Shambulio la Sevastopol: Fahamu jinsi ndege zisizo na rubani za Ukraine zilivyoshambulia Meli za Urusi

Eneo la chini la meli za kijeshi za Urusi zilizopo katika bahari nyeusi katika Ghuba ya Sevastopol zilishambuliwa na kundi la ndege zisio na rubani baharini na angani asubuhi ya Oktoba 29. Operesheni hiyo kubwa ilifanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya dunia. Moscow ililaumu Ukraine na Uingereza kwa shambulio hilo.

Kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Urusi, meli katika ghuba hiyo zilishambuliwa na ndege zisio na rubani baharini. Jeshi la Urusi lilihesabu kulikuwa na ndege 9 za kwanza, na nyengine 7 za pili.

Hatahivyo Wizara ya Urusi ina hakika kwamba "shambulio la kigaidi" lilipangwa na vikosi maalum vya Ukraine chini ya uongozi wa Uingereza. Lakini inaonekana kwamba vikosi vya usalama vya Urusi viliweza kuzuia shambulio hilo na ni meli moja tu "iliyoharibiwa vibaya".

Kulingana na mahesabu ya wataalam wa kijeshi, meli 3 au 4 za meli hizo za Bahari Nyeusi, hasa ile ya "Admiral Makarov", zingeweza kuathiriwa.

Operesheni hii ikawa sababu ya Kremlin kutangaza kusimamishwa kwa ushiriki wake katika "mkataba wa nafaka".

Uingereza ilikanusha shtaka hilo, Ukraine haikuchukua jukumu la shambulio hilo, lakini haikukanusha moja kwa moja taarifa za Moscow.

Je Urusi inasemaje

Kulingana na toleo la Kirusi la matukio hayo, Jumamosi, Oktoba 29, saa 4:20 asubuhi, ndege zisizo na rubani za angani zilianza kushambulia meli na vyombo vya kiraia vilivyokuwa kwenye kambi ya kijeshi ya Sevastopol.

Urusi inasema ndege zote zisizo na rubani UAV zilishambuliwa na risasi kutoka kwa meli hizo za Urusi kupitia silaha za majini na angani (helikopta).

Urusi pia ilisema kwamba ilimpata shujaa ambaye aliokoa meli hizo kwa jina Artem Zhiltsov.

Kulingana na taarifa ya Wizara ya Ulinzi, Shujaa huyo alikuwa wa kwanza kugundua ndege isiyo na rubani ya baharini ikielekea kwenye bandari ya Sevastopol usiku. Hii ilisaidia kuzifyatulia risasi kwa wakati na "kuvuruga mpango wa adui kutekeleza kitendo cha kigaidi."

Urusi inasema kwamba ndege hizo zilitumwa na Ukraine kutoka pwani karibu na Odesa na kwanza zilivamia "ukanda wa nafaka" na kisha kuelekea Sevastopol. Inadaiwa kwamba ndege hizo zisizo na rubani zilisafiri umbali wa kilomita 300-320, sawa na maili 170 baharini.

Huu ni umbali mrefu kwa ndege zisizo rubani kusafiri baharini.

Urusi inasema kwamba ndege hizo ziliundwa nchini Canada.

Ndege zisizo na rubani – ni nini?

Inajulikana kuwa Canada hutumia ndege zisizo na rubani kwa madhumuni ya kisayansi.

Kwa mfano, mnamo Januari, kampuni ya Canada ya JASCO Ilitumia ndege hizo kwa uchunguzi wa kisayansi baharini

Sensa za ndege hizo na kamera za video ziliweza kugundua mamalia wa baharini katika pwani ya Columbia na kutuma data hiyo kwa wachambuzi walio katikati ya ukaguzi huo.

Ndege zisizo na rubani za sakafuni zina miundo na sifa mbalimbali. Zinaweza kuonekana kama mashua ndogo.

Ndege isiyo na rubani iliyo mbele ya meli inaweza kuwa na vilipuzi, na kuigeuza kuwa silaha ya kukera. Kawaida zina mfumo wa ufuatiliaji wa video, utafutaji na mawasiliano mbali na kituo cha udhibiti wake

Kwa kweli, kwenye video ya shambulio hilo katika ghuba ya Sevastopol, iliyochapishwa kwenye vyombo vya habari, unaweza kuona jinsi boti zisizo na rubani "huwinda" meli za Urusi ili kuzishambulia na kusababisha uharibifu.

Rasmi, ni nchi chache tu zinazounda vifaa kama hivyo haswa kwa madhumuni ya kijeshi.

Kwa hivyo, miaka miwili iliyopita, Uturuki iliwasilisha mradi wake wa ndege zisizo na rubani zinazoitwa ULAQ.

Kifaa hiki kina vifaa vya kielektroniki na vituo vya rada kwa ajili ya kutambua na kufuatilia eneo inalolenga. Uzito wa drone hiyo ni tani 2, kasi yake ya juu ni hadi 65 km / h), na inaweza kusafiri hadi maili 215 baharini (yaani, hadi kilomita 400).

Boti hiyo isiyo na rubani pia ina uwezo wa kurusha makombora.

Mnamo Agosti mwaka huu, uzalishaji wa mfululizo wa ndege zisizo na rubani za Uturuki ulianza.

Marekani na Uingereza pia ziliripoti kuhusu utengenezaji wa ndege zao zisizo na rubani.

Andriy Ryzhenko, nahodha wa safu ya kwanza ya hifadhi ya Kikosi cha Wanamaji cha Ukraine, anasema kwamba vifaa hivyo tayari vinatumika sana, lakini bila utangazaji mwingi.

"Zinatumika sana, ingawa hazitangazwi. Huwezi kupata kwenye tovuti za Jeshi la Wanamaji la nchi yoyote kwamba wana mifumo kama hiyo. Yote ni ya operesheni maalum ya kuharibu malengo ya kijeshi yenye thamani zaidi katika kina fulani,"

Ndege zisizo na rubani za mataifa ya Magharibi

Tangu kuanza kwa uvamizi kamili wa Urusi, washirika wa Magharibi wamehamisha drones kadhaa za majini kwenda Ukraine. Hasa, Uingereza ilifanya hivyo hadharani.

Hata hivyo, ndege sita zisizo na rubani za REMUS-100 zilizotolewa na taifa hilo mwezi wa Agosti ni ndege ndogo zisizo na rubani za chini ya maji zinazotumiwa mahususi kwa kutegua mabomu.

Ndege hii isiyo na rubani, inayoonekana sawa na torpedo au manowari ndogo, yenye urefu wa m 1.6 tu, na uzani wa kilo 37, inaweza kupiga mbizi mita 100 na kutafuta migodi chini ya maji kwa masaa 10 pekee.

Kuhusu ndege zisizo na rubani, Marekani iliripoti uhamisho wa vifaa kama hivyo kuelekea mjini Kyiv mnamo Aprili. Katika kifurushi cha usaidizi wa ulinzi kutoka Pentagon, "ndege isio na rubani ya majini " ilitangazwa. Wizara ya Ulinzi ya Marekani haikuzungumza zaidi kuhusu mifano ya "zana" hizi.

Hata hivyo, inajulikana kutoka kwa vyanzo vya umma kwamba Marekani hutumia aina chache tu ya ndege zisio na rubani miongoni mwa walinzi wake wa pwani na vikosi vya majini.

Hizi ni, kwa mfano, Sea Hunter, Sea Hawk, Fleet, Saildrone Explorer na Ranger. Lakini zote ni kubwa kabisa na hazitumiki kama ndege zisizo na rubani za kamikaze.

Kwa hivyo, meli ya Sea Hunter isiyo na rubani, yenye urefu wa m 40, inaweza kukaa baharini kwa muda mrefu na kufuatilia meli za adui. Walakini, hakuna silaha za kukera kwenye bodi.

Baadhi ya mifumo ya anga isiyo na rubani pia hutolewa kwa Ukraine na serikali ya Ujerumani. Angalau katika orodha ya misaada ya kijeshi, ambayo ilitolewa kwa umma na mamlaka ya Ujerumani mnamo Oktoba 26, imeonyesha kuwa drones 2 za sakafuni zimehamishiwa Kyiv na uhamisho wa 8 zaidi unatayarishwa.

Hakuna maelezo juu ya nini hasa vifaa hivi ni nini.

Hapo awali, haikujulikana hadharani jiwapo Ujerumani ilikuwa ikikuza drones za sakafuni za kivita.

Shambulio hilo lilitekelezwa vipi?

Kuna ugumu unaotokea katika kuhakikisha udhibiti wa drones za sakafuni wakati wa shambulio la shabaha inayosonga.

Sio vigumu kifaa hicho kusalia juu yam aji kwa muda mrefu ili kutekeleza shambulio. Lakini kwa utekelezaji mzuri wa misheni, droni lazima iwe katika mawasiliano ya mara kwa mara na amri au mtu anayeidhibiti moja kwa moja.

"Hii inaweza kufanyika kwa msaada wa mawasiliano ya redio. Lakini kuna vikwazo vingi hapa, hasa, matumizi ya EW (vita vya redio-elektroniki) na upande wa Urusi, kuundwa kwa kelele, zinazoathiri ndege hizo , Yakovenko anaeleza.

Chaguo jingine ni matumizi ya teknolojia ya satelaiti kutangaza ishara kati ya droni na sehemu ya udhibiti.

Yakovenko anaamini kuwa chaguo hili lilitumika katika shambulio la meli huko Sevastopol.

Wataalamu kutoka Marekani wanakiri kwamba ndege zisizo na rubani za baharini zilifika sehemu fulani karibu na pwani ya Crimea kwa kutumia GPS, na hapo udhibiti wao ulikuwa tayari umechukuliwa na mdhibiti kwenye ufuo.

Pia kuna madai kwamba ni droni za angani ambazo zilisaidia waendeshaji kudhibiti kwa ustadi droni za sakafuni.

Mnamo Septemba 21, mamlaka ya uvamizi ya Sevastopol iliripoti ugunduzi na uharibifu wa droni ya sakafuni isiojulikana kwenye pwani.

Katika picha iliyochapishwa na vyombo vya habari vya ndani, inaweza kuonekana kwamba drone ni ndogo kwa ukubwa na ina umbo la kayak .

Wakati huo huo, eneo la kifaa sawa na antenna ya satelaiti inaonekana kwenye droni hiyo. Pia kwenye mwili wa mashua isiyo na rubani kuna kamera ya video, sensa ya mionzi na pengine vilipuzi

Wachambuzi wa chapisho maalum la NavalNews wanaamini kwamba hii ndiyo ndege mpya zaidi ya mashambulizi ya Ukraine, na ni vifaa hivyo vilivyotumika Oktoba 29 kwa shambulio la Sevastopol.

Kulingana na picha ya video ya shambulio la ndege isiyo na rubani ambayo imesambazwa kwenye vyombo vya habari, wanaamini kwamba vikosi vya Ukrain labda viliweza kuharibu safu kuu ya Meli ya Bahari Nyeusi ya Shirikisho la Urusi - frigate ya Admiral Makarov.

Rekodi zinaonyesha mashua ya mashambulizi inaikaribia kwa kasi meli ya aina hiyo.

Katika mkutano na waandishi wa habari mnamo Oktoba 31, Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kuwa boti za Ukraine zisizo na rubani ni hatari sio tu kwa jeshi, bali pia kwa meli za kiraia.

Kwa sababu zinapaswa kuwa na urefu wa mita 6 na kubeba takriban tani 500 za vilipuzi (kiongozi wa Kremlin ni wazi alifanya makosa, akimaanisha kilo 500).

Mchambuzi wa NavalNews, afisa wa zamani wa Jeshi la Wanamaji la Uturuki la Taifun Ozberk anahitimisha kuwa Urusi, ambayo zamani ilikuwa nchi yenye nguvu ya baharini, imepoteza uwezo wa kimsingi wa ulinzi wa bandari, akili bora na tathmini ya uwezo wa adui.

"Operesheni ya mashambulizi ya ndege isio na rubani" huko Sevastopol, anabainisha, itabadilisha mtazamo hatua zitakazopigwa na vikosi vya majini kote ulimwenguni.

"Katika mizozo ya siku zijazo, itakuwa ngumu zaidi kwa meli ambazo hazina mifumo madhubuti ya ulinzi na usalama, na makundi ya ndege zisizo na rubani yatakuwa mwiba kwa meli kubwa za kivita," mchambuzi anatabiri.

Sio shambulio la kwanza

Mashambulizi ya pamoja ya ndege zisizo na rubani za sakafuni na angani zilizofanywa karibu na pwani ya Crimea ni za kipekee. hathivyo, utumiaji wa ndege zisizo na rubani za majini au boti za kushambulia meli za adui ni mazoezi yaliyothibitishwa katika historia.

Hivi sasa, USA, Uchina, Israeli na Irani zinafanya kazi kwa bidii katika uundaji wa meli zote za meli zisizo na rubani.

Kwa upande wa mwisho, inaaminika kuwa ni Tehran ambayo inasambaza ndege zisizo na rubani kwa waasi wa Houthi nchini Yemen.

Kwa msaada wao, wanashambulia meli kubwa karibu na pwani ya adui yao wa kijeshi - Saudi Arabia.

Kwa hivyo, mnamo Desemba 2020, meli ya mafuta ilishambuliwa na ndege isio na rubani ya majini karibu na bandari ya Saudi ya Jeddah, na mnamo Januari 2017, frigate ya Jeshi la Wanamaji la Saudi Arabia ilipata shambulio kama hilo.

Tukio hili linachukuliwa kuwa kisa cha kwanza kilichothibitishwa cha matumizi ya vyombo vya juu vya ardhi visivyo na rubani na vilipuzi kushambulia chombo cha adui.

Msanidi wa Ukjraine anayehusika na vifaa kama hivyo, Yuriy Nikolenko, anasema kuwa teknolojia hii ni mustakabali wa migogoro ya silaha baharini. Kwanza kabisa, kwa sababu ya hali ya kifedha.

"Kwa mfano, frigate inagharimu makumi kadhaa ya mamilioni ya dola, ujenzi wake na mafunzo ya wafanyakazi huchukua miaka kadhaa. Muundo wake, ukarabati, ufungaji wa silaha, kuongeza mafuta pia hugharimu makumi ya mamilioni ya dola. Huku droni 10 zikigharimu dola chache. Masharti ya uundaji wao na gharama za uendeshaji hazilinganishwi hata kidogo."

Kwa hivyo, swali linatokea ikiwa ni sawa kuwekeza fedha kubwa katika ujenzi wa meli za kivita ambazo zinaweza kuharibiwa na droni za bei nafuu zaidi.

Kwa kuongezea, mtaalam huvutia umakini, akirudi kwenye mada ya "tukio la Sevastopol", ndege zisizo na rubani ziliweza kukaribia maeneo ya kuegeshwa meli za adui. Hii ina maana kwamba walishughulikia zaidi ya njia bila kutambuliwa.

Hii inazungumza juu ya ufanisi wao.

"Wao (Warusi) walizigundua pale tu walipoanza kushambulia moja kwa moja meli hatahivyo walikuwa wamechelewa tayari," Yuriy Nikolenko anaelezea.