi) inayoitwa Noriae, akidai kwamba waligeuka kuwa mbwa-mwitu kwa siku kadhaa kila mwaka.
Huko Ulaya haswa, kati ya karne ya kumi na tano na kumi na saba, watu kadhaa walishtakiwa kwa mashtaka ya kubadilika kugeuka mbwa mwitu.
moja ya simulizi maarufu katika muktadha huu ni ile ya mwenye shamba aitwaye Peter Staub wa huko Ujerumani.
Mnamo 1589, wawindaji nchini humo walidai kuwa walimwona akibadilika kutoka mbwa mwitu hadi mwanadamu.
Baada ya kuteswa, Petro alikiri kuwa na mkanda wa kichawi ambao aliutumia kujigeuza kuwa mbwa mwitu, ukimuwezesha kuwinda na kula watu.
Jinsi mwezi mpevu unavyoathiri Maisha yetu
Watu wengine wanaamini kwamba mwezi mpevu husababisha kukosa usingizi.
Uchunguzi unaonyesha kwamba wakati wa mwezi mpevu au unapokaribia kufika , watu huchukua muda mrefu kupata usingizi, hutumia muda kidogo katika usingizi mzito, kulala kidogo, na kuwa na viwango vya chini vya melatonin - homoni inayokusaidia kulala.
Kwa mujibu wa wataalamu waliripoti kuwa ubora wa usingizi ulipungua hata walipolala katika vyumba vilivyofungwa, vilivyo na giza ambavyo vilizuia mwanga wa mwezi mpevu.
Watunza bustani wengi hupanda mbegu wakati wa mwezi mpevu (kama Wabalinese wanavyofanya wakati wa mwezi mpevu (purnama)) kwa imani kwamba hii inaimarisha udongo.
Mwezi uwapo mpevu nguvu zake za uvutano huegemea upande mmoja wa Dunia huku nguvu ya uvutano ya jua ikivuta upande mwingine. Mbali na kusababisha mawimbi mengi, inadhaniwa kuwa pia kusababisha hali ya unyevu zaidi kwenye uso wa Dunia.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa huko Bradford, Uingereza, mnamo 2000, mwezi mpevu husababisha wanyama kuuma zaidi.
Utafiti huo uligundua kuwa kati ya 1997 na 1999, idadi ya watu walioumwa na wanyama iliongezeka sana siku ambazo mwezi ulikuwa mpevu.
Ni masikitiko kwamba kisa cha kuumwa na binadamu mbwa mwitu kilichorekodiwa.
Imetafsiriwa na Martha Saranga na kuhaririwa na Yusuf Jumah