Miji mitano salama zaidi kuishi duniani 2025

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 7

Wakati Vienna imeongoza orodha ya miji salama ya kuishi duniani miaka kadhaa, 2025 ilichukua taji la kwanza. Kuanzia Copenhagen hadi Melbourne, tuliwauliza wenyeji ina maanisha nini kuishi katika miji hii maarufu.

Kitengo cha Ujasusi cha Wanauchumi (EIU) kimeorodhesha miji kwa muda mrefu kote duniani, kikitoa picha inayoungwa mkono na data ya mahali ambapo maisha ni mazuri na salama kuishi. Miji iliyoorodheshwa zaidi duniani imekuwa na msimamo thabiti katika miaka michache iliyopita.

Lakini mnamo 2025, jambo moja kuu lilitikisa viwango: kwa mara ya kwanza katika miaka mitatu, Vienna iliondolewa katika nafasi ya kwanza. Copenhagen ilipanda hadi kileleni kutokana na alama bora zaidi katika uthabiti, elimu na miundombinu - vigezo vitatu vigumu kushinda.

Hata hivyo, misukosuko mikubwa zaidi mwaka wa 2025 haikuwa tu kuhusu kupanda au kushuka kwa alama - yalihusu usalama, huku mivutano ya kisiasa ikiongezeka kote duniani. Vienna, haswa, ilikumbwa na tishio la bomu ambalo lilisababisha kuahirishwa kwa tamasha la Taylor Swift la 2024 pamoja na shambulio lililopangwa hivi karibuni dhidi ya kituo cha gari moshi.

Bado, miji ya Ulaya Magharibi, Australia, New Zealand na cnada inaendelea kufanya vyema katika viwango, huku Osaka ikiwa jiji pekee la Asia lililoingia kwenye orodha ya 10 bora. Lakini je, inamaanisha nini hasa kwa jiji lako kutajwa kuwa mojawapo ya maeneo salama duniani? Wenyeji wa miji hiyo mitano wanaeleza.

1. Copenhagen

Licha ya kushikilia nafasi ya kwanza ya miji salama zaidi kuishi duniani, mji huu mkuu wa Denmark pia hivi karibuni uliorodheshwa kama jiji ambalo wakaziwake wana furaha zaidi duniani. Vigezo hivi viwili vianendana, kwani uthabiti wa hali ya juu wa Copenhagen, miundombinu na mazingira huchangia moja kwa moja furaha ya kila siku kwa wakaazi.

"Treni hufika kituoni kwa muda uliowekwa kama ni saa sita na dakika kumi na sita muda huo ukifika utaona treni imewasili. Hakuna mtu atakayekuangalia kwa mshangao ukiingia kwenye mgahawa wa kifahari ukiwa umevalia mavazi ambayo hayaendani na mazingira hayo, na pia unaweza kuogelea hata Januari ukiwa na ujasiri huo," anasema mkazi wa Copenhagen Thomas Franklin, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya fintech ya Swapped.com. "Copenhagen inanivutia kila wakati kwa utulivu wake. Mitaa ni pana, baiskeli ni nyingi kuliko magari kusema ukweli ni jiji lilonaendeshwa kwa ustadi."

Bustani ya Tivoli jijini Copenhagen

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bustani ya Tivoli jijini Copenhagen

Franklin pia anasifia mshikamano wa watu wa jiji hili. Hakuna shinikizo la kuweka mambo sawa kabla ya kukutana na rafiki. Hii inamaanisha kuwa mnaweza kukutana hata bila mipango na kunywa kahawa huku mkipiga soga kwa saa mbili. Ingawa anga mara nyingi inaweza kuwa kijivu, anasema jiji linaangazwa na masoko ya wazi, na sauti za watoto wanaokimbia kwenye bustani. "Ni jiji ambalo linajitahidi sana kufikia malengo ya wakazi wake," alisema.

Miji 10 salama zaidi kuisha 2025:

1. Copenhagen, Denmark

2. Vienna, Austria (ilishikilia nafasi sawa)

2. Zurich, Switzerland (ilishikilia nafasi sawa)

4. Melbourne, Australia

5. Geneva, Switzerland

6. Sydney, Australia

7. Osaka, Japan (ilishikilia nafasi sawa)

7. Auckland, New Zealand (ilishikilia nafasi sawa)

9. Adelaide, Australia

10. Vancouver, Canada

2. Vienna

Mji huu mkuu wa Austria huenda umeshuka kutoka nafasi ya kwanza hadi ya pili, lakini alama za huduma zake bora za afya bado iko juu kuliko mji mingine. Pia imeendelea kudumisha alama muhimu katika masuala ya elimu na miundombinu. Vigezo hivi vinaifanya kuwa mahali ambapo wakaazi wake wanajivunia kuishi.

"Mimi ni mkaazi wa New Yorker nchini Marekani alakini nilihamia Vienna takriban miaka minne iliyopita na sina mpango wa kurudi nyumbani," anasema Nataleigh O'Connell, mshauri wa masuala ya mawasiliano katika shirika la UNIDO. "Nimepata maisha bora ambayo sikuwahi kufikiria yangewezekana katika jiji kuu."

Nje kidogo ya jiji la Vienna, kuna mikahawa ya mvinyo na mitaa iliyojengwa kwa mawe ya Grinzing ambayo inaleta taswira ya maisha ya vijijini ndani ya jiji kuu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nje kidogo ya jiji la Vienna, kuna mikahawa ya mvinyo na mitaa iliyojengwa kwa mawe ya Grinzing ambayo inaleta taswira ya maisha ya vijijini ndani ya jiji kuu.

Anaonyesha uwezo wa kumudu hali ya maisha kama kichocheo kikuu, akibainisha kuwa kodi ya nyumba ni nafuu sana, na ghorofa ya katikati ya jiji yenye chumba kimoja cha kulala inagharimu chini ya €850 kwa mwezi. Mtandao mpana wa usafiri wa umma wa Vienna pia unawavutia sana wenyeji hasa kutokana na wa bei yake nafuu. Wakaazi wana weza kutumia €1 tu kwa usafiri kwa siku.

"Ni jiji ambalo hutoa kila kitu cha kutosha, iwe mikahawa mipya, maonyesho ya kiwango cha kimataifa au maonyesho ya sanaa, bila kuonekana kulemewa na shughuli hizo," alisema O'Connell. Ili kupata uzofu wa Vienna kama mwenyeji, anapendekeza kutembelea heurigen, shamba la mizabibu la ndani ya mipaka ya jiji. "Njia za kupanda mlima zinazoziunganisha zinaunyesha mandhari ya kuvutia ya jiji," alisema.

3. Geneva

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Uswizi mara kwa mara inashika nafasi ya juu kwa ubora wa maisha, hii inatokana na sera na miundombinu inayounga mkono ustawi. Miji ya Zurich na Geneva zilifanikiwa kuingia kwenye orodha ya tano bora mwaka huu, lakini wakaazi wa Geneva wanasema jiji lao lina mvuto wa kipekee - mtulivu zaidi lakini kwa manufaa ya kuwa kitovu cha kimataifa.

"Geneva ni jiji linalosimamiwa vyema katika nchi inayoendeshwa vizuri," alisema mkazi James F Royal, ambaye alihamia hapa kutoka Florida miaka kadhaa iliyopita na ni mwandishi wa kitabu Options Trading 101. "Kinaangazia faida nyingi za kuishi katika jiji hili kubwa - muziki, sanaa, biashara - katika mazingira ya utulivu, kumaanisha kupata faida nyingi za maisha ya mijini bila hofu ya kupata hasara za kawaida."

Mbali na kuwa na alama bora za afya na miundombinu, jiji hili pia ni safi, salama na rahisi kumuelekeza hata mgeni. "Iwapo unataka kutembea kwa miguu hadi unakoenda au kutotumia mfumo wa usafiri wa umma, unaweza kuzunguka kwa urahisi bila kutumia gari," Royal alisema. Zaidi ya hayo, mtandao wa treni unaotegemewa wa Uswizi na eneo la kati hurahisisha kusafiri karibu kila mahali barani Ulaya kwa saa chache tu.

Geneva inaoanisha urembo wa asili na miundombinu bora na umaridadi wa kimataifa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Geneva inaoanisha urembo wa asili na miundombinu bora na umaridadi wa kimataifa

Geneva pia ni moja ya miji ya Uswizi yenye watu wengi kutoka maeneo tofauti, na zaidi ya 40% ya wakaazi waliozaliwa nje ya nchi. "Waakazi hupata manufaa ya utofauti huo, kama vile vyakula mbalimbali na watu wenye asili ya kuvutia," Royal alisema. Uzuri wa asili wa jiji hilo - hasa Ziwa Geneva lenye umbo la mpevu na mandhari yake ya mlima - pia huongeza mvuto wa maisha ya kila siku.

4. Melbourne

Imeorodheshwa ya nne kati ya miji salama zaidi duniani, Melbourne ilipata alama kamili katika huduma ya afya na elimu. Lakini alama zake za juu katika utamaduni na mazingira ndizo zilizoiweka juu ya miji mingine ya Australia - ikiwa ni pamoja na Sydney na Adelaide, ambayo pia ilijumuishwa miongoni mwa miji 10 bora.

Melbourne pia alifanya vyema katika kigezo cha miundombinu - na wakili Oliver Morrisey anasema aliamua kuendesha shughuli zake hapo kutokana na ufanisi wa jumla ambao haupatikani katika miji mingine mikubwa.

"Ninaweza kutembea kutoka Mahakama ya Juu na kukutana na mteja karibu na Mtaa wa Collins kwa chini ya dakika 15; na ninaweza kufanya kazi wakati wa mchana kisha nikampeleka binti yangu kwa matembezi kupitia bustani ya Fitzroy baada ya shule," alisema. "Hiyo ndiyo maana halisi ya maisha kwangu. Sio tu kuhusu mtindo wa maisha. Ni kuhusu urahisi wa kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine kutekeleza majukumu muhimu bila matatizo yoyote ."

Migahawa ya Laneway, vyuo vikuu vya kiwango cha kimataifa na maeneo ya kijani kibichi husaidia kuifanya Melbourne kuwa moja ya miji bora zaidi kuishi ulimwenguni.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Migahawa ya Laneway, vyuo vikuu vya kiwango cha kimataifa na maeneo ya kijani kibichi husaidia kuifanya Melbourne kuwa moja ya miji bora zaidi kuishi ulimwenguni.

Pia anapenda mchanganyi wa kitamaduni wa wakaazi wa Melbourne, ambayo huwaleta pamoja watu wa tabaka mbalimbali na kuchochea mchanganyiko mzuri wa shughuli, matukio na vyakula. "Haichoshi, na kila mara kuna mbinu mpya ya kupanua mtazamo wako na kujaribu kitu tofauti," alisema.

Anapendekeza wageni watembee kwa mbiguu mitaa ya jiji la Melborne wajoinee michoro ya grafiti, baa za kama vile Beneath Driver Lane na Bar chini kwa chini ya Miss Gunn. Morrisey anapendekeza chakula cha mchana kwenye Mtaa wa Lygon, unaosifika kuwa utamaduni wa kubarizi jijini. "Kula polepole, ongea kwa sauti ya juu na ufanye vitu kwa wakati wako," alisema. "Hiyo ndiyo Melbourne halisi."

5. Osaka

Jiji pekee la Asia kuingia katika orodha ya 10 bora (iliyoorodheshwa ya saba kwa jumla), Osaka ilipata alama bora katika uthabiti, afya na elimu. Na ingawa mara nyingi hufunikwa na Tokyo inayong'aa, mtindo wa maisha ya Osaka ndiyo huwavutia wakazi wanaishi hapa.

"Osaka ni jiji lililostawi sana, lililotulia sana," alisema mkaazi wa muda mrefu Graham Hill ambaye anaendesha tovuti ya ukaguzi ya Osaka City. "Ni Wajapani unaweza kufananishwa na mji wa San Francisco nchini Marekani: mji mdogo, lakini wenye ladha na vionjo vya kipekee."

Miundombinu ya kutegemewa ya jiji hilo - ikiwa ni pamoja na mfumo thabiti wa usafiri - hufanya Osaka iwe rahisi kuishi, bila msongamano wa magari unaoshuhudiwa Tokyo. Hill anasema ni rahisi zaidi kupata makaazi katika maeneo ya tabaka la juu, kwa bei ni nafuu pia.

Bustani ya Utsubo katikati ya Osaka

Chanzo cha picha, Alamy

Ingawa Osaka ina vivutio vikuu vya watalii kama vile Kasri la kihistoria la Osaka, Hill inapendekeza wageni watafute starehe za kila siku za Osaka. "Kubarizi katika Mkahawa wa Streamer huko Shinsaibashi ni baadhi ya vitu vinavyoenziwa sana katika jiji hili," alisema. "Kununua vitafunio vya Utsubo Bakery Panena na kuketi katika Hifadhi ya Utsubo ni baadhi ya starehe zinazopatikana kwa urahisi kwa mwenyeji wa Osaka."

Pia unaweza kusoma:

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi