Je, India inabadilisha jina lake kuwa Bharat?

"India, hiyo ni Bharat, itakuwa muungano wa majimbo," inasema ibara ya kwanza ya katiba. Utangulizi unasema: "Sisi, watu wa India..."

Bharat hutumiwa sana kuitaja India katika lugha ya Kihindi. Linapokuja suala la mawasiliano rasmi kwa Kiingereza, India hutumiwa kila wakati.

Serikali ya Narendra Modi sasa inabadilisha utaratibu huu wa muda mrefu. Imetuma mwaliko wa chakula cha jioni kwa jina la 'Rais wa Bharat' katika mkutano wa tarehe 9 Septemaba wa G20.

Na jina hilo limetolewa zaidi ya mara mbili na kutolewa kwa vyombo vya habari kuhusu mkutano wa kilele wa Asean-India ambao unamtaja Narendra Modi kama 'Waziri Mkuu wa Bharat'.

Bharat ni nini?

Fasihi ya Kihindu inafafanua ardhi iliyoko kati ya Himalaya na bahari kama "Bharatvarsh".

Kwa mujibu wa hadithi za Kihindu, Bharata alikuwa Mfalme wa Hastinapura (sasa akiitwa Hastinapur na yuko mashariki mwa Delhi). Alishinda nchi yote na akachukuliwa kama mfalme mwenye haki.

Katika maandishi ya kale ya Kihindu, Rig Veda, Bharata linatajwa kama jina la kikundi cha watu.

Bharata ywa ulimwengu huko Sanskrit pia inamaanisha ardhi ambayo inathamini na kutoa. Inaweza kuashiria utamaduni.

Waziri Mkuu wa India Jawaharlal Nehru aliandika katika mwaka 1927: "India ilikuwa Bharata, nchi takatifu ya Wahindu, na hili linaambatana na umuhimu wake kwamba maeneo makubwa ya Hija ya Hindu yako katika pembe nne za India."

Lakini Bharat sio mtu wa kihistoria.

Msomi wa Paris Catherine Clementin-Ojha aliandika katika waraka wake wa mwaka 2014: "Bharata ni mazungumzo juu ya nafasi lakini mazungumzo ambayo hayaruhusu uwakilishi wa unaoweza kushuhudiwa wa nafasi hiyo. Haiwezekani kwa msingi wa hotuba hiyo kuchora ramani katika maana ya kisasa ya neno."

Vipi kuhusu majina ya India na Hindustan?

Waajemi waliuita mto Indus 'Hindu' ambao uligeuka kuwa 'India' katika lugha ya Kilatini. Jina 'India' pia ni la kale.

Waislamu wa Mughals ambao walitawala nchi kwa zaidi ya karne mbili walijivunia kama "Badshahs of Hindustan", watawala au wafalme wa Hindustan.

Jina 'Hindustan' pia linatokana na Kiajemi. Kwa hivyo India na Hindustan ni majina ya muda mrefu yaliyotangulia utawala wa kikoloni wa Uingereza ambao ulianza na ushindi wa mafanikio wa Bengal mnamo 1757.

Wafanyabiashara wa Uingereza waliwasili India mwaka 1600 kuanzisha Kampuni ya India Mashariki.

Nchi hiyo pia ilijulikana kama 'Indie' katika toleo la kwanza la Biblia ya King James kwa Waprotestanti. Matukio haya yote yalifanyika kabla ya Uingereza kuitawala India.

Hofu na upinzani

Waziri Mkuu Narendra Modi ametawala India tangu mwaka 2014 na anatoka chama cha Bharatiya Janata Party (BJP), ambacho kiko madarakani katika majimbo mengi pia.

Ni chama cha mrengo wa kulia chenye uhusiano wa karibu na Rashtriya Swayamsevak Sangh (Shirika la Kitaifa la Wanaojitolea) ambalo linasema India inapaswa kuwa 'taifa la Kihindu'.

Narendra Modi alijiunga na RSS akiwa kijana na akainuka kupitia

RSS ambayo ilipigwa marufuku mara tatu baada ya uhuru wa India.

Mara ya kwanza baada ya mauaji ya Mahatma Gandhi mwaka 1948 ambapo RSS ilituhumiwa kupanga mauaji ya kiongozi wa taifa lakini baadaye tuhuma hizo zilifutwa.

Makundi ya kizalendo ya Kihindu yalichangia pakubwa katika mapambano ya uhuru wa India.

Serikali inasema kubadilisha jina hilo kuwa 'Bharat' kutasaidia taifa hilo kuondoa uhusiano wake wa kikoloni wa Uingereza.

"Uamuzi wa kutumia 'Bharat' ni kauli kubwa dhidi ya fikra za kikoloni," anasema Waziri wa Elimu wa India Dharmendra Pradhan.

Lakini jina la India limetumika kwa zaidi ya milenia mbili.

Pengine kumbukumbu ya zamani zaidi ya India zinatoka kwa mwanahistoria wa Kigiriki Megasthenes, aliyezaliwa 350BC. Aliandika vitabu vinne kwa jina la 'Indica'.

Mwandishi wa maigizo ya Kiingereza William Shakespeare pia alitumia jina la India katika kazi yake."Taji langu liko moyoni mwangu, sio kichwani mwangu, halijapambwa na almasi na mawe ya India," anasema Mfalme Henry VI katika mchezo Henry VI sehemu ya 3, inayoaminika kuwa iliandikwa 1591-2.

Serikali ya Modi imetoa wito wa kufanyika kwa kikao maalum cha bunge kuanzia Septemba 18 hadi 22. Wanasiasa wa upinzani na wachambuzi wanabashiri kuwa hii inaweza kuwa kubadilisha jina la nchi.

Itakuwa kikao cha kwanza katika jengo jipya la bunge lililojengwa ambalo tayari lina ramani ya Bharat Kubwa.

Ramani hii inajumuisha maeneo ya nchi jirani kama vile sehemu za Afghanistan, Pakistan nzima, Nepal, Bangladesh, Sri Lanka na Myanmar.

Majirani wa India wameandamana rasmi.

Wakosoaji wanasema BJP inajiandaa kutumia picha za kitamaduni za Kihindu kama alama kuu za kihistoria na upinzani tayari unajiandaa kuonyesha upinzani dhidi ya hatu hiyo.

"Wakati hakuna pingamizi la kikatiba la kuiita India 'Bharat', ambayo ni moja ya majina mawili rasmi ya nchi, natumaini serikali haitakuwa na ujinga sana kiasi cha kuachana kabisa na 'India', ambayo ina thamani ya chapa isiyohesabika iliyojengwa kwa karne nyingi," Shashi Tharoor, mbunge wa chama cha India National Congress, aliandika kwenye X, Tovuti hiyo zamani ilijulikana kama Twitter.