Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi kubwa 5 za Soka Ulaya jioni hii
Manchester City na Leipzig zinakamilisha uhamisho wa mlinzi Joško Gvardiol ambapo makubaliano yatasainiwa Ijumaa na mchezaji huyo atafanyiwa vipimo siku hiyo kabla ya kutua City. Gvardiol anatua kwa ada ya €90m, ambayo itamfanya kuwa beki wa kati ghali zaidi duniani (Romano)
Harry Kane huenda akasalia Tottenham Hotspurs iwapo timu hiyo na Bayern Munich hazitafikia makubaliano kabla ya ligi kuanza. Mazungumzo yanaendelea baina ya vilabu hivyo na Bayern ikipaswa kuongeza dau lake la awali £82m ili kumnasa nahodha huyo wa England aliyesalia na mwaka mmoka katika mkataba wake Spurs (Sky sport Football).
Mlinzi wa Arsenal, Takehiro Tomiyasu ataendelea kusalia London licha ya ripoti kudaiwa anasakwa na moja ya vilabu vikubwa vya Italia (Romano).
Rais wa Besiktas Ahmet Nur Cebi amekutana na Alex Oxlade-Chamberlain kwenye hoteli moja jijini London.
Klabu hiyo ya Uturuki inajaribu kumshawishi winga huyo wa zamani wa Arsenal, Oxlade-Chamberlain, ambaye ametemwa hivi karibuni na Liverpool, kujiunga nao katika dirisha hili la usajili.
West Ham haijakata tamaa ya kumsajili James Ward-Prowse –licha ya Southampton kukataa ofa yao ya £30m ikitaka £40m. Ingawa imeanza kuangalia mbadala wake, lakini inaamini wanaweka kumpata kabla ya ligi kuanza mwishoni mwa juma lijalo.