Kwanini kimondo cheusi kinaaminika kuchangia kuleta maji duniani?

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Jonathan O'Callaghan
- Nafasi, BBC Future
- Muda wa kusoma: Dakika 7
Vitu hivi vya ajabu vinaweza kueleza jinsi maji yalivyofika duniani, lakini pia vinaweza kusababisha tishio lisilojulikana hapo awali kwa sayari yetu.
Sasa, chombo cha anga kinaelekea kwenye mojawapo ili kuchunguza.
Hii ni kati ya miamba ya ajabu katika mfumo wetu wa jua.
Wao si asteroidi kabisa wala kimondo kabisa, lakini mchanganyiko wa ajabu wa hizo mbili.
Wanaitwa "kimondo cheusi" na hakuna mtu anayejua nini cha kufanya kutoka kwao.
Hata hivyo, kulingana na wanasayansi wanaozichunguza, miamba hiyo ya ajabu na mpya ya anga ya juu inaweza kuwakilisha aina mpya kabisa ya vitu katika mfumo wa jua, ambayo inaweza kusaidia kujibu maswali kuhusu asili ya maji duniani.
Wanaweza pia kusababisha tishio lisilojulikana hapo awali kwa sayari yetu.
Sasa tuna fursa ya kujifunza zaidi kuhusu vitu hivi vya ajabu kutokana na chombo cha anga za juu cha Kijapani ambacho, kinaelekea kwenye mojawapo hivi sasa.
Ikiifikia mwaka wa 2031, tunaweza kujua kwa uhakika vitu hivi ni nini na jinsi vinavyofanya kazi.
Vidokezo vya kwanza vya kuwepo kwa kimondo cheusi vilionekana mwaka wa 2016, wakati wanafalaki waligundua kile walichoamini kuwa asteroidi inayofanya kama kimondo.
Ingawa asteroidi ni vitu vya mawe ambavyo havifanyi kazi vinavyopatikana katika ukanda mpana kati ya sayari ndogo na Jupita, kimondo huundwa na mwamba na barafu na huwa na mikia mikubwa inayoenea kwa mamilioni ya kilomita.
Kawaida hutoka kwenye mfumo wa jua wa nje.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kitu kilichoonekana mnamo 2016 kilikuwa cha kushangaza sana.
Ilionekana kusonga kama kimondo, lakini haikuonyesha sifa za kawaida za moja.
Watafiti walipochunguza mzunguko wake wa kuzunguka jua, kitu hicho kilionekana kupokea msukumo wa mara kwa mara, wa ghafla kutoka kwa nguvu nyingine isipokuwa mvuto, ambayo ilibadilisha mwendo wake kidogo sana.
Ingawa harakati hizi zilikuwa ndogo, kwa mpangilio wa sehemu chache za mita kwa sekunde, zilionekana vya kutosha wakati zilizingatiwa kupitia darubini kutoka duniani.
Aina hii ya "kuongeza kasi isiyo ya mvuto" ni ya kawaida kwa kimondo, ambayo barafu yake huwaka kwa kasi inapokaribia jua, na kusababisha kutolewa kwa gesi na vumbi ambalo hufanya kama kusogeza mbele.
Kwa upande wa kitu kilichoonekana mwaka wa 2016, hata hivyo, hapakuwa na njia inayoonekana ya vumbi au barafu, na kitu kilionekana kisicho na hewa.
Mwaka mmoja baadaye, wanafalaki waliona kitu kingine kikiwa na tabia kama hiyo: kipande cha mawe, chuma na barafu chenye umbo la sigara, kati ya urefu wa mita 115 na 400, ambacho kiliitwa 'Oumuamua.
Baadaye iligeuka kuwa moja ya vitu vya kwanza vinavyojulikana vya anaga baina ya nyota kutembelea mfumo wetu wa jua.
Mwamba ulizunguka jua letu kabla ya kurudi kwenye nafasi ya nyota.

Chanzo cha picha, ESO/M Kornmesser
Kisha, mwaka wa 2023, timu ya wanafalaki wakiongozwa na mwanafalaki Darryl Seligman wa Chuo Kikuu cha Jimbo la Michigan nchini Marekani walitangaza kwamba wamegundua vitu sita vinavyofanana vinavyozunguka jua letu, katika mizunguko inayofanana na asteroidi, isiyo na mikia ya kupendeza lakini ikipitia kasi isiyo ya kawaida.
Nyota hao wa giza, wote kati ya mita 4 (13 ft) na 32 m (104 ft) upana, walikuwa wakipata kasi ya hadi nanometa moja kwa sekunde-kiasi kidogo, lakini kutosha kuwaondoa kwenye njia zao kwa kilomita mia kadhaa kila baada ya miaka michache.
Takriban wakati huo huo, Seligman na wenzake walichapisha utafiti unaoonyesha kwamba asteroidi ya karibu na dunia, iitwayo 2003 RM na yenye upana wa mita 300 , pia ilikuwa na tabia kama kimondo cheusi.
Mnamo Desemba 2024, walichapisha karatasi mpya iliyo na habari juu ya vitu vingine kama hivyo, na kuleta jumla ya vitu vinavyojulikana katika mfumo wa jua hadi 14.
Hata hivyo, sababu ya harakati zao zisizo na uhakika bado ni siri.
"Bado hatujui ni nini husababisha," Seligman anasema.
Aina mpya ya miamba

Chanzo cha picha, ESA/ Rosetta/ NAVCAM
Wanafalaki wanaamini kwamba asilimia kubwa ya asteroidi na kimondo ni mabaki ya kipindi cha awali cha uundaji wa sayari katika mfumo wa jua, takribani miaka bilioni 4.6 iliyopita.
Baadhi ya asteroidi ni vipande vya vitu ambavyo havikuungana kabisa kuunda sayari, ilhali kimondo hutokana na mgando wa barafu na vumbi kutoka maeneo ya mbali na jua.
Kwa kawaida, wataalamu hugawanya miili hii ya angani katika makundi mawili:
asteroidi zisizo na shughuli na kimondo zenye misukosuko, ambazo barafu yake huyeyuka moja kwa moja kutoka hali ya barafu hadi gesi, na kutupa vitu angani vinavyounda mikia yao ya kuvutia.
Uwepo wa kimondo cheusi inaashiria kwamba si rahisi kila wakati kutofautisha kwa wazi kati ya aina hizi mbili za miili ya angani.
"Hii ni sehemu ya taswira inayoibuka ya asteroidi na kimondo kama mwendelezo mmoja," anasema Michele Bannister, mwanafalaki kutoka Chuo Kikuu cha Canterbury, New Zealand.
"Kihistoria, kimondo hujulikana kwa kuwa na mkia wa kuvutia sana, ilhali asteroidi ni mwamba mkavu kabisa. Taswira hiyo sasa haipo tena."
Urahisi wa mfumo wa kugawanya kati ya asteroidi na kimondo ulianza kutiliwa shaka tangu mwaka 1996, baada ya kugunduliwa kwa asteroidi hai, aina ya asteroidi inayotoa vitu kutoka katika uso wake na kutengeneza mkia unaofanana na wa kimondo.
"Shughuli" hiyo huenda inasababishwa na barafu iliyoko chini ya uso wa asteroidi kufichuka baada ya kugongana na asteroidi nyingine, au asteroidi kujizungusha kwa kasi kiasi cha kujipasua.
Mara barafu hiyo inapofichuka, joto la jua huiyeyusha na kusababisha vitu kurushwa nje, na hivyo kufanya asteroidi iwe "hai."
"Baadhi yao huonyesha tabia kama za kimondo," anasema Jessica Agarwal, mwanaafalaki kutoka Taasisi ya Max Planck ya Utafiti wa mfumo wa jua nchini Ujerumani, ambaye amekuwa akisomea asteroidi hai kwa miaka mingi.
Hata hivyo, kimondo cheusi ni tofauti.
Tofauti na asteroidi hai, hazionyeshi dalili yoyote ya kutoa vitu kutoka kwenye uso wake, lakini zinaonekana wazi kuwa na kasi ya mwendo wa aina ya kimondo.
Kasi hiyo pia inaaminika kuwa kubwa mno kiasi kwamba haiwezi kuelezewa na joto linalotolewa, ambalo linaweza kuzifanya zijizungushe kwa kasi zaidi mchakato unaoitwa athari ya Yarkovsky.
"Tunaona zinapotea kwa kasi zaidi kuliko inavyotarajiwa kutokana na athari ya Yarkovsky," anafafanua Teddy Kareta, mwanafalaki katika kituo cha angani cha Lowell huko Arizona.
Ili kuelewa vizuri zaidi kimondo cheusi, itatulazimu kuzifikia kwa ukaribu.
Lakini kwa bahati nzuri, tukio la ajabu linatupa nafasi hiyo katika kipindi cha miaka sita ijayo
Fursa ya kuizuru

Chanzo cha picha, Alamy
Mnamo Desemba 2020, chombo cha angani cha Kijapani Hayabusa2 kilirudi duniani kikiwa na sampuli kutoka asteroidi Ryugu, zilizotoa taarifa muhimu kuhusu chanzo cha maji na uhai duniani.
Baada ya mafanikio hayo, shirika la anga la Japan (JAXA) kilituma chombo hicho katika misheni ya ziada kuelekea kwenye sayari ndogo 1998 KY26.
Kwa mshangao, iligundulika kuwa 1998 KY26 ni miongoni mwa kimondo cheusi miili ya angani isiyo na mkia unaoonekana, lakini inasafiri kwa kasi isiyoeleweka kirahisi.
Kimondo hiki ni tofauti na asteroidi au kimondo za kawaida, na huenda zinahusiana na historia ya maji duniani.
"Hatukujua kuhusu kimondo cheusi tulipopanga misheni hii ya ziada. Ni jambo la kusisimua sana." asema Yuichi Tsuda, Msimamizi wa Mradi wa Hayabusa2, JAXA
Chombo cha Hayabusa2 kinatarajiwa kufika kwenye 1998 KY26 mwaka 2031, ambapo kitapiga picha, kuchunguza kama kuna barafu inayoyeyuka, na huenda kikatua juu ya asteroidi hiyo.
Lengo ni kuelewa muundo wa ndani na tabia ya kimondo hizi zisizoeleweka vizuri.
Wakati huo huo, wanafalaki wanatarajia kutumia darubini kubwa kama JWST na Lowell Discovery Telescope kuendelea kuzifuatilia.
Hii inaweza kusaidia kuelewa kasi zisizo za kawaida na kuchunguza iwapo kimondo hizi zimesaidia kuleta maji duniani au zinaweza kuwa tishio kisayansi kwa baadaye.
"Kama sababu ya kasi hiyo ni utoaji gesi kama wa kimondo, Hayabusa2 itaiona bila shaka." asema Darryl Seligman, mwanafalaki.
Aina mbili za kimondo cheusi

Chanzo cha picha, Alamy/ Nasa
Mnamo Desemba 2024, wanasayansi waligundua kuwa kimondo cheusi huweza kuwepo katika aina mbili:
Kimondo cheusi cha nje- zina ukubwa wa mita 100 hadi kilomita 1, na zinatoka katika maeneo ya mbali karibu na Mshtarii.
Kimondo cheusi cha ndani – ndogo zaidi (mita 10–20), zenye mzunguko unaofanana na wa dunia, na huenda ni asteroidi zilizopasuka na kufichua barafu iliyofichwa ndani.
Kimondo hiki huenda ni mabaki ya kimondo "zinazokufa" zikiwa zinamaliza gesi ya mwisho ya uhai wake wa anga.
"Tunaziangalia wakati zinakaribia kumaliza gesi yao ikiwa ni pumzi zao za mwisho kama kimondo," anasema Teddy Kareta.
Ugunduzi huu unaweza kusaidia kuelewa jinsi maji yalivyofika duniani.
Kimondo cheusi kinaaminika kuwa chanzo kinachowezekana cha maji duniani.
"Iwapo kuna miili mingi karibu na dunia ambayo hatukujua ilikuwa na unyevu, huenda ilichangia kuleta maji duniani," asema Seligman.
Kimondo hizi pia zinaweza kuwa tishio la baadaye kwa dunia, kwani zinaweza kuonekana kuwa salama lakini kwa ghafla zikabadili mwelekeo na kuelekea duniani.
"Unaweza kuona ni salama mara ghafla kikagonga dunia wakati hatukutarajia kabisa," anaonya Taylor.
Kwa sasa, kimondo nyeusi ni nadra na mabadiliko yao ya mwelekeo ni madogo, lakini bado ni muhimu kuzifuatilia kwa makini.
"Kama hatuwezi kuzitambua ipasavyo, hatutajua kama zitagonga dunia au la," Taylor anasisitiza.
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid












