Chatu wa futi 18 aliyetoroka awatisha wakazi Hampshire,Uingereza

Wakaazi wameelezea mshtuko wao baada ya chatu mwenye urefu wa futi 18ft (5.5m) kuonekana akijaribu kuingia ndani ya nyumba.

Chatu huyo wa Kiburma, ambaye alikuwa ametoroka kutoka eneo la karibu, alionekana akijaribu kupitia dirisha la ghorofani kutoka kwenye paa la nyumba huko Chandler's Ford, Hampshire,Uingereza

Nyoka huyo alisababisha hofu alipoonekana mapema Jumanne.

Hatimaye ilichukuliwa na jirani ambaye alimtambua na kumrudisha kwa mmiliki wake.

Jenny Warwick alisema alichungulia nje ya dirisha saa 05:15 BST na kumwona nyoka huyo mkubwa wa manjano kwenye paa la jirani yake lakini hakutambua ni nini hadi alipomwona akijaribu kuingia kwenye dirisha la ghorofani.

Alisema: "Niliwaona wakijaribu kumchomoa na akaanguka kwenye gari lao. Alikuwa Mkubwa.

"Watu waliokuwa wakipita walikuwa wakitazama na hawakuamini macho yao."

Linda Elmer, ambaye alimtambua nyoka huyo, alisema aliamshwa saa 07:00 na majirani waliokuwa na wasiwasi wakigonga mlango wake, wakijaribu kumtafuta mwenye nyumba.

Alisema: "Kila mtu alikuwa na hofu.

"Nilimnyanyua - hakuna aliyetaka kusaidia. Ilikuwa vigumu sana kwa sababu yeye ni nyoka mkubwa na nilifanikiwa kukimbia barabarani huku chatu huyu wa futi 18 akinizunguka na kugonga mlango wa mwenye nyumba.

"Nadhani ilikuwa mshtuko kwetu sote.

"Yeye ni mrembo na ni wa kutoka Burma ni watulivu sana. Wao si nyoka wakali hata hivyo na nilikuwa na mimi mwenyewe hivyo nilikuwa na raha kumuokota."

Awali shirika la kuwalinda wanyama RSPCA liliwataka wamiliki kuwazuia nyoka wakati wa joto kwani hali hiyo huwafanya kuwa na uwezo wa kutoroka