Vita vya Ukraine: Mashambulizi ya Ukraine ya kusini yamekwama

USSIAN MINISTRY OF DEFENCE

Chanzo cha picha, RUSSIAN MINISTRY OF DEFENCE

Maelezo ya picha, Urusi ilitoa picha za vifaru vilivyoharibiwa siku za awali za mshambulizi

Jenerali anayehusika na mashambulizi ya Ukraine upande wa kusini, anasema Urusi imezika safu ya mabomu na kuimarisha ulinzi, na kufanya vigumu kwa zana za kijeshi, ikiwa ni pamoja na vifaru na magari ya kivita yanayotolewa na nchi za Magharibi, kusonga mbele.

"Jeshi la Urusi limeonyesha utaalamu kwa kuzuia vikosi vya Ukraine kusonga mbele haraka," Jenerali Oleksandr Tarnavskyi ameiambia BBC. "Simdharau adui," anaongeza.

Kufikia sasa kuna ushahidi mdogo wa kuonyesha vifaru vilivyotolewa na nchi za Magharibi na magari ya kivita yameweza kuleta usawa katika vita kwa upande wa Ukraine.

Vifaru kadhaa vya Leopard na magari ya Marekani ya Bradley yameharibiwa katika siku za kwanza za mashambulizi, karibu na mji wa Orikhiv.

Kikosi cha 47 cha Ukraine, ambacho kwa kiasi kikubwa kimefunzwa na kupewa vifaa na nchi za Magharibi kujaribu kuvunja njia za Urusi, kimekwama kusonga mbele kwa sababu ya mabomu yaliyozikwa.

Urusi ilitoa vidio nyingi za tukio hilo ikidai mashambulizi ya Ukraine yameshindwa.

Tulitembelea karakana ya kikosi hicho, iliyofichwa kwenye msitu nyuma ya mstari wa mbele wa mapambano, ambapo sasa wanajaribu kukarabati zaidi ya magari kumi na mbili ya kivita – mengi yao yakiwa ni Bradleys.

Yalifika yakiwa mazima lakini sasa yamebeba makovu ya vita. Magari yaliyovunjika na matairi yaliyopinda - ishara kwamba yamekanyaga mabomu ya Urusi.

Serhii, mmoja wa wahandisi, anasema: "Kadiri tunavyoweza kuyakarabati kwa haraka, ndivyo tunavyoweza kuyarudisha kwenye mstari wa mbele kwa haraka ili kuokoa maisha ya mtu."

gfrtrt
Maelezo ya picha, Serhii
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Lakini anakiri zingine hazijakarabatiwa na italazimika kutafutiwa vipuri au kurudishwa kwa washirika wetu ili kuundwa upya. Wakati silaha za Magharibi zimewapa wanajeshi wa Ukraine ulinzi bora, hazijaweza kupenya safu za mabomu ya Urusi.

Tuliposafiri upande wa kusini, tuliona pia magari ya kivita ya Uingereza aina ya Mastiff yakiwa yameharibiwa.

Kikosi cha 47 sasa kinatumia baadhi ya vifaru vyake vya zamani vya enzi ya Usovieti kusafisha maeneo yenye mabomu ya ardhini. Lakini vifaru hivyo haviwezi kuepuka vilipuzi vilivyofukiwa ardhini, hata vikiwa vimewekewa vifaa maalum vya kusafisha mabomu.

Karibu na mstari wa mbele wa mapambano, kamanda wa vifaru, Maksym, alituonyesha kifaru chake cha T-64 kilichoharibiwa hivi karibuni. Kimewekwa mashine mbili mbele ili kutegua mabomu ya ardhini.

"Kwa kawaida mashine zetu zinaweza kustahimili hadi milipuko minne," anasema. Lakini Warusi, wameweka mabomu juu ya mabomu ili kuharibu vifaa vya Ukraine vya kusafisha mabomu.

"Ni vigumu sana kwa sababu kuna mabomu mingi," Maksym anasema, akiongeza kuwa mara nyingi kuna zaidi ya safu nne zenye mabomu mbele ya safu za ulinzi za Urusi.

Ni uchungu kutazama vita vinavyoendelea kwa Doc na timu yake ya upelelezi wa ndege zisizo na rubani kutoka Jeshi la Kujitolea la Ukraine. Doc, alishiriki katika mashambulizi ya mwaka jana huko Kherson. Lakini anasema wakati huu mambo ni magumu.

Anasema kwa mara ya kwanza, askari wanajeruhiwa na mabomu ya ardhini zaidi kuliko makombora: "Tunaposonga mbele tunakutana na maeneo yenye mabomu kila mahali."

wewreqqrgr
Maelezo ya picha, Rubani wa droni za Ukraine, Doc

Doc ananionyesha video aliyoirikodi hivi majuzi kutoka katika moja ya ndege zake zisizo na rubani, huku wanajeshi wa Ukraine wakielekea kwenye mtaro wa Urusi.

Mlipuko mkubwa unatokea mara tu askari wanapoingia. Mtaro huo ulikuwa mtupu lakini ulikuwa na mabomu. Doc anasema vikosi vya Urusi sasa vinatumia mabomu yanayolipuliwa kwa mbali.

Kuna mantiki ya kijeshi la Ukraine kushambulia kusini. Eneo hilo linatazamwa kama ufunguo wa kuvigawanya vikosi vya Urusi na kufikia miji inayokaliwa ya Melitopol na Mariupol - hadi Crimea.

Jenerali Tarnavsky anasema vikosi vyake vinafanya "kazi ngumu na ya maumivu". Anaeleza "ulinzi wowote unaweza kuvunjwa lakini kunahitajika subira na vitendo vya ustadi".

Pia, anaamini Ukraine inamchosha polepole adui yake, Urusi. Vilevile anaamini, Urusi haijali kupoteza wapiganaji wake, na mabadiliko ya hivi karibuni katika uongozi wao wa kijeshi "inamaanisha kuna mambo hayako sawa."

“Polepole, mashambulizi yanafanyika na hakika yatafikia lengo lake,” anasema.

Ninamuuliza Jenerali Tarnavsky, je tunaweza kusema kuna mafanikio au kufeli?

Anatabasamu na kujibu: "Kama mashambulizi yasingefaulu, nisingezungumza nawewe sasa."

fddfdfdf