Nalanda:Fahamu Chuo Kikuu ambacho kilibadilisha ulimwengu

.

Chanzo cha picha, Tahir Ansari/Alamy

Zaidi ya miaka 500 kabla ya Chuo Kikuu cha Oxford kuanzishwa, Chuo Kikuu cha Nalanda cha India kilikuwa na vitabu milioni tisa na kilivutia wanafunzi 10,000 kutoka kote ulimwenguni.

Gari letu lilipita magari ya kukokotwa na farasi, njia ya usafiri ambayo bado ni maarufu katika maeneo ya mashambani ya jimbo la Bihar, mashariki mwa India.

Baada ya kukaa usiku mmoja katika mji wa Bodhgaya, makazi ya kale ambako Bwana Buddha anasemekana kupata nuru, nilianza asubuhi hiyo kuelekea Nalanda, ambayo magofu yake ya matofali mekundu ndio yaliyosalia kama mojawapo ya mabaki ya kituo kikubwa zaidi cha masomo katika ulimwengu wa kale.

Ilianzishwa mwaka wa 427 CE, Nalanda inachukuliwa kuwa chuo kikuu cha kwanza cha makazi duniani, aina ya taasisi ya enzi ya kati ya Ivy League iliyo na vitabu milioni tisa ambavyo vilivutia wanafunzi 10,000 kutoka kote Asia ya Mashariki na Kati.

Walikusanyika hapa ili kujifunza udaktari, mantiki, hisabati na – zaidi ya yote – kanuni za Kibuddha kutoka kwa baadhi ya wasomi walioheshimika zaidi enzi hizo.

Kama Dalai Lama alivyowahi kusema: "Chanzo cha maarifa yote [ya Kibudha] tuliyo nayo, yametoka Nalanda."

.

Chanzo cha picha, BROKER/Alamy

Maelezo ya picha, Wanafunzi elfu kumi kutoka kote Asia walikuja Nalanda kujifunza kanuni za Kibudha kutoka kwa baadhi ya wasomi wa enzi hiyo walioheshimika.

Katika zaidi ya karne saba ambazo Nalanda alistawi, hakukuwa na kitu kingine kama hicho ulimwenguni.

Chuo kikuu cha kimonaki kilitangulia Chuo Kikuu cha Oxford na chuo kikuu kongwe zaidi cha Uropa, Bologna, kwa zaidi ya miaka 500.

Zaidi ya hayo, mbinu iliyoelimika ya Nalanda ya falsafa na dini ilisaidia kuunda utamaduni wa Asia muda mrefu baada ya chuo kikuu kukoma kuwapo.

Jambo la kufurahisha ni kwamba wafalme wa Milki ya Gupta iliyoanzisha chuo kikuu cha kimonaki cha Wabuddha walikuwa Wahindu waaminifu, lakini wenye huruma na kukubali Ubuddha na hamasa ya kiakili ya Kibuddha na maandishi ya falsafa yaliyoongezeka ya wakati huo.

Mfumo wa kale wa matibabu wa Kihindi wa Ayurveda, ambao umekita mizizi katika mbinu za uponyaji za asili, ulifundishwa sana huko Nalanda na kisha kuhamia sehemu nyingine za India kupitia wanafunzi wa zamani.

.

Chanzo cha picha, Mithun Pramanik/BBC Reel

Maelezo ya picha, Kurudi kwa chuo kikuu kongwe zaidi duniani
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Lakini labda urithi wa kina zaidi na unaoendelea wa Nalanda ni mafanikio yake katika hisabati na unajimu.

Aryabhata, anayechukuliwa kuwa bingwa wa hisabati ya Kihindi, anakisiwa kuwa aliongoza chuo kikuu katika Karne ya 6 BK.

"Tunaamini kwamba Aryabhata alikuwa wa kwanza kubaini sifuri kama tarakimu, dhana ya kimapinduzi, ambayo imerahisisha hesabu za hisabati na kusaidia kutoa njia ngumu zaidi kama vile algebra na calculus," Anuradha Mitra, profesa wa hisabati wa Kolkata alisema.

"Bila sifuri, hatungekuwa na kompyuta," aliongeza. "Pia alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza katika kuvumbua hesabu za ‘’square na cubic roots, mambo ya trigonometrical hadi utumiaji wa seti.

mizizi ya mraba na ujazo, na matumizi ya utendaji wa trigonometrical kwa jiometri ya duara. Pia alikuwa wa kwanza kuhusisha mng'ao wa mwezi na mwanga wa jua."

Kazi hii ingeathiri sana maendeleo ya hisabati na unajimu kusini mwa India na kote kwenye Rasi ya Arabia.

Chuo kikuu kilituma mara kwa mara baadhi ya wasomi na maprofesa wake bora katika maeneo kama Uchina, Korea, Japan, Indonesia na Sri Lanka ili kueneza mafundisho na falsafa ya Kibuddha.

.

Chanzo cha picha, Dinodia Photos/Alamy)

Maelezo ya picha, Eneo lililochapishwa na Unesco lipo katika hekta 23, lakini kuna uwezekano ni sehemu tu ya chuo asili.

Lakini labda urithi wa kina zaidi na unaoendelea wa Nalanda ni mafanikio yake katika hisabati na unajimu.

Aryabhata, anayechukuliwa kuwa bingwa wa hisabati ya Kihindi, anakisiwa kuwa aliongoza chuo kikuu katika Karne ya 6 BK.

"Tunaamini kwamba Aryabhata alikuwa wa kwanza kubaini sifuri kama tarakimu, dhana ya kimapinduzi, ambayo imerahisisha hesabu za hisabati na kusaidia kutoa njia ngumu zaidi kama vile algebra na calculus," Anuradha Mitra, profesa wa hisabati wa Kolkata alisema.

"Bila sifuri, hatungekuwa na kompyuta," aliongeza. "Pia alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza katika kuvumbua hesabu za ‘’square na cubic roots, mambo ya trigonometrical hadi utumiaji wa seti.

mizizi ya mraba na ujazo, na matumizi ya utendaji wa trigonometrical kwa jiometri ya duara. Pia alikuwa wa kwanza kuhusisha mng'ao wa mwezi na mwanga wa jua."

Kazi hii ingeathiri sana maendeleo ya hisabati na unajimu kusini mwa India na kote kwenye Rasi ya Arabia.

Chuo kikuu kilituma mara kwa mara baadhi ya wasomi na maprofesa wake bora katika maeneo kama Uchina, Korea, Japan, Indonesia na Sri Lanka ili kueneza mafundisho na falsafa ya Kibuddha kote Asia.

.

Chanzo cha picha, REY Pictures/Alamy

Mabaki ya kiakiolojia ya Nalanda sasa ni eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO.

Katika miaka ya 1190, chuo kikuu hicho kiliharibiwa na kikosi cha wavamizi kilichoongozwa na jenerali wa kijeshi wa Turko-Afghan Bakhtiyar Khilji, ambaye alitaka kufunga kituo cha maarifa cha Wabuddha wakati wa ushindi wake wa kaskazini na mashariki mwa India.

Chuo hicho kilikuwa kikubwa sana hivi kwamba moto uliowashwa na mshambuliaji ulisemekana kuwaka kwa miezi mitatu.

Leo, eneo la hekta 23 lililochimbwa huenda ni sehemu tu ya chuo kikuu cha awali, lakini kutembea kupitia wingi wa vyumba vya watawa na mahekalu kunaibua hisia ya jinsi ilivyokuwa katika eneo hili la simulizi ya kihostoria.

Nilizunguka kwenye ukumbi wa nyumba za watawa na vyumba vya madhabahu ya mahekalu.

Baada ya kuteleza kwenye ushoroba wenye kuta ndefu za matofali mekundu, nilifika kwenye ua wa ndani wa nyumba vya watawa.

Nafasi ya pango, ya mstatili ilitawaliwa na jukwaa la mawe lililoinuliwa.

"Hili lilikuwa jumba la mihadhara ambalo lingeweza kuchukua wanafunzi 300. Na jukwaa lilikuwa jukwaa la mwalimu," alisema Kamla Singh, kiongozi wangu wa ndani, ambaye alinitembeza karibu na kwenye mabaki.

Niliingia kwenye chumba kimojawapo kidogo kilichokuwa kwenye ua walipokuwa wakiishi wanafunzi kutoka mbali sana kama Afghanistan.

Vyumba viwili vya kulala vilivyotazamana vilikusudiwa kuweka taa za mafuta na vitu vya kibinafsi, na Singh akaeleza kwamba shimo dogo, lenye umbo la mraba karibu na mlango wa seli lilitumika kama sanduku la barua la kibinafsi la kila mwanafunzi.

Kama vyuo vikuu vya kisasa vya wasomi, uandikishaji ulikuwa mgumu.

Wanafunzi wanaotarajia kujiunga walihitaji kushiriki katika mahojiano makali ya moja kwa moja na maprofesa wakuu wa Nalanda.

Wale ambao walipata bahati walifundishwa na kikundi cha maprofesa kutoka pembe tofauti za India na kuendeshwa kwa pamoja chini ya mabwana wa Kibudha walioheshimika zaidi wa enzi hiyo.

Nakala milioni tisa za maktaba hiyo zilizoandikwa kwa mkono na za majani ya mitende zilikuwa hazina tajiri zaidi ya hekima ya Kibuddha ulimwenguni, na moja kati ya majengo yake matatu ya maktaba ilielezewa na mwanazuoni wa Kibuddha wa Tibet Taranatha kama jengo la orofa tisa "linapanda mawingu".

Ni chache tu za majani ya mitende na karatasi za mbao zilizopakwa rangi zilizonusurika moto - zilizobebwa na watawa waliokimbia kuokoa vilivyomo katika chuo hicho.

Sasa vinaweza kupatikana katika Makumbusho ya Sanaa ya Kaunti ya Los Angeles nchini Marekani na Makumbusho ya Yarlung huko Tibet.

.

Chanzo cha picha, Sugato Mukherjee

Maelezo ya picha, Mabaki ya Nalanda yanasalia kuwa mahali muhimu pa kuhiji na kutafakari kwa Wabudha

"Ni vigumu kutaja sababu dhahiri ya chuo hicho kuvamiwa," alisema Shankar Sharma, mkurugenzi wa jumba la makumbusho, ambalo linaonyesha vitu vya sanaa 350 vya kale zaidi ya 13,000 ambavyo vilihifadhiwa baada ya kuokolewa wakati wa uchimbaji katika chuo Nalanda. Vitu hivyo ni kama sanamu za shaba za Buddha, na vipande vya pembe za ndovu na mifupa.

"Haikuwa shambulio la kwanza kwa Nalanda," Sharma alisema, tulipokuwa tukipita kwenye magofu. "Ilishambuliwa na wahuni chini ya Mihirkula katika Karne ya 5, na tena ilipata uharibifu mkubwa kutokana na uvamizi wa mfalme wa Gauda wa Bengal, katika Karne ya 8."

Katika kipindi cha karne sita zilizofuata, Nalanda iliporomoka taratibu mabaki yake kuzikwa, kabla ya "kugunduliwa" na mtafiti wa Uskoti Francis Buchanan-Hamilton mnamo 1812, na baadaye kutambuliwa kama Chuo Kikuu cha zamani cha Nalanda na Sir Alexander Cunningham mnamo 1861.