Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi utumbo wa samaki sangara utakavyoipaisha Tanzania kimataifa
Mabondo ya samaki aina ya Sangara ambayo miaka ya nyuma yalionekana kama bidhaa isiyokuwa na faidi kubwa katika eneo la Afrika Mashariki, kwa sasa imeanza kushika kasi baada ya serikali ya Tanzania na China kusaini mkataba maalum wa kuuziana bidhaa hiyo.
Kwa mujibu wa benki ya maendeleo Afrika, Tanzania, Kenya na Uganda kwa pamoja hupata takriban dola milioni 100 kwa mwaka kutokana na uuzaji wa mabondo nje ya nchi zao ambayo kwa sasa imekuwa bidhaa maarufu.
Mwandishi wa BBC David Nkya aliutembelea mkoa wa Mwanza uliopo Kaskazini mwa Tanzania, na hii ni taarifa yake