Omar al-Bashir: Hivi ndivyo Sudan inavyolipa gharama za mateso ya miaka 30 ya utawala wake

Sudan

Chanzo cha picha, Getty Images

The conversation

Tangu uhuru mwaka 1956 Wasudan wamepitia mapinduzi 35, majaribio ya mapinduzi na njama za mapinduzi - ikiwa ni zaidi ya nchi nyingine yoyote ya Afrika. Wakati uasi wa mwaka 2019 dhidi ya dikteta wa muda mrefu Omar al-Bashir ulipounda serikali ya mpito ya kijeshi na kiraia, Wasudan walitumai kuwa nchi yao ingeingia kwenye utawala wa kidemokrasia.

Lakini matumaini yao yalikatizwa Oktoba 2021 wakati Abdel Fattah al-Burhan alipoongoza mapinduzi dhidi ya wenzake katika serikali ya mpito.

Katika duru ya hivi karibuni mzozo ulioanza tarehe 15 Aprili 2023, vita vya wenyewe kwa wenyewe vinakaribia ambapo wale walionufaika na kudondoka kwa Bashir wanapigania maslahi yao.

Nimesoma siasa za Sudan kwa miaka 15, na awamu ya hivi karibuni ya mzozo ndiyo mbaya zaidi katika historia ya nchi hiyo. Na urithi wa utawala wa Bashir ni kiini cha msiba huu.

Bashir alihakikisha taasisi za serikali zinatumikia utawala wake. Alichagua mzozo badala ya maelewano katika kukabiliana na makundi yaliyotengwa kisiasa huko Darfur, magharibi mwa Sudan, na kusini. Alitumia nguvu kushikilia madaraka. Hii ilichochea uungwaji mkono wake kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), ambavyo vilitumiwa kufuatilia waasi wa kikanda na jeshi.

Urithi wa Bashir unaonekana kuendelea mpaka leo. Washirika wake wa zamani wamejipanga kuzuia utawala wa mpito wa kiraia. Hili lilikuwa limeahidiwa kwa watu wa Sudan chini ya mkataba uliotiwa saini Disemba 2022 na jeshi na muungano wa wawakilishi wa kiraia.

Kwa maoni yangu, hofu ya Burhan ya majaribio ya kiraia ya kutawala ilimfanya kusalia na vipengele muhimu vya mfumo wa Bashir. Hili limekuwa na mkono wa mgawanyiko katika mzozo wa sasa.

Itikadi ya Uislamu

Sudan

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Picha iliyochapishwa Julai 21, 2020 ikimuonyesha rais wa zamani wa Sudan akishuka kwenda Mahakamani kwa tuhuma mbalimbali zinazomkabili na alizozitenda wakati wa utawala wake
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Sehemu ya urithi wa Bashir inahusiana na siasa za Kiislamu. Ni urithi huu ambao Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana zaidi kama Hemedti na ambaye anaongoza kikosi cha wanamgambo, alitaka kuutumia vibaya ili kumpendelea alipomtaja Burhan kuwa "Muislamu mwenye msimamo mkali".

Hili lilitengenezwa dhidi ya mamlaka ya Magharibi. Lakini halikuwa sahihi. Ili kuelewa kwa nini, mtu anapaswa kuelewa mwelekeo wa kiitikadi wa utawala wa Bashir.

Wakati Bashir alipofanya mapinduzi mwaka 1989, alikuwa anakaimu kama mwakilishi katika jeshi lililokuzwa kwa uangalifu na National Islamic Front ambacho ni Chama cha siasa kilichoratibu mapinduzi hayo na Bashir.

National Islamic Front iliongozwa na Hasan al-Turabi, ambaye aliongoza Harakati ya Kiislamu ya Sudan tangu miaka ya 1960. Hakuwa sawa kufuatia kushindwa kwake kutambulisha sheria ya Kiislamu (Sharia), kupitia bunge.

Mara tu baada ya mapinduzi, Bashir na Turabi walianzisha mchakato wa tamkeen (uwezeshaji). Sera hii, ambayo urithi wake bado umesalia, iliwawezesha kuwapa wafuasi wa imani ya kiislamu na wakubwa wa usalama walio tayari kushirikiana nao kudhibiti karibu kila sehemu ya maisha ya umma nchini Sudan.

Hapo awali, Bashir aliweka serikali huru, ya kiteknolojia kiutendaji, hata hivyo, mamlaka yalikuwa ni ya muungano wa kijeshi na Kiislamu ambao uliendesha nchi nyuma ya pazia.

Katika miaka ya 1990, Bashir alianza kuyasafisha bila huruma mashirika huru ya kiraia na vyama vya kisiasa vya Sudan. Kufikia mwisho wa muongo huo, alikosana na Turabi.

Alimtoa Turabi kutoka Serikalini mwaka 1999 na kuwachagua wawakilishi waliochaguliwa wa upinzani katika utawala wake katika miongo iliyofuata. Bashir alidumisha muungano wa kijeshi na Kiislamu kama msingi wa Chama chake cha National Congress. Akajisimika.

th

Kurekebisha hali ya mambo

Abdel Fattah al-Burhan

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Abdel Fattah al-Burhan

Katika miaka ya 1990, serikali ya Sudan ilikuwa mwenyeji wa Waislam wenye itikadi kali ambao walitaka kuvusha itikadi za kimapinduzi nje ya nchi na kujaribu kuangusha serikali jirani zilizochukuliwa kuwa washirika wa Magharibi.

Hata hivyo, baada ya mgawanyiko na Turabi mwaka 1999, utawala wa Bashir ulijaribu kurekebisha muonekano wake kimataifa kwa kujiweka mbali na makundi hayo ya wapiganaji. Pia ilianza kushirikiana na mashirika ya kijasusi ya Magharibi.

Katika kipindi cha baadaye cha Bashir, serikali ya Sudan iliunga mkono muungano wa Saudi-Emirati dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu wa Houthis nchini Yemen. Burhan alisimamia hilo.

Alipoibuka kama kiongozi wa kijeshi wa mpito mnamo 2019, Burhan alinufaika kutokana na dhana kwamba alikuwa mwanajeshi kitaaluma zaidi ya Muislamu.

Bashir huenda alianguka mwaka 2019, lakini maafisa wake waandamizi kijeshi wameendelea kusalia na kuendeleza misingi ya utawala wake. Mabaki haya yanaendelea kudhoofisha juhudi za mpito wa kidemokrasia nchini Sudan, na hatimaye kuendelea kuleta matokeo mabaya.