Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je ndege iliokuwa imembeba Prigozhin iliangukaje?
Upekee wa ajali ya ndege ya Yevgeny Prigozhin ni kwamba tukio hili lina limechanganyika na siasa - mmiliki wa Wagner na wapiganaji wake walihusika katika mgogoro na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Kuna madai ya aina mbili, wapo wanaosema mlipuko ulitokea ndani ya ndege yenyewe. Wengine wakidai ilidunguliwa kutoka ardhini. Kila mmoja ana hoja zake. Lakini hakuna jibu la wazi limepatikana kwa kile kilichotokea.
Uchunguzi unasemaje
Shirika la Habari la RBC, likinukuu chanzo kutoka vyombo vya usalama, liliripoti kwamba uchunguzi utazingatia madai yote juu ya kile kilichotokea, ikiwa ni pamoja na makosa ya rubani, matatizo ya kiufundi na hujuma kutoka nje.
Maeneo yote makubwa yatachunguzwa, pamoja na maeneo madogo na yale ya kawaida. Kwani anga kwa ujumla hufuata sheria na taratibu, na ajali mara nyingi hutokana na ukiukaji wa hizo sheria na taratibu.
Uchunguzi unaweza kutazama sampuli za mafuta, makontena ambayo ndege hiyo ilijazwa mafuta, data zake za kiufundi zitaangaliwa, pamoja na hati za matibabu za wafanyakazi zitakaguliwa. Hatua hizi zote zimo katika aya ya 2.3 ya Kanuni za uchunguzi wa ajali za ndege.
Rekodi za picha
Mojawapo ya rekodi zinaonyesha jinsi ndege inavyoanguka chini, wingu jeupe la moshi linaonekana mbinguni. Mwanamke anayezungumza akiwa na kamera anasema kuwa milipuko miwili ilisikika na kwamba droni ilidunguliwa. Pia anasema "vipande vinaruka."
Aidha, picha za mabaki hayo zimetolewa na picha mbili kati ya hizo zinasemekana kuonyesha matundu madogo ambayo yanaonekana kama zilipigwa na kombora la kutungulia ndege. Picha zingine zinaonyesha sehemu ya mkia wa ndege, ambayo haionyeshi alama ya matundu.
Hakuna taarifa kwamba wafanyakazi walitoa ishara ya uwepo wa tatizo. Wala hakukuwa na ripoti ya hali mbaya ya hewa.
Mlipuko kwenye Ndege
Ni ukweli kwamba ndege ilianza kuanguka angani. Wataalam wa anga pekee wanaweza kujibu swali hili bila shaka. Moja ya vipande vya ndege hiyo kilipatikana kilomita mbili kutoka eneo la ajali. Wakati inaanguka Injini zilikuwa bado zinafanya kazi.
Madai kuwa kulitokea mlipuko ndani ya ndege ni madai magumu zaidi. Ni vigumu kuweka kifaa chenye nguvu cha kulipuka kwenye ndege kwa sababu ya tanki la mafuta, bila shaka ingeshika moto. Lakini video hazionyeshi moto mkali wakati ndege inadondoka.
Ikiwa mlipuko ulitokea kwenye sehemu ya mkia, kwanini bawa moja la ndege ndio lipatikane umbali mkubwa na ndege ilipoanguka.
Kombora kutoka ardhini
Hata mfumo wa ulinzi wa anga wa masafa mafupi wa Pantsir S1 una uwezo wa kufikia umbali wa ndege hiyo ilipokuwa.
Gazeti la Financial Times liliripoti, likinukuu chanzo cha Magharibi, kwamba ndege hiyo ilidunguliwa na mfumo wa ulinzi wa anga, lakini haikutoa maelezo. Madai hayo pia yalitolewa na mtandao wa kijamii wa Telegram unaomilikiwa na Wagner.
Madai haya yanaungwa mkono na hoja kadhaa. Moshi mweupe unaonekana katika mojawapo ya video inaweza kuwa moshi wa mlipuko wa roketi. Pili, kuna maneno ya mashahidi ambao walisikia mlipuko. Picha za vipande vya ndege, kunaonekana mashimo madogo ambayo yanaweza kuwa alama ya vipande vya kombora.
Wapinzani wa madai haya wanasema. Wingu jeupe angani linaweza kuwa matokeo ya bomu kutoka kwenye ndege. Wakati huo huo, hakuna mwonekano wa roketi ikikimbia angani. Sauti ya mlipuko iliyosikika na mashahidi pia inaweza kuwa matokeo ya mlipuko ndani ya ndege.
Madai mengine
Mnamo Septemba 29, 2006, ndege aina ya Legacy iligongana angani na ndege ya shirika la Boeing 737. Na kusababisha zote mbili kuharibika vibaya. Ndege aina ya Boeing ilianguka na kuua watu 154. Licha ya uharibifu mkubwa ndege ya Legacy iliweza kutua.
Mshauri wa masuala ya usafiri wa anga John Strickland aliambia BBC kuwa "ndege kuanguka chini wakati wa safari ya kawaida ni nadra sana." Alielezea Embraer ni kampuni yenye "rekodi bora ya usalama".