Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mashambulizi ya Iran na Israel: Nani kunufaika nani kupoteza?
"Uhusiano mzuri kwa ajili ya Iran." Hivi ndivyo baadhi ya wachambuzi walivyoelezea shambulio lisilokuwa na kifani la Iran katika eneo la ndani la Israel, baada ya Tehran kurusha zaidi ya makombora 300 na ndege zisizo na rubani kuelekea Israel, kwa mujibu wa jeshi la Israel.
Jeshi la Iran lilikuwa limetangaza kuwa mashambulizi yake ya ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya Israel yalikuja "kujibu shambulio la ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus, na kufikia maeneo yake yote yaliyolengwa."
Hapo awali Tehran iliapa kujibu mashambulizi ya anga ambayo yalilenga ubalozi wake mdogo katika mji mkuu wa Syria, Damascus, takribani wiki mbili zilizopita, ambayo yalisababisha vifo vya watu 13, wakiwemo wanajeshi saba wa Ulinzi wa Mapinduzi ya Iran na raia sita wa Syria.
Nchi mbili ziko kati ya hali ya kushinda au kupoteza
Kulikuwa na sherehe nyingi za Wairani za shambulio hilo, lakini Ali Nourizadeh, mtafiti wa Iran na mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Iran, ya Kiarabu huko London, anaamini kwamba shambulio hilo halikupata faida yoyote "badala yake, ilionesha udhaifu kwa sababu haukuangamiza shabaha yoyote nchini Israel, jambo ambalo lilizua kejeli katika mitaa ya Iran.” Alisema, akibainisha kwamba kama Tehran ingeendeleza vita vya kisaikolojia, ingepata mengi zaidi.
Kwa upande mwingine, Dk Eric Rundetsky, mtafiti wa sayansi ya Mashariki ya Kati na mtaalamu wa siasa za Israel katika Kituo cha Moshe Dayan katika Chuo Kikuu cha Tel Aviv, alisema kuwa Israel ilipoteza kwa kuleta dharura isiyo ya kawaida Israel, kwani anga ilikuwa inaleta hali ya wasiwasi, "na watu wengi waliogopa kujirudia kwa mashambulizi haya katika siku zijazo."
Ali Nourizadeh, anaamini kuwa Netanyahu anahisi kuwa na nguvu zaidi, kwa kuimarika uhusiano wake na Marekani na nchi za Magharibi.
Wakati mtafiti wa Israel alisema, "Nchi yake ilipoteza kutokana na shambulio hili na kufaidika wakati huo huo. Kwa upande wa hasara, shambulio hili lilithibitisha kwamba Israel haitambui kwamba inashughulika na nchi kubwa katika Mashariki ya Kati, na haipaswi kupuuza nguvu katika eneo hilo kwa sasa.
Pia ilithibitisha kuwa Israel haiwezi kuizuia Iran kama inataka kushambulia ndani ya Israel.”
Kurudia kuikumbatia marekani na changamoto zake
Kurudia kuikumbatia marekani na changamoto zake
Eric Rondetsky, mtafiti wa Israel, aliona kwamba shambulio la Iran pia lilikuwa na faida kwa Israel, akisema, "Shambulio hili linaweza kuwa hatua ya mabadiliko katika ngazi ya kisiasa, kwa sababu Israel inafurahia, kwa mara ya kwanza baada ya miezi, msaada wa Magharibi, na inaweza kurejea katika kukumbatia nchi hizi, hasa Marekani, baada ya mvutano usio na kifani katika mahusiano.” ".
Alizadeh, mtafiti wa Iran, alisema kuwa Tehran ilipoteza katika ngazi ya kisiasa, iwe ndani au nje. Iran ilipoteza nchi jirani na hakukuwa na uungwaji mkono kutoka kwa nchi yoyote, akiashiria kile alichokitaja kuwa ni majaribio ya kuiingiza Iran katika vita vya moja kwa moja na Marekani.
Je! Israel inapofikiria kuIjibu Iran, je Washington inaweza kuzuia vita vya kila upande?
Rondetsky alifahamisha kuwa kuna wasi wasi mkubwa ndani ya Israel na kwamba jambo hilo linaathiri vibaya Israel, akieleza kuwa kipindi cha hivi karibuni kumeshuhudiwa hasira zinazoongezeka kutokana na mashinikizo ya ndani sanjari na vita, pamoja na ukosefu wa maendeleo katika kablasha la waliotekwa nyara huko Gaza.
Zadeh pia anaamini kwamba Kiongozi wa Iran Ali Khamenei yuko chini ya shinikizo kubwa, sio tu mitaani, lakini pia kuna shinikizo kubwa kutoka kwa watu wanaowajibika ndani ya serikali. Kuna shinikizo kutoka kwa jeshi baada ya kuuawa makamanda saba wa Kikosi cha Quds mikononi mwa Israel. Jeshi la Walinzi lilikuwa likitaka kulipiza kisasi.
Ujumbe wa moto na kurejesha heshima
Brigedia Jenerali Hisham Jaber, mtaalamu wa kijeshi na kimkakati na mkurugenzi wa Kituo cha Mashariki ya Kati cha Mafunzo ya Kimkakati huko Beirut, alisema katika mahojiano na BBC News Arabic kwamba mshangao wa shambulio hilo ni kwamba haikuwa ya kushangaza, na ilitanguliwa na mashambulio ya namna mbili.
Wiki za vita vya kisaikolojia, kwani Israeli ilikuwa katika hali ya hofu na hii ilisababisha uharibifu. Kisaikolojia na nyenzo, kwa sababu ya usumbufu wa vifaa vingi na kuondoka kwa raia wengi kutoka Israeli.
Nini kilitokea Israel baada ya shambulio la Iran?
Jaber anaamini kuwa Tehran imenufaika kijeshi na kistratejia pia kutokana na kubadilisha kanuni za ushiriki. Kisiasa, imepata tena baadhi ya heshima yake ambayo ilipoteza katika miaka ya hivi karibuni wakati wa kufuata kile kinachoitwa "sera ya subira ya kimkakati," kulingana na maelezo yake.
Mtaalamu huyo wa masuala ya kijeshi anaendelea kusema kuwa Iran ilirusha kiasi hiki kikubwa cha ndege zisizo na rubani "ili tu kuvuruga ulinzi wa anga wa Israel," akibainisha kuwa Iron Dome haikuwa peke yake katika kuweza kuyarudisha makombora hayo, kwani Marekani na Uingereza ziliisaidia kupitia vituo. katika Mashariki ya Kati.
Kuhusu jibu ambalo Israel iliahidi, Jaber alisema, “Ikiwa Israel itachagua jibu la kijeshi, inaweza kufika Iran na makombora yake, huku haiwezi kuendelea na kufikia umbali mrefu. Mara itakapofika bara, majibu ya Iran yatakuwa makali. Israel inaweza kulipua Iran kwa njia ya ndege, lakini si ndege hizi zinaweza kufika tu ikiwa zitaruka juu ya nchi za Kiarabu, ambazo Iran imeonya dhidi yake, au ikiwa zitaondoka kutoka kwa kambi za kijeshi za Marekani, jambo ambalo Marekani haitaruhusu.
Kubadilisha dira na kurejesha kujiamini
Fawaz Girgis, profesa wa uhusiano wa kimataifa mjini London, anaamini kuwa mafanikio ya Israel ni makubwa kuliko yale ya Iran. Kwa sababu mashambulio ya Irani hayakusababisha uharibifu katika Israeli au vifo vya wanadamu, na pia kwa sababu Magharibi yote sasa inasimama na Israeli, na Merika inajaribu kuhamasisha uungaji mkono wa Magharibi katika suala la silaha, ushirikiano wa kijasusi, na msaada wa kifedha kwa Israeli.
Girgis anasema kwamba Payne, kwa kuitisha mkutano wa haraka wa Kundi la Saba ili kuhamasisha uungwaji mkono kwa Israeli, anaionyesha kama mwathirika katika kile kinachotokea, kama anavyoweka.
Je, hali ikoje nchini Iran baada ya shambulio la Israel?
Pia, "Netanyahu atashinda kisiasa baada ya umakini kuelekezwa, hata kwa muda, kutoka kwa hali mbaya na ukatili uliofanywa katika Ukanda wa Gaza," Gerges anaongeza, akionesha kwamba Netanyahu atafaidika kwa kurejesha uhusiano na Magharibi, haswa na Rais Joe Biden , baada ya nchi za Magharibi kuikosoa Israel hivi karibuni dhidi ya hali ya Matukio huko Gaza,
Hii ni pamoja na faida za ndani za kisiasa.
Kuhusu mafanikio ya Iran kutokana na shambulio hilo, Girgis anasema kuwa Tehran ilipata faida kisiasa; Iliweza kujionesha kwa watu wake, washirika wake, na maadui zake kuwa na utashi wa kisiasa na kuweza kuingia katika makabiliano ya moja kwa moja na Israel.
Profesa wa Uhusiano wa Kimataifa, Fawaz Girgis, anaamini kuwa, kilichofanywa na Iran kilionesha kuwa Israel haiwezi kujilinda peke yake isipokuwa kupitia washirika wake wa Magharibi, baada ya Marekani, Uingereza, Ufaransa na Jordan kuangusha makombora mengi ya Iran.
Aliongeza kuwa lengo kuu la Israel katika mashambulizi yake ya mara kwa mara dhidi ya Iran katika kipindi cha hivi karibuni ni kuonesha kwamba Iran ilikuwa dhaifu na haikuthubutu kukabiliana nayo, "lakini mashambulizi hayo yalivunja mtazamo huu," alisema.
Girgis anasema kuwa eneo hilo sasa liko kwenye hali ngumu, kwani Iran imesema kuwa itaongsana, na hii kwa sasa inaweka eneo hilo kwenye shimo baya la kisiasa, kijeshi na kiuchumi.
Imetafsiriwa na Lizzy Masinga