Manchester City: Je, yeyote anayeweza kuwazuia washindi wa Ligi ya Premier wa Pep Guardiola?

Ubingwa wa tano wa Ligi Kuu ya Manchester City katika kipindi cha miaka sita na jinsi ulivyopatikana lazima upeleke hofu kwa wale wanaotafuta njia za kuwaondoa mabingwa wa Pep Guardiola.
City walihifadhi taji lao huku Nottingham Forest wakiilaza Arsenal siku ya Jumamosi na itakuwa mbaya kwa wapinzani wowote wanaotafuta kupunguza hamu yao ya mafanikio.
Kwa hakika, nia ya City ya kuendeleza ubingwa wao inaonekana kuimarika.
City ndio timu ya kwanza kushinda Ligi ya Premia kwa misimu mitatu mfululizo tangu Manchester United mnamo 2006-07, 2007-08 na 2008-09.
Pia wako mbioni kuiga historia ya United ya 1999 na kuwa timu ya pili ya Uingereza kutwaa taji hilo kisha kushinda Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa.
Fikra za Guardiola zimejenga nasaba ambayo itaimarika zaidi.
Klabu hiyo ilishtakiwa mapema mwaka huu na Ligi ya Premia kwa kukiuka zaidi ya sheria zake 100 za kifedha kati ya 2009-2018, lakini City, ambao mara zote wamekanusha makosa ya kifedha, wanasema "wanatarajia suala hili kuahirishwa mara moja na kwa wakati".
Tayari watakuwa vinara wa kutwaa taji hilo tena msimu ujao - kwa hivyo vilabu vingine vinavyokodolea macho taji hilo vina msimu mfupi wa kupango namna ya kuwaondoa mchezoni wanasoka hao wanaoonekana kutozuilika.
Je, kuna mtu yeyote anayeweza kuihimili mikikimikiki ya City?
Uwezo wa City wa kutoa shinikizo na kukabiliana hata na wapinzani wenye nguvu umekuwa mazoea yao, wameshiriki michezo 24 bila kushindwa na kushinda ligi na kuandaa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester United uwanjani Wembley, kabla ya mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Inter Milan mjini Istanbul.
Rekodi yao inawachapa wapinzani wao kisaikolojia, katika miaka ya hivi karibuni Liverpool na msimu huu Arsenal, ikionekana kuwa sare inaweza kuondoa hisia kama kushindwa.
Kuimarika kwa Liverpool chini ya Jurgen Klopp kumeleta taji moja pekee - ambalo linakubalika kuwa la kwanza katika miaka 30 - katika kile kinachoonekana kama mwamko wa aina yake Anfield.

Chanzo cha picha, Getty Images
The Reds walipoteza mara mbili kwa pointi moja katika siku ya mwisho - kwa mfululizo wa ushindi wa City mara 14 mwaka 2019, kabla ya mabao matatu ya dakika za lala salama ndani ya dakika tano yakisaidia kikosi cha Guardiola kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kuifunga Aston Villa siku ya mwisho ya msimu uliopita.
Arsenal ilikuwa nyingine msimu huu, ilichapwa mara mbili na City kwa mtindo wa kuridhisha, kabla ya kuchakazwa na kuwekwa katika hali ya kutoweza kuepukika.
Sio tu shinikizo la soka ambayo City waliweka kwa wapinzani wao. Pia ni kiakili na kimwili.
Je, nani atakuwa na uwezo wa kuikabili City mwaka ujao?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Je, nani atakuwa na uwezo wa kukabili City mwaka ujao?
Liverpool wanaweza kuwa wameshuka kasi ya kuwania taji msimu huu, na kumaliza msimu mikono mitupu baada ya kushinda Kombe la FA na Kombe la Ligi - wakati wa harakati zao za kuwania kuweka historia ya kucheza mara nne mwaka jana.
Kikosi cha Klopp kilionekana kusambaratika kiafya na kisaikolojia kwa muda kutokana na juhudi zao, na kukosa ubingwa kwa njia ya kukatisha tamaa kisha kupoteza fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid.
Mwanzoni mwa msimu ujao, hata hivyo, watarajie Liverpool kuimarika na kufufuka upya wakielekeza juhudi zao katika kupata sura mpya kwenye safu ya kiungo wa kati inayohitaji marekebisho, kitu ambacho tayari kinaendelea na kutarajiwa kuwa na mfululizo wa ushindi kuelekea mwisho wa kampeni hii.
Jude Bellingham, masikitiko makubwa kwa mashabiki wengi wa Liverpool, hatawasili Anfield lakini nguvu kazi muhimu itawasili, ikiwa ni pamoja na Mason Mount wa Chelsea, mshindi wa Kombe la Dunia la Argentina Alexis Mac Allister na Bayern Munich huku wakimwacha nje Ryan Gravenberch.
Klopp ameweka wazi nia yake na kutaka kuanza kazi yake kabla ya msimu kuanza, mapema iwezekanavyo tayari kwa mashambulizi mapya ya kutwaa mataji.
Haitashangaza kuona Liverpool wakifanya upya mashambulizi yao dhidi ya City wakiwa kileleni mwa jedwali na kuibuka kuwa wapinzani wao wakubwa.
Arsenal imekuwa katika nafasi ya kutwaa ubingwa, ingawa imesababisha machungu mengi kwa mashabiki baada ya kuteleza na kuchukuliwa kwa Ligi ya Premia lililokuwa mikononi mwao kwa mara ya kwanza tangu 2003-04, na sasa itataka kupata mazuri zaidi.
Meneja Mikel Arteta atadai maboresho yanayohitajika baada ya msimu uliokuwa wa kipekee kwao ambapo The Gunners walitarajiwa kupigania kuwa katika nafasi nne bora zaidi, wala sio kusukuma City kutwaa ubingwa.
Arsenal wanatumai awamu inayofuata itakuwa na mambo mazuri kwao yenye kujumuisha nahodha bora wa West Ham United Declan Rice.
Ikiwa mchezaji huyo 24, anaweza kusajiliwa, hii haitakuwa tu ishara ya dhamira yao ya kutinga tena kileleni wakati wa msimu lakini pia kuashiria kwa nguvu zaidi kwamba Uwanja wa Emirates kwa mara nyingine tena ni marudio ya wale walio na nia kubwa ya kutafuta zawadi kubwa zaidi.
Manchester United imepiga hatua za polepole kuelekea kuibuka kidedea kwa miaka inayosimamiwa na makocha nyota kama Ole Gunnar Solskjaer chini ya Erik ten Hag msimu huu.
Walishinda Kombe la Ligi, taji la kwanza tangu 2017, huku wakifukuzia nafasi ya nne-bora na kufika fainali ya Kombe la FA, lakini uimarishaji zaidi unahitajika kufanywa kabla ya kuwapa changamoto City katika harakati za kuwania taji hilo.
Kipaumbele kinachofuata cha Ten Hag lazima kiwe mfungaji mabao ili kuipa United makali waliyokosa, hasa ugenini.
Haishangazi nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane amekuwa akihusishwa na kutaka kuhama Tottenham, huku mchezaji mahiri wa Napoli, Victor Osimhen pia akivutia nadhari.
Ten Hag amesogeza mbele United, akijenga msingi wa kuvutia, lakini bado ni vigumu kuwaona wakiwa wapinzani wazuri kwa City kwenye Ligi ya Premia - ingawa itakuwa ya kuvutia kuona ni athari gani wamiliki wapya wanaweza kuwa nayo.
Newcastle United wameelekea kwenye Ligi ya Mabingwa chini ya meneja Eddie Howe, wakichochewa na utajiri mkubwa wa umiliki wao wa Saudi Arabia na kazi nzuri kwenye soko la hisa, ambako kumewadia kwa kasi ambayo pengine imewashangaza hata wao wenyewe.
Ni vigumu kuona matarajio yao yakitimizwa pengine kwa wakati huu lakini upinzani katika kutwaa ubingwa inaweza isije msimu ujao ila bila shaka ndio lengo lao la muda mrefu.
Na kisha kuna – Chelsea ambayo mengi hayajafahamika kuihusu.
Blues imekuwa na msimu mbaya sana chini ya wamiliki wapya Todd Boehly na Behdad Egbhali.
Wametumia takriban pauni milioni 600 bila mpangilio, meneja Thomas Tuchel alitimuliwa na mrithi Graham Potter akadumu kwa mechi 31 pekee.
Mauricio Pochettino amekubali kufuta kile kinachoonekana kama makosa yaliyojitokeza lakini bila shaka kuna vipaji kikosini.
Ikiwa Pochettino ataruhusiwa kufanya maamuzi makubwa, bila kusajili wachezaji, na kuleta aina ya soka ya kusisimua na usimamizi wa watu wenye busara ambao ilimfanya kupendwa sana na mashabiki wa Spurs, basi kunaweza kuwa na timu yenye mafanikio ndani ya Chelsea inayosubiri Muargentina huyo.
Hata hivyo, City itabaki kuwa timu ya kushinda.
Kwa matamanio yote ya wapinzani wa City, bado ni vigumu sana kujenga hoja zinazowazuia kusherehekea taji lingine wakati huu msimu ujao.
Kikosi cha Guardiola hakitatulia tu kusubiri wengine wamfikie - atajua tu tamaa za wapinzani za kutaka kuwaondoa kwenye nafasi hiyo lakini tayari atakuwa anafanya mipango ya kuwazima.













