Imani kuhusu kahawa na divai nyekundu ambazo unafikiri ni za kweli, kumbe sivyo

Mara nyingi tunajawa na habari kuhusu vyakula na vitu ambavyo vinapaswa kuwa na athari za kingakwa kiafya na umuhimu kilishe.

Lakini ushauri wa lishe na maoni tunayosikia juu ya vyakula vingi hubadilika kila wakati.

Vyakula viwili vilivyochunguzwa zaidi kwa athari zake kwa afya ya binadamu ni kahawa na divai nyekundu.

Na tunapewa maoni yanayopingana juu yao.

Wakati mwingine vinasemekana kuwa na madhara kwenye miili yetu na wakati mwingine vinasemekana kuwa na manufaa.

Tafiti za hivi punde za kisayansi zinasema nini kuvihusu?

Tulizungumza na wanasayansi wawili ambao wamekuwa wakitafiti athari za kahawa na divai nyekundu kwa afya ya binadamu.

Uhusiano wa kahawa na vifo

Kwamba kikombe cha kahawa cha asubuhi kama sehemu ya utaratibu wetu wa kila siku ni kusongeza mbele siku za maisha yetu.

Utafiti uliochapishwa Julai katika jarida la The Annals of Internal Medicine unasema hivyo.

Takriban watu laki mbili wamefanyiwa utafiti kwa miaka 10.

Watafiti waligundua kuwa watu ambao walikunywa kati ya kikombe kimoja na nusu hadi vitatu na nusu vya kahawa kwa siku, hata kwa kuongeza kijiko cha sukari, walikuwa na uwezekano mdogo wa kufa katika kipindi cha muongo mmoja wa utafiti wao kuliko wale ambao hawakunywa kahawa.

Uwezekano huo ulionekana kuwa chini kama asilimia 30.

Wale waliokunywa kahawa isiyo na sukari walikuwa na hatari ya chini ya kifo kwa asilimia 16 hadi 21.

Na wale ambao walikuwa na hatari ndogo zaidi ya kifo wakati wa utafiti walikuwa wale ambao walikunywa hadi vikombe vitatu vya kahawa kwa siku.

Pia unaweza kusoma:

Huu sio utafiti wa kwanza kuripoti kupunguza hatari ya kifo kwa wanywaji kahawa.

Mnamo mwaka wa 2018, utafiti mwingine ambao ulikusanya data kwa zaidi ya watu 500,000 kwa miaka 10 pia ulipata kupunguzwa kwa asilimia 16 kwa hatari ya kifo cha mapema.

Na katika tafiti kadhaa, upunguzaji huu pia ulionekana kwa wanywaji kahawa ya decaf, ambayo inaweza pia kumaanisha kuwa baadhi ya maelfu ya michanganyiko katika kahawa ni ya manufaa.

Hata hivyo, watu wengi wanaendelea kufikiri kwamba kahawa ni hatari na kwamba tunapaswa kupunguza matumizi yetu ya kinywaji hiki.

Je, tunakosea kuhusu kahawa?

Dk Esther López García, profesa wa dawa za kinga na afya ya umma katika Chuo Kikuu cha Autonomous Madrid, aliiambia BBC: Kwa muda, mtazamo wetu kuhusu madhara ya kiafya ya kahawa umebadilika sana.

Utafiti mkubwa ulianza mwaka wa 2003 ambao uliangalia unywaji wa kahawa mara kwa mara kwa miaka mingi na kuangalia jinsi unavyoathiri hatari ya kifo cha mapema, ugonjwa wa moyo au kisukari cha aina ya 2, Lopez anasema.

Baada ya kurekebisha vizuri mambo yanayoathiri afya, kama vile matumizi ya tumbaku na pombe, hakuna madhara ya matumizi ya kahawa ya kawaida yalizingatiwa.

Imepatikana hata kusaidia kuzuia kisukari cha aina ya 2 na kiharusi.

‘’Pia imeonekana kuwa madhara ya kafeini hayaendelei kwa watumiaji wa kawaida, na huendeleza uvumilivu kwa kwa kinywaji hiki na athari za manufaa za vipengele vingine vya kahawa kwa afya zao,’’ Lopez anasema.

Tafiti nyingi kuhusu kahawa zimeonyesha ushahidi kuwa ina athari za kinga dhidi ya ugonjwa wa Parkinson.

Pia inasemekana kulinda dhidi ya kuzorota kwa utambuzi, magonjwa ya moyo na mishipa, saratani, kisukari cha aina ya 2 na aina fulani za kisukari kwa ujumla.

Lakini Profesa López Garcia anasisitiza kwamba ushahidi thabiti zaidi ni wa kisukari cha aina ya 2.

Kwa magonjwa mengine, bado haijulikani.

Inafikiriwa kuwa haina madhara kwa ugonjwa wa moyo na pia haina madhara kwa saratani ya matiti.

Na kafeini inafikiriwa kupunguza hatari ya magonjwa ya mfumo wa neva, lakini matokeo yake bado hayako wazi.

Kuna zaidi ya misombo elfu ya kemikali katika kahawa, na mingi yao inachunguzwa kwa kina.

Kwa mfano, ina kiasi kikubwa cha vitu vinavyozuia ongezeko la oksijeni ambayo utafiti mwingine unapendekeza inaweza kuzuia au kuchelewesha uharibifu wa seli.

Profesa Garcia anaeleza kwamba athari za manufaa za kahawa ni hasa kutokana na mojawapo ya vitu hivi vinavyozuia ongezeko la oksijeni, ni asidi ya klorojeni.

Kulingana na wao, vitu vinavyozuia ongezeko la oksijeni hii ina athari nyingi za manufaa kwenye kimetaboliki ya glucose.

Pia ina vitu vingine, kama vile magnesiamu, ambayo ni madini ambayo yana athari nyingi kwa afya.

Labda kahawa imekuwa na sifa mbaya hapo awali kwa sababu kafeini inaweza kusababisha wasiwasi au kukosa usingizi kwa watu wengine.

Ndiyo maana Prof. Garcia anasema kuwa kwa watu wenye afya njema, ulaji wa kila siku wa vikombe 3 hadi 5 vya kahawa huenda ukawa na manufaa.

Kahawa isiyo na sukari sasa inapendekezwa kama kinywaji cha afya katika miongozo mingi ya vyakula.

Lakini iliongeza kuwa watu wote walio na matatizo ya kiafya ambayo yanaweza kuwa mabaya zaidi kutokana na kahawa wanapaswa kutafuta ushauri wa kibinafsi kuhusu kutumia kinywaji hicho.

Mvinyo na 'Athari zake za Kinga'

Divai nyekundu mara nyingi huwasilishwa kama kitu chenye manufaa katika pombe.

Tafiti kadhaa katika miongo michache iliyopita zimetushawishi kuwa glasi ya mvinyo ya mara kwa mara ni nzuri kwa afya ya moyo na mishipa.

Kwa mfano, utafiti uliochapishwa mwaka wa 2019 katika jarida la Molecules unapendekeza kwamba aina mbalimbali za misombo ya polyphenol katika divai nyekundu inaweza kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo.

Lakini Januari mwaka huu, Shirikisho la Moyo Duniani (WHF) lilichapisha hakiki ya utafiti inayoonyesha kwamba pombe kwa hakika si nzuri kwa afya ya moyo na mishipa.

Ripoti ya WHF inasema kwamba ugonjwa wa moyo na mishipa (CVD) umeongezeka karibu mara mbili katika miongo ya hivi karibuni na pombe imekuwa na jukumu kubwa katika visa hivi vingi.

Kulingana na WHF, kwa zaidi ya miaka 30 uwongo umeenezwa kwamba pombe huongeza maisha hasa kwa kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo.

Lakini ripoti hiyo inasema kwamba unywaji pombe huongeza hatari ya CVD na magonjwa mengine.

Kwa hivyo divai nyekundu ni nzuri au mbaya?

Tuliuliza swali hili kwa Dk. Miguel Marcos Martín, mtafiti katika Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Biolojia ya Salamanca na profesa katika Chuo Kikuu cha Salamanca.

Ameshiriki katika tafiti kadhaa kuhusu madhara ya pombe kwa afya.

‘’Ni kweli kwamba kuna tafiti zinazohusisha unywaji wa pombe na manufaa ya kiafya yanayowezekana na matokeo yenye utata na yasiyoeleweka, lakini hatuwezi kusahau kwamba tafiti nyingine nyingi zinaonyesha wazi kuwa ni dutu yenye madhara mengi, hata katika kidogo tu’’.

Kulingana na yeye, Kwa sababu hizi zote, kiasi chochote cha pombe au vinywaji vingine vile haviwezi kupendekezwa kwa sababu za afya kwa wakati huu.

Dk Marcus Martin anathibitisha kwamba ujumbe kwamba mvinyo mwekundu una madhara ya kinga kwa moyo ni wazi hautokani na ushahidi wa kisayansi kwani hii haijathibitishwa kikamilifu.

Kwa upande mwingine, hata kama ni kweli kwamba divai ina athari ya kinga dhidi ya magonjwa fulani, hatuwezi kupuuza madhara ambayo inaweza kusababisha.

Vinywaji vya pombe husababisha utegemezi, na kusababisha ugonjwa wa ini na kongosho na kadhalika.