Landais: Kijiji ambacho kila mtu ana ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu

Landais Alzheimer, kijiji kilichopo kusini-magharibi mwa Ufaransa - wanakijiji wote wana tatizo la kupoteza kumbukumbu.

Mkulima wa zamani Francis anachukua gazeti lake - na ninapendekeza twende tukanywe kahawa katika mgahawa maarufu wa kijiji hicho.
Nilimuuliza Francis alijisikiaje daktari alipomwambia ana ugonjwa wa kusahau.
Alitikisa kichwa na baada ya ukimya akasema: "Nilijiskia vibaya. Lakini Siogopi. Nitaishi maisha yangu licha ya ugonjwa huu.''
Baba yake pia alikuwa na tatizo la kusahau.

Philippe na Viviane wananiambia kuwa wanaendelea kuishi kawaida kufuatia kugunduliwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu.
Nilipowauliza ikiwa wanayafurahia maisha hapa, mara moja aligeuza kichwa na tabasamu na kusema: "Ndio, tunayafurahia."
''Wakati unasonga tofauti hapa,'' anayeniongoza hapa kijijini anasema.
Hakuna saa zilizowekwa kwa ajili ya miadi.
Kijiji kwa Ajili ya Utafiti

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mauricette 89, ameketi chumbani kwake, Dominique ameketi karibu na mama yake huyo, anasema: "Nina amani, kwa sababu najua mama yuko katika amani na yuko salama."
Chumba cha Mauricette kimejazwa picha za familia, michoro na samani za familia, chumba kina dirisha kubwa.
Bila ya miadi watu huja na kuondoka wapendavyo hapa. Na Dominique anasema yeye na dada zake hawakutarajia mama yao angepata utunzaji ambao ni mzuri sana.
''Hapa ni kama niko nyumbani kwake tu - niko nyumbani kwa mama yangu," anasema Dominique.
Kila ghorofa moja hukaa watu wapatao nane, na jiko la jumuiya, sebule na vyumba vya kulia.
Wanakijiji hao huchangia pesa kukaa hapo - sawa na nyumba za kutunza wazee. Lakini pesa nyingi zinalipwa na serikali ya mkoa ya Ufaransa ambayo ililipa pauni milioni 17 kuanzisha kijiji hiki.
Kijiji hicho kilipofunguliwa 2020, kilikuwa ni kijiji cha pili cha aina hiyo - lakini ni cha kipekee kuwa sehemu ya mradi wa utafiti.
Kijiji hicho kimevutia watu wengi ulimwenguni, hasa wale wanaotafuta suluhu la tatizo la kupoteza kumbukumbu.

Patricia, 65 anasema kijiji cha Landais Alzheimer kimemrudishia maisha yake: "Nilikuwa nikiishi nyumbani - lakini nilikuwa nachoka," anasema.
"Nilikuwa na mwanamke wa kunipikia. Sikuwa nikijisikia vizuri. Nilitaka kuwa mahali ambapo ningeweza kusaidia pia.''
"Katika nyumba nyingine za utunzaji, ni kama hapa - lakini hawafanyi chochote. Hapa ni maisha halisi. Ninaposema halisi, ninamaanisha halisi."
Wataalamu wanasemaje?

Mara nyingi, shida ya akili inaweza kufanya watu watengwe. Lakini hapa, inaonekana kuna hisia za umoja, na watu wanapendana kwa dhati na wako pamoja katika shughuli zote.
Na watafiti wanasema maisha hayo ya kijamii yanaweza kuwa sehemu ya ufunguo wa kuishi maisha ya furaha, na yenye afya zaidi - wakiwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu.
Kuna takribani wanakijiji 120 na idadi sawa ya wataalamu wa afya na watu wa kujitolea.
Bila shaka ni ugonjwa usiotibika. Lakini kila mwanakijiji, anapewa msaada anaouhitaji.
Baadhi ya wahusika waliomba majina yao ya ukoo yahifadhiwe.
Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Dinah Gahamanyi












