Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mipango mitano 5 muhimu kukusaidia kufikia malengo yako mwaka mpya
Na Dinah Gahamanyi
BBC News Swahili
Bila shaka kulikuwa na mafanikio, changamoto, makosa uliyoyafanya, uzoefu uliokufurahisha na uliokuza ujuzi wako, na mambo ambayo hayakukufurahisha katika mwaka huu...haya ni mambo ya kawaida ambayo hayapasi kukukatisha tamaa.
Andika mambo haya mahali ili uyatumie kuweka mkakati wako kuwa wa maana kwa ajili ya mwaka ujao.
Angalia mambo unayofaa kuyapa kipaumbele katika mipango yako ya mwaka.
Je ni mambo gani unayopaswa kuyaangalia unapoandaa mipango ya mwaka ujao? .
Angalia yale yaliyokuendeleza na yaliyokurudisha nyuma.
1. Tofautisha mipango yako ya kikazi na kibinafsi
Malengo yako ya kikazi yatakuwa ni tofauti na yale ya kibinafsi ,licha ya kwamba yanategemeana. Vinginevyo huenda usifanikiwe kwa kiasi ambacho ulikitarajia.
Malengo yako ya kikazi yatakuwa ni tofauti na yale ya kibinafsi ,licha ya kwamba yanategemeana. Vinginevyo huenda usifanikiwe kwa kiasi ambacho ulikitarajia.
End of Unaweza pia kusoma:
2. Andaa mpango kwa ajili ya mwaka mpya
Fikiria ni malengo gani hasa unayotaka kuyafikia tarehe 31 Disemba ya mwaka ujao. Kisha, panga hatua unazohitaji ili uweze kuyafikia malengo hayo.
Andika mahali shughuli muhimu au mafanikio unayotarajia kuyaona kama viashiria vya vitakavyokuwezesha kufikia mafanikio hayo.
Viashiria hivi vinaweza kuwa miradi, au ujuzi wa kitaaluma.
Pia, angalia uwezekano wa vikwazo vya mafanikio uliyoyapanga. Kama mwaka huu umetufundisha kitu fulani, hicho ndicho kitakacho kuwa mpango wa pili au wa tatu kama mambo hayatakwenda ulivyopanga.
Huenda usihitaji mipango hii mbadala.
Kuwa na mipango hii mbadala hatahivyo hutusaidia kuwa na kiasi fulani cha utulivu wa akili,huku tukijiandaa kusonga mbele na mpango wa awali.
3. Panga orodha ya mambo ambayo hautayafanya
Kupanga orodha ya mambo ambayo hautayafanya haimaanishi kuwa unaachana na mambo ambayo hutaki kuyafanya. Ni pia kuachana na mambo ambayo yanakuzuia kiutendaji kufikia malengo yako.
Kubaini mambo ambayo unapaswa kuachana nayo itakuwezesha kuwa na ufanisi zaidi katika utekelezaji wa malengo yako ya mwaka.
4: Tenga muda kwa ajili yako binafsi.
Panga muda wako binafsi wa likizo au mapumziko mapema. Kama unahisi kuwa unahitaji kwenda kutembea mahala fulani, jipange mapema na utenge kiasi cha pesa zinazoweza kukuwezesha kwenda likizo.
Mchoko na msongo wa mawazo wa kuendelea kufanya kazi bila kupumzika sio mzuri kwa afya yako binafsi, na wala kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika hakukuongezei uwezo wa ufanisi wa kikazi kwa ajili ya kufikia malengo yako.
Ni muhimu kufikiria kwa umakini afya ya mwili na akili yako, unapopanga malengo yako ya mwaka ujao.
5. Panga mradi wako wa kando ili ukuongezee kipato
Angalia kati ya mambo unayoyapenda uyatumie kama mradi wako wa kando wa kukuongezea kipato, usitegemee sana kazi unayoifanya pekee kama chanzo cha mapato yako.
Mradi wa kando hukusaidia kujifunza mbinu mpya na ujuzi ambao vinginevyo
usingeupata katika kazi yako ya kila siku, na unaweza kukunufaisha kimaisha.
Kila mara uwe na subra na furahia kila kitu unachojifunza.