Kwanini ni vigumu kwa baadhi ya viongozi wa Afrika kuondoka madarakani?

wdc

Chanzo cha picha, Getty images

Maelezo ya picha, Mkutano wa kilele wa viongozi wa ECOWAS mwezi Januari 2013 mjini Abidjan
    • Author, Isidore Kouwonou
    • Nafasi, BBC

Rais Macky Sall alisisitiza jana wakati wa ufunguzi wa mazungumzo ya kitaifa nchini Senegal nia yake ya kuondoka madarakani mwishoni mwa muhula wake mwezi Aprili 2.

Alipochaguliwa mwaka 2012 kwa muhula wa miaka saba na kuchaguliwa tena mwaka wa 2019 kwa miaka mitano.

"Afrika haihitaji wanaume wenye nguvu, lakini taasisi imara," Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alisema wakati wa ziara rasmi nchini Ghana, Julai 11, 2009.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ilijaribu kutatua tatizo la kukaa marakani kwa kuunda itifaki ya utawala bora na demokrasia mwezi Disemba 2001 - inataka muhula wa urais lazima uwe na ukomo.

Itifaki hii ni nyongeza kwa itifaki inayohusiana na utaratibu wa kuzuia, usimamizi, utatuzi wa migogoro, kudumisha amani na usalama ambao tayari ilikuwepo.

Lakini katika baadhi ya nchi, hasa ECOWAS, kuna marais wanaohudumu zaidi ya mihula miwili, kinyume na matakwa ya watu wao. Na katiba hufanyiwa marekebisho ili hilo liwezekane.

Tunaweza kutaja mfano wa Côte d'Ivoire, Togo, na Guinea, nchi ambazo marekebisho ya katiba yalianzisha maandamano yenye vurugu na vifo, majeraha na vifungo.

Pia unaweza kusoma

Alassane Ouattara, muhula wa tatu, Ivory Coast

gb

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alassane Dramane Ouattara, Rais wa Jamhuri ya Côte d'Ivoire yuko katika muhula wake wa 3

Alassane Dramane Ouattara, Rais wa Jamhuri ya Côte d'Ivoire, alichaguliwa tena kwa asilimia 94.27% Oktoba 2020 kwa muhula wa tatu ambao utakamilika mnamo 2025.

Kabla ya uchaguzi huo, mwaka 2017, aliwaahidi raia wa Ivory Coast kwamba hatagombea muhula mwingine, baada ya mihula wa pili ulioisha mwaka 2020.

Tamaa hii ya kugombea tena, ilizusha ghasia mbaya nchini Côte d'Ivoire, huku upinzani ukitoa wito wa kususia uchaguzi na kutokea uasi wa raia kwa sababu, muhula wa tatu wa Rais Ouattara ni kinyume cha katiba. Katiba ya Ivory Coast iliweka mihula miwili ya urais.

Mwaka 2020, marekebisho yalihusu vifungu 20 katika Katiba ya Côte d'Ivoire. Katiba hii awali inaeleza kwamba Rais wa Jamhuri anachaguliwa kila baada ya miaka mitano.

Maandamano kufuatia mabadiliko hayo yalisababisha vifo 85 na zaidi ya 500 kujeruhiwa.

Miaka 19 ya Faure Gnassingbé, Togo

c

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Faure Gnassingbé, Mkuu wa Jimbo la Togo, muhula wa 4
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Rais wa sasa wa Togo, Faure Gnassingbé, aliingia madarakani kufuatia kifo cha babake Gnassingbé Eyadéma mwez Februari 5, 2005.

Urithi huu kinyume cha katiba, upinzani ulisema wakati huo. Msururu wa maandamano yalipelekea zaidi ya watu 500 kuuwawa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Baada ya kuchaguliwa tena katika chaguzi mbili za urais (2010 na 2015) zilizopingwa na upinzani, Faure Gnassingbé alikabiliwa na maandamano makubwa dhidi ya utawala wake.

Maandamano haya yaliyoendelea hadi mwaka 2018 ya vyama 14 vya upinzani kuunda muungano, hayakufanikiwa kurejesha katiba katika muundo wake wa awali wa 1992.

Baada ya uchaguzi wa Disemba 2018 ambapo upinzani ulikataa kushiriki, Bunge lilirekebisha tena katiba, hasa ibara inayohusiana na uchaguzi wa Rais.

Ni wazi kwamba Faure Gnassingbé anaweza kugombea mwaka 2025, kulingana na katiba mpya. Nchi hiyo kwa sasa inatikiswa na mzozo wa kisiasa ambapo upinzani unaitaka ECOWAS na mashirika mengine ya Afrika na kimataifa kuingilia kati mzozo wa Togo.

Togo inajiandaa kwa uchaguzi wa wabunge utakaofanyika Aprili. Mwaka ujao uchaguzi wa urais utafanyika. Katiba katika hali yake ya sasa, inamruhusu Faure Gnassingbé kuwania muhula wa tano.

Blaise Compaoré urais miaka 17, Burkina-Faso

dc

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mkutano unaoongozwa na jeshi wa mawaziri wa AES

Blaise Compaoré, alikuwa rais wa Burkina-Faso kwa miaka 27. Alijiulu baada ya maandamano yaliyotokea Oktoba 30 na 31, 2014.

Maandamano hayo yalikuwa ni matokeo ya nia ya Rais Compaoré ya kutaka kurekebisha katiba ya nchi ili kugombea urais na kubaki madarakani. Tayari alikuwa kashachaguliwa mwaka 1991, 1998, 2005 na 2010.

Mwaka 2014, Blaise Compaoré alitaka kurekebisha ibara ya 37 ya katiba ambayo, tangu 2000, imeweka mamlaka ya urais kutoka miaka 5.

Oktoba 30, 2014, wakati kura katika Bunge hilo inapaswa kupigwa, bunge lilivamiwa na umati wa watu na Jenerali Honoré Traoré akatangaza kulivunja Bunge, na akachukua majukumu kama mkuu wa nchi.

Muhula wa tatu wa Alpha Cond

fdc

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa zamani wa Guinea, Alpha Condé alipinduliwa na mapinduzi Septemba 5, 2021.

Guinea leo inaongozwa na serikali ya kijeshi baada ya mapinduzi yaliyompindua Rais Alpha Condé mwezi Septemba 5, 2021. Kiongozi huyo, licha ya maandamano ya upinzani, alirekebisha katiba ya nchi yake ili kuwania kiti cha urais muhula wa tatu.

Maandamano ya kupinga muhula wa tatu wa Alpha Conde yalikandamizwa, pakatokea vifo na majeruhi.

Kwa shangwe kubwa watu walikaribisha mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na komando wa kikosi maalumu cha jeshi la Guinea kilichoongozwa na Kanali Mamadi Doumbouya, aliye madarakani kwa sasa.

Nchini Cameroon Paul Biya, mwenye umri wa miaka 90, alisherehekea miaka 41 madarakani mwaka jana, na Yuweri Mussévéni, mwenye umri wa miaka 80, miaka 38 yupo madarakani nchini Uganda.

Pia nchini Congo, Dénis Sassou N'Guesso, mwenye umri wa miaka 81, yupo madarakani tangu 1997. Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, mwenye umri wa miaka 82, yupo madarakani tangu 1979 nchini Equatorial Guinea.

''Viongozi wanaona ni jambo la kawaida kukaa zaidi ya miaka 40 madarakani na wakati mwingine kwa mfululizo wakipokezana kwa nasaba. Tabia hii imemea kwa viongozi hawa,'' anasema Nathaniel Olympio, rais wa Kituo cha masomo ya kimkakati cha Kékéli huko Afrika Magharibi.

“Tabia hii ya kung’ang’ania madaraka ni matokeo ya kulimbikiza madaraka mikononi mwa mkuu wa nchi, madaraka yanatekelezwa bila kikomo na bila uwajibikaji, pamoja ubadhirifu.''