Fahamu siri ya kushiriki mazoezi ya kunyanyua uzani

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanamke akifanya mazoezi ya kunyanyua uzani

Shughuli zinazoimarisha misuli - kama vile kunyanyua vitu vizito - zinapaswa kuwa sehemu ya mazoezi ya kila wiki ya mtu mzima, utafiti unapendekeza.

Watu wanaofanya mazoezi ya aerobic na misuli wana uwezekano mkubwa wa kuishi muda mrefu zaidi kuliko wale ambao walifanya moja kati yazo, watafiti wa Marekani waligundua.

Lakini sio lazima kwenda kwenye mazoezi - kubeba mifuko mizito ya ununuzi, na kuchimba bustani zote zinahesabu.

Aina zote za mazoezi zinapendekezwa.

NHS inawashauri watu wazima wenye zaidi ya umri wa miaka 65 kufanya maoezi ya viungo kila siku ili kuimarisha nguvu.

 Inapendekeza takriban dakika 150 ya kufanya mazoezi kwa wiki au dakika 75 za mazoezi makali iwapo tayari umekuwa ukifanya mazoezi.

Masuala ya misuli

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kuongeza mapigo ya moyo mara kwa mara kunawafanya watu kuwa na afya bora, na kusaidia kurefusha maisha yao.

Lakini kuna ufahamu mdogo unaojulikana juu ya athari za kunyanyua uzani au mazoezi ya kuimarisha misuli kuhusu ni muda gani watu wanaweza kuishi.

Utafiti huo wa Marekani, uliochapishwa katika Jarida la British Journal of Sports Medicine, uliwauliza zaidi ya watu 150,000 wenye umri wa miaka 60 na 70 kuhusu utaratibu wao wa kufanya mazoezi kisha ukawafuatilia.

Watafiti waligundua kuwa watu waliotumia dakika 150 za mazoezi ya wastani kwa wiki waliishi muda mrefu zaidi kuliko wale ambao hawakufanya - lakini wale ambao walichanganya mazoezi ya kawaida ya aerobic na shughuli za kuimarisha misuli mara moja au mbili kwa wiki walifanya vizuri zaidi.

Walikuwa na hatari ya chini ya 47% ya kufa kutokana na sababu yoyote, mbali na saratani, katika kipindi cha miaka tisa ijayo – ikilinganishwa na wale ambao hawajihusishi na mazoezi kabisa .

Kufanya mazoezi ya kunyanyua uzani peke yako kunapunguza hatari kwa hadi 9-22% na mazoezi ya aerobic kwa 24-34%.

Mifano ya mazoezi ya aerobic, ambayo hufanya moyo na mapafu kusukuma damu kwa kasi , ni pamoja na kutembea haraka, kukimbia, kuendesha baiskeli na kuogelea.

Utafiti huo pia uligundua kwamba wanawake pia walifaidika zaidi kwa kufanya mazoezi ya kunyanyua uzani zaidi ya wanaume.

Kundi la watafiti , kutoka taasisi ya kitaifa ya Saratani mjini Maryland na Chuo kikuu cha Iowa, walielezea kwamba mazoezi ya kuimarisha misuli yanaweza kufanya mwili kuwa mwembamba na mifupi kuwa na nguvu na hivyobasi kuishi Maisha ya afya katika miaka ya uzeeni.

‘’Ugunduzi wetu kwamba hatari ya kuaga inaonekana kuwa kidogo kwa wale walioshiriki katika aina zote za mazoezi unaunga mkono mapendekezo ya kushiriki katika mazoezi ya aerobic na kuimarisha misuli’’ , alisema mwanzilishi wa utafiti huo Dkt Jessica Gorzelitz.

"Wazee wanaweza kufaidika kwa kuongeza mazoezi ya kunyanyua uzani kwenye mazoea yao ya mazoezi ya mwili."