Kwa nini Uswidi ilijaribu kutengeneza bomu la atomiki kisiri?

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika miaka ya baada ya Vita vya Dunia vya pili, Uswidi, taifa ambalo limekuwa na msimamo wa wastani na kuunga mkono amani liliandaa programu kujenga bomu la atomiki.
Uswidi haijashiriki katika vita vyovyote tangu 1814. Lakini baada ya kumalizika kwa Vita vya dunia vya pili, nchi hii ya zamani ya Kaskazini mwa Ulaya ambayo ilikuwa na msimamo wa wastani ilianzisha mpango wa zaidi wa miaka 20 wa kulihami jeshi lake na bomu la atomiki.
Baada ya mijadala mirefu kwenye uwanja wa umma, hatimaye mnamo 1968, serikali iliamua kusitisha mpango huu.
Kwa njia hii, Uswidi, pamoja na Uswizi, Ukraine na Afrika Kusini, waliunda kundi la kipekee la nchi ambazo zimeacha mipango yao ya silaha za nyuklia na kuonyesha ulimwengu kwamba upokonyaji wa silaha za nyuklia unawezekana.
Ukubwa wa shughuli za nyuklia za Uswidi haukuwafurahisha wanasiasa ambao walitaka kurejesha sura ya nchi yao katika uwanja wa kupiga marufuku silaha za nyuklia.
Lakini hatimaye, mwaka wa 1985, mwandishi wa habari anayeitwa Krister Larson alifichua ukweli kuhusu mpango huu wa nyuklia, na Uswidi ikalazimika kukubali historia yake iliyofichwa katika uwanja wa silaha za nyuklia.
Kufichwa kwa mapambano ya kuweka nyuma ya pazia rekodi za programu hii kulizidisha mashaka kwamba huenda hata sasa Sweden inaweza kuwa na mpango wa siri kabisa wa kupata silaha za nyuklia.
Na sasa, miongo kadhaa baadaye, baada ya miaka 200 ya kutoegemea upande wowote katika vita, na baada ya uvamizi wa hivi karibuni wa Urusi na kuikalia Ukraine, Uswidi inajiunga na NATO, ambayo baadhi ya wanachama wake wana silaha za nyuklia.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kwa nini Uswidi ilitaka kupata silaha za nyuklia hapo kwanza? Na kwa nini aliacha kujaribu baadaye?
Huko Orsvik, kitongoji tulivu nje kidogo ya Stockholm, kuna shule ambayo jengo lake kubwa linaonekana zaidi kama taasisi ya siri ya utafiti.
Kwa kweli, sio suala lisilo la msingi, kwa sababu mara moja lilitumiwa kwa kazi hiyo. Haya yalikuwa makao makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Ulinzi wa Kitaifa wa Uswidi; Moja ya mabaki machache yaliyosalia ya mpango wa silaha za nyuklia wa Uswidi.
Mnamo 1945, wiki mbili baada ya picha za kutisha za miji iliyoharibiwa ya Hiroshima na Nagasaki kufika Uswidi, kamanda mkuu wa nchi hiyo aliyejitegemea sana aliuliza wakala mpya wa ulinzi ulioanzishwa hivi karibuni kutoa ripoti ya siri juu ya uwezo wa nchi hiyo wa kutengeneza mabomu.
Kwa hakika, inaweza kusemwa kwamba Uswidi ilikuwa nchi isiyofungamana na upande wowote, lakini viongozi wake waliamini kutoegemea upande wowote huku wakiwa na silaha - kuliwezekana tu kwa msaada wa jeshi lenye nguvu - na uelewa wa viongozi wa nchi ulikuwa kwamba katika siku zijazo, ili kudumisha kutoegemea upande wowote kwa nchi yao, inawezekana Bomu la atomiki lingehitajika wakati wa vita.
Idadi yao ndogo ya watu na mipaka mirefu ya maji iliwafanya waonekane kama "mawindo rahisi" kwa wapinzani wao, kama vile jirani yao, Muungano wa Sovieti.
Nchi hii ya Scandinavia pia ilikuwa na migodi ya uranium, ingawa uranium ya ubora wa chini. Pia, kutokana na kutoegemea upande wowote katika Vita vya dunia vya pili, ilikuwa nchi yenye ustawi na miundombinu yenye afya.
Baada ya kusema hivyo, wazo la kutengeneza bomu la atomiki, tofauti na leo, halikuwa mbali sana.
Miaka mitatu baada ya milipuko ya mabomu ya atomiki ya Hiroshima na Nagasaki, mnamo 1948, taasisi hii ilizindua "laini ya uzalishaji ya Uswidi" kwa msaada ambao Uswidi, bila msaada wa nchi zingine, inaweza kutengeneza bomu ya atomi ya plutonium peke yake.
Mpango wao ulikuwa kupata plutonium katika vinu vya nyuklia vya Uswidi kwa kuchanganya nyuklia wa uranium ya Uswidi na maji mazito.
Hawakuwa na upatikanaji wa vyanzo vya ubora wa juu wa urani, wala ujuzi wa nyuklia wa Wamarekani, hivyo wanasayansi wa Uswidi, kwa siri walipaswa kuanza mchakato mzima kutoka mwanzo.
Pia iliamuliwa kwa nguvu kuendeleza mpango wa silaha za nyuklia chini ya bendera ya kiraia na kuficha asili yake halisi.
Thomas Younter ndiye mwandishi wa kitabu "Suluhisho la Kuzuia Uenezaji wa Nyuklia: Mpango wa Uswidi wa Silaha za Nyuklia katika Miaka ya Vita Baridi". "Katika miaka hiyo, kila kitu kilikuwa tayari kupata plutonium yenye usafi unaohitajika kwa matumizi ya silaha," anasema.
Mpango wa Uswidi ulijumuisha vinu viwili. "Moja ilikuwa mtambo wa maji unaoitwa Augusta, ulio kusini mwa Stockholm, na mwingine, unaoitwa Marviken, ulijengwa nje ya Norrkoping lakini haukuwahi kuzalisha" anasema Yunter. "Wazo kuu lilikuwa kujenga silaha 100 za kimkakati."
"Tulijua hatua za ujenzi kwa uangalifu. "Tulikuwa na kila kitu isipokuwa vifaa vya kuchakata na pia mifumo ya kubeba silaha

Chanzo cha picha, Getty Images
Na mipango ya polepole ya ujenzi wa mpango huo wa silaha ndiyo sababu iliyosababisha kushindwa kwake.
Programu hizi za silaha hazikuwahi kukosolewa kwenye umma, kwa sababu rahisi kwamba, isipokuwa kwa idadi ndogo ya wanasiasa na makamanda wakuu wa jeshi na, wapelelezi wa Urusi.
Hakuna aliyejua kuhusu programu hizi. Lakini ufichaji huu uliisha mwaka wa 1954, wakati Kamanda Mkuu wa Uswidi Nils Swedenlund alipothibitisha kuwepo kwa mpango huo wa silaha, akisema kwamba silaha hizo zilihitajika haraka ili kukabiliana na uwezekano wa mashambulizi ya Soviet.
Mnamo Aprili 1957, CIA ilikadiria kuwa "programu ya kinu ya Uswidi iko katika hatua ambayo itaweza kutoa silaha za atomiki ndani ya miaka mitano ijayo." Haikupita muda wakapunguza makadirio haya hadi miaka minne.
Waziri Mkuu wa Uswidi wakati huo Tage Ölands, ambaye alifunzwa katika fizikia, mara kwa mara alifanya majadiliano kuhusu bomu la atomiki na wanafizikia mashuhuri duniani, akiwemo mshindi wa Tuzo ya Nobel Niels Bohr. Niels Bohr ni mwanafizikia yuleyule wa Denmark ambaye alichukua jukumu muhimu katika kuendeleza ujuzi wa fizikia ya nyuklia.
Baada ya kukaliwa kwa Denmark na Ujerumani, alikimbilia Marekani kwa siri na kujiunga na Mradi wa Manhattan, mradi ambao ulipeleka kuundwa kwa bomu la kwanza la atomiki duniani.
Kadiri Waziri Mkuu alivyokuwa akizungumza na wanafizikia hao, ndivyo alivyokuwa akisitasita zaidi katika kuunga mkono mpango wa silaha za atomiki, na hatimaye, katika kutafuta mwafaka wa kina, aliahirisha uamuzi wa mwisho mara kadhaa hadi matokeo ya mazungumzo ya udhibiti wa silaha ambayo yalikuwa yakiendela kati ya Usovieti na Marekani yalipotimia.
Msimamo wa waziri mkuu - au hatua ya busara ya kisiasa, kulingana na neno la nani unaamini - iliweka wakosoaji wa mpango wa silaha za nyuklia katika uangalizi.
Wengi wa wakosoaji hawa walikuwa wanawake waliokuwa katika Shirikisho la Kidemokrasia ya Kijamii, linaloongozwa na Inga Thorson, "lililokuwa mpinzani mkubwa wa silaha za nyuklia," Yunter anasema.
Lakini Rosengren, ambaye ni mtafiti wa mahusiano ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Stockholm, anasema, "Wanawake walikuwa miongoni mwa wapinzani wa kwanza wa mpango huu na waliamini kwa sababu nyingi kwamba Uswidi haipaswi kutafuta silaha za nyuklia.
Haiwezekani kwamba kuwa na silaha kama utasaidia taifa hilo kujilinda bali pia kuwa shabaha, mwishowe, badala ya kuongeza usalama wa nchi, silaha hizo zitapunguza usalama.
"Pia walisema kwamba hasara na matokeo ya kibinadamu ya silaha za nyuklia ni kubwa sana kwamba matumizi yake hayakuwa ya kimaadili.
Kwa hivyo, nchi inayopenda amani kama Uswidi haikupaswa kamwe kuwa sababu ya mateso ya kusikitisha kwa wanadamu.
Inaendelea kutafsiriwa na Seif Abdalla












