Alois Alzheimer: Daktari aliyegundua ugonjwa wa kusahau

Chanzo cha picha, Getty Images
Ilikuwa mwaka wa 1901 ambapo maisha ya daktari wa magonjwa ya akili Alois Alzheimer yalikutana na yale ya mgonjwa ambaye alimfanya kuwa maarufu miaka ya baadaye: Auguste Deter.
Daktari ana kesi ya kushangaza mbele ya macho yake, ambayo hajawahi kuona hapo awali.
Kupoteza kumbukumbu na ufahamu, afasia, kuchanganyikiwa, tabia isiyotabirika, paranoia na ulemavu wa kisaikolojia ni baadhi ya dalili zinazooneshwa na mama wa nyumbani Mjerumani mwenye umri wa miaka 51.
Baada ya kumfuata kwa muda mrefu, mtaalamu wa magonjwa ya akili aligundua nyumbani ugonjwa ambao haukujulikana wakati huo, lakini ambao leo unaathiri mamilioni ya watu duniani. Anauita "ugonjwa wa kusahau".
Mwanzo wa ugonjwa
Pengine umesikia neno "Alzheimers" (ugonjwa wa kusahau) mara nyingi katika maisha yako. Lakini pia kuna uwezekano kwamba unajua kidogo au hujui chochote kuhusu daktari ambaye aliigundua (na kuipa jina lake).

Alois Alzheimer alizaliwa mnamo Juni 14, 1864 katika kijiji kidogo katika jimbo la Ujerumani la Bavaria.
Alianza masomo yake ya matibabu huko Berlin, mji mkuu wa Ujerumani, kwa ombi la wazi la baba yake, mthibitishaji kitaaluma.
Aliamua kurudi katika mji wake ili kukamilisha masomo yake katika Chuo Kikuu cha Würzburg mwaka wa 1887.
Tangu wakati huo, alijitolea kwa magonjwa ya akili, neuropathology na utafiti wa magonjwa ya akili. Muda mfupi baada ya kupata diploma yake, akiwa na umri wa miaka 23, aliajiriwa kama daktari wa binafsi kwa mwanamke aliyekuwa na matatizo ya akili.
Anasafiri naye kwa miezi mitano, ambayo inamruhusu kufuatilia kwa karibu kutazama mabadiliko ya shida zake.
Baada ya uzoefu huu, aliajiriwa katika hifadhi ya manispaa ya watu wenye matatizo ya akili na kifafa katika jiji la Ujerumani la Frankfurt.
Huko alibobea katika utafiti juu ya tishu za mwili wa binadamu na gamba la ubongo. Pia alikutana na daktari maarufu, neuropathologist Franz Nissl, ambaye alishiriki naye maabara na kuunda urafiki mkubwa.
Wanasayansi hao wawili walifanya tafiti kadhaa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo ya akili. Mnamo 1894, Alzheimers alimuoa Nathalie Geisenheimer, ambaye alizaa naye watoto watatu. Mwanasayansi alikua mgane mnamo 1902.
Kukutana na Auguste Deter
Mwanzoni mwa miaka ya 1900, Alzheimer"alipata wazo kwamba magonjwa ya akili yalikuwa magonjwa kama magonjwa mengine," Conrad Maurer, profesa aliyestaafu wa magonjwa ya akili katika Chuo Kikuu cha Goethe huko Frankfurt, aliiambia BBC.

Alifikiri kwamba "kama kulikuwa na magonjwa ya mwili, pia kulikuwa na magonjwa ya ubongo". Kulingana na Maurer, daktari wa magonjwa ya akili alidhamiria kutafuta mgonjwa ili kuthibitisha hilo.
Wakati huo ndipo alipokutana na Auguste Deter ambaye , kutoka mwaka 1901, alipoteza kumbukumbu , alikuwa na wasiwasi na kupiga kelele au kulia kwa saa katikati ya usiku.
Alipomwona, Alzheimer alijisemea "hii ni kesi yangu", anasema Maurer. Daktari alifungua jalada la matibabu kwa ajili ya Deter ambalo lilipatikana katika miaka ya 1990 na timu ya Maurer, mkurugenzi wa hospitali ya magonjwa ya akili ambapo Alzheimers alifanya kazi.
"Ninamuonesha penseli, kalamu, mkoba, funguo, shajara na sigara, na anazitambua kwa usahihi," alisema. "Nilipomtaka aandike Mme Auguste D., anaandika Mme na kisha tunalazimika kurudia maneno mengine kwa sababu anayasahau. kuendelea katika uandishi wake na kurudia 'Nilipotea'".
Shukrani
Auguste Deter aliishia kuishi miaka mitano zaidi hospitalini. Alikufa Aprili 8, 1906.

Kwa mujibu wa Maurer, mara tu baada ya kifo chake, ubongo wake ulichambuliwa vizuri na mtaalamu wa magonjwa ya akili.
Ugonjwa wa Alzheimer ulitokeza alama nyingi ambazo bado zinaweza kuchunguzwa hadi leo kwa darubini. Kipengele muhimu zaidi ambacho daktari wa akili alipata katika ubongo wa Augustus kwamba cortex ya ubongo ilikuwa nyembamba kuliko kawaida (atrophic).
Pia aligundua mkusanyiko wa plaques na neurofilaments, ambayo ilielezea ugonjwa wake. Hata leo, "tunadhani hiyo ndiyo sababu ya ugonjwa," Maurer anasema.
Takribani miezi sita baada ya kifo cha Auguste, Alzheimer alitoa mada muhimu katika Mkutano wa 37 wa Kisaikolojia wa Ujerumani Kusini, akielezea mwendo wa kupungua kwake kiakili, dalili za neva, pamoja na changamoto zake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Daktari huyo alifariki mwaka wa 1915, akiwa na umri wa miaka 51, bila kushuku kwamba ugonjwa wa Auguste siku moja ungeathiri maisha ya mamilioni ya watu na kusababisha jitihada kubwa za utafiti wa kimataifa.
Wanasayansi wanamtaja sio tu mgunduzi wa ugonjwa wa neurodegenerative, lakini pia njia ya ubunifu ya utafiti, kwani utambuzi wa ugonjwa wa shida ya akili bado unategemea njia sawa za utafiti kama zile zilizotumiwa mnamo 1906.















