Mambo 10 usiyoyajua kuhusu BBC inapoadhimisha miaka 100

Mwaka 1967, kipindi Dunia yetu-Our World ilianzisha historia.
Kipindi kilifanyiwa majaribio katika baadhi ya nchi kupitia setilaiti kabla ya kutangazwa kwenye televisheni.
BBC ilikuwa kituo cha kwanza kutangaza kwa ubora wa hali ya juu katika mwaka 1936.
Our world kilikuwa ni kipindi tofauti, kilijaribu kuonesha ni nini kinachotokea mubashara katika nchi za kila bara.
Lilikuwa ni jaribio la kwanza la kuunganisha dunia kwa njia ya setilaiti.
Wakati Uingereza ilichangia kwenye kipindi , Beatles walitumbuiza wimbo , All you need is love. Wimbo huu ukawa maarufu sana.
BBC ni Shirika kubwa duniani. Lilianzishwa tarehe 18 Oktoba 1922 mjini London. BBC ina historia ya muda mrefu, ya kusisimua na ya muda mrefu.
Kuadhimisha karne ya BBC, ngoja tuangalie baadhi ya matukio muhimu ya miaka iliyopita na jukumu muhimu katika safari ya BBC. Shirika la utangazaji la Uingereza-BBC limetimiza miaka 100.
1. Kituo cha kwanza cha redio
Baada ya baadhi ya vituo vya redio kufungwa katika siku za mwanzo, BBC ilizindua kituo chake cha kila siku cha redio mjini London, tarehe 14 Novemba 1922.
Kila jioni gazeti lilikuwa linakuja kutangazwa kwa kuzingatia habari zilizotolewa na mashirika mbali mbali ya habari.
Baada ya taarifa za magazetini, taarifa ya habari za hali ya hewa zilikuwa zinatangazwa. Taarifa iliyokuwa inaandaliwa na Huduma ya taifa ya hali ya hewa.
Arthur Burroughs alikuwa akisoma taarifa hiyo. Alikuwa akifanya kazi kama Mkurugenzi wa kipindi

Alikuwa anasoma habari kamili mara moja kwa haraka na kuisoma tena mara moja taratibu. Alikuwa anafanya hivi ili wasikilizaji waweze kuandika kile wanachokisikia.
2. Kuanzishwa kwa Idhaa ya Dunia
Tarehe 19 Desemba 1932, George V alitoa hotuba ya Siku ya Krismasi kwa Uingereza na kwa maeneo mengine ya dunia.
Katika hotuba hii, alitangaza uzinduzi wa idhaa hii . Idhaa hii ni huduma kwa wanaume na wanawake waliotenganishwa na majangwa, maeneo ya baridi na bahari.
Huduma ya himaya ya BBC ilizinduliwa siku ile. Sasa inaitwa Idhaa ya Dunia ya BBC ( BBC World Service.)

Idhaa ya dunia ya BBC ni huduma kubwa zaidi ya utangazaji kwa nchi, lugha na kwa idadi ya wasikilizaji.
BBC inatangaza mtandaoni, kupitia mitandao ya kijamii, Televisheni na redio katika takribani lugha 40.
3. Kinasa sauti cha BBC
Vinasa sauti vya BBC katika miaka ya 1930 vilikuwa ghali. Kwahiyo BBC ilishirikiana na kampuni inayoitwa Macroni kutengeneza vinasa sauti vyake.
Kuanzishwa kwa Aina A ya kinasa sauti katika mwaka 1934 kulileta mageuzi katika sekta ya utangazaji.

Aina hii ya kinasasauti ilitengenezwa na hatimaye kufahamika kama kinasa sauti cha BBC katika mfululizo wa maigizo na tamthilia.
4. BBC Idhaa ya Kiarabu – Idhaa ya kwanza ya lugha ya kanda
BBC Idhaa ya Kiarabu ilikuwa ndio lugha ya kwanza ya kikanda ya BBC kutangaza matangazo yake ya redio
Idhaa hii ilianzishwa mwaka 1938. Ahmed Kamal Sorur Efendi alikuwa 'mtangazaji mkuu' wa idhaa.
Kwa kuanzishwa kwake, Idhaa hiyo ilikuwa maarufu kwa haraka. Kwasababu Effendi alikuwa tayari ni maarufu katika Ulimwengu wa Kiarabu.

Idhaa kadhaa za aina hiyo za kikanda zilizinduliwa katika muongo uliofuata. Vipindi kadhaa vilianzishwa kwenye televisheni na redio.
Kitengo cha mtandao cha BBC kilianzishwa mwaka 1997. Wakati huo huduma za mtandao zilizinduliwa katika lugha nyingine pia.
Mitandao ya kijamii imefanya kitengo cha habari cha BBC – BBC News na Idhaa ya BBC ya Dunia kupatikana kwenye majukwaa mbalimbali.

Kwa sasa BBC inaangazia zaidi huduma ya habari kwa njia ya digitali.
5. Mwanamke wa kwanza mtangazaji wa BBC
Una Marson alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi mtangazaji wa BBC.
Una alikuwa mwenye asili ya Jamaica. Bado anafanya uandishi wa habari wa majira. Alianza kazi katika BBC mwaka 1939.

Mwanzo alikuwa msaidizi katika studio za Televisheni ya Alexandra Palace. Alijiunga na BBC kama mfanyakazi wa muda wote mwaka 1941.
Alikuwa anapenda sana ushairi. Msururu wake wa ushairi uliojulikana kama
Calling the West uliipatia BBC sauti ya mtu kutoka Caribean.
6. Mwisho wa vita vya pili vya Dunia
Tarehe 1 Mei, 1945, BBC iliripoti kuwa Hitler alikuwa amejiua. Kipindi cha jioni kilisimamishwa saa moja jioni. Katika siku ile, ujerumani ilijisalimisha kwa Italia. Tarehe 4 Mei, waliizingira Denmark na vita viliisha.
Wengi hawakuwa na uhakika kwa siku kadhaa zilizofuatia kwamba hili lilitokea.
Tarehe 7 Mei, watu wengi walikusanyika mbele ya Kasri ya ufalme wa Uingereza- Buckingham Palace.
Taarifa ambayo nchi yote ilikuwa inasubiri kwa miaka mitano haikuja mpaka mwisho.
Waingereza walikuwa wanasubiri kusikia kutoka kwa Wamarekani na Warusi kwamba wanazi wameangamizwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Saa kumi na mbili jioni BBC iliwaambia wasikilizaji kwamba Churchill hatazungumza siku ile. Halafu saa Moja na dakika 40 vipindi vyote vikasimamishwa na siku iliyofuata ilitangazwa kama ushindi.
Vita barani Ulaya vilikuwa vimeisha. Churchill alitoa tangazo siku iliyofuatia. Wengi walitaka kujua hilo. Watu walisherehekea siku ile.
BBC ilifanya vipindi maalumu kwa siku kumi zilizofuatia. Wakati ule, jumba la utangazaji lilikuwa na muonekano tofauti.
BBC TV ilifika kote duniani

Wimbo uliweka msingi wa kipindi maarufu kilichojulikana kama Live Aid, ambacho kilitangazwa katika mwaka 1985.
Pia Bob Jeldoff na Midge Ure walitumbuiza katika maeneo mbali mbali. Matukio haya yalifanyika kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ukame nchini Ethiopia.
Wakati ule BBC ilikuwa katika kipindi cha mafanikio makubwa. Ilikuwa ni chombo cha utangazaji cha televisheni kwa njia ya Setilaiti. BBC hutangaza kipindi mubashara kwa watazamaji milioni 400 katika nchi 60.
8. Vishchhatri alimuua mwandishi wa habari wa BBC
Mwandishi wa habari wa BBC aliuliwa na kifaa kinachofana na mwavuli. Jina lake lilikuwa ni Georgi Markov.
Tarehe 7 Septembea 1978, Markov alikuwa njiani kuelekea katika ofisi za utangazaji za BBC wakati huo- Bush House. Wakati ule mtu asiyejulikana akafungua kifaa hicho miguuni pake na kukimbia.

Chanzo cha picha, INTERNATIONAL SPY MUSEUM
Baada ya tukio hili, Markov aliugua sana. Ilibidi alazwe hospitalini. Aliwaambia wafanyakazi wenzake kuwa ujasusi wa Burgaria na ujasusi wa Urusi walimpa sumu.
Alifariki siku tatu baadaye. Alikuwa na umri wa miaka 49. Aliacha mke na binti yake mwenye umri wa miaka miwili.
Alikuwa akikosoa mara kwa mara Chama cha Kikomunisti cha Bulgaria. Kwahiyo, KGB na huduma za ujasusi za Bulgaria walishukiwa kwa muda mrefu katika kifo chake.
Jina la muuaji lilifichuliwa katika faili za polisi kama Picadilly. Lakini hawakupata haki ya kisheria hadi mwisho.
9. Mwanamichezo wa Afrika wa Mwaka
Taji hili lilitolewa kwa mwanamichezo bora wa Afrika. Lilijumuisha mchezaji wa soka wa Primia Ligi wa Liverpool Mohamed Saleh. Alipata taji hili mwaka 2018.

Tangu mwaka 2001, tuzo hili lilitolewa kwa wachezaji wa soka pekee. Katika mwaka 2021, tuzo hili hutolewa kama Mwananamichezo Bora wa Afrika wa Mwaka.
10. David Attenborough na Green Planet
David Attenborough alikuwa akifanya kazi katika BBC. Vipindi vya makala ya mazingira viliifanya sauti yake ifike kote duniani.
Blue Planet, Life collection na Natural World vimetazamwa na mamilioni ya watu hadi sasa. Alipokea tuzo mbalimbali kwa kipindi chake.
David Attenborough alianza kufanya kazi BBC katika miaka ya 1960. Wakati huo alikuwa afisa utawala wa ngazi ya juu katika BBC. Baadaye akapanda kwenye wadhifa wa Afisa wa Udhibiti wa vipindi vya BBC

Chanzo cha picha, David Attenborough
Alitunukiwa tuzo ya 'Champion of the Earth' na Umoja wa Mataifa kwa kazi yake katika kuwaelimisha watu.
Msururu wake wa vipindi -Green Planet ni maarufu sana. Kipindi hiki huelezea jinsi miti inavyoishi katika mazingira tofauti ya hali ya hewa kote duniani













